Ingawa intaneti inatupata taarifa wakati tunaihitaji, mara nyingi tunapata taarifa za uongo kushinda za ukweli, na tukizungumzia njia za uzuiaji mimba na homoni, ni muhimu kutambua uongo ili watu waweze kufanya maamuzi kutokana na ukweli wa sayansi.
Tuzungumunzie uongo kuhusu utumiaji wa homoni kama njia ya kuzuia mimba
Uongo: Utaongeza uzani
Wanawake wengi hawapati matatizo ya ongezeko la uzani kutoka kwa homoni iliyo kwenye njia ya uzuiaji mimba wanayotumia. Ongezeko la uzani ni jambo la asilia inayoletwa na uzee na hali zingine za maisha, na kwa vile mabadiliko haya yanafanyika kiasilia, wanawake wengi huamini kuwa ni kwasababu ya homoni. Hata hivyo, tafiti za kimatibabu zinaonyesha kwamba mabadiliko haya hayana uhusiano na njia za uzuaji mimba.
Idadi ndogo ya wanawake wataona mabadiliko kwenye uzani, ambayo itakoma wanapowacha kutumia njia za uzuiaji mimba na uzani wao wa kawaida utarudi. Bado chanzo cha hiki hakijulikani.
Uongo: Zinasababisha saratani
Tafiti za kisayansi zinaonyesha kwamba saratani ya matiti hupata wanawake wengi kidogo ambao wamewahi tumia tembe za uzuiaji mimba kushinda wanawake ambao hawajawai kutumia tembe hizo.Lakini hili halimaanishi kwamba kuna uhusiano kati ya saratanai ya matiti na utumiaji wa tembe za uzuiaji mimba au kwamba saratani haitakuwa ndani ya mtu kabla yeye kuanza kutumia tembe
Vinginevyo, kilicho thibitishwa ni kwamba utumiaji wa tembe hupunguza hatari ya kupata saratani ya ndani ya mji wa mimba, saratani ya ovari, saratani ya utumbo mpana na saratani ya rektamu.
Uongo: Husababisha utasa
Kwasababu ni njia ya homoni, sio wanawake wote wanaweza kushika mimba mara tu baada ya kuwacha kutumia njia za uzuiaji mimba. Kwa kawaida, huchukua siku chache kabla mzunguko wa hedhi kurudi sawa na mwanamke ashike mimba, lakini pia kuna visa ambavyo miezi hupita kabla ya mzunguko wa hedhi kurudi sawa. Kumbuka kwamba kila mtu ni tofauti na tafiti zinaonyesha kwamba hakuna shida ya kupata mimba kwa wanawake ambao wametumia njia za uzuiaji mimba za kumeza kwa muda mrefu .
Uongo: Zinaweza kufikia watoto wachanga kupitia maziwa ya mama
Uongo mtupu! Imethibitishwa kisayansi kwamba utumiaji wa njia za uzuiaji mimba zenye homoni hauathiri uwingi au mchanganyiko wa maziwa au kusababisha kasoro yoyote kwa mtoto mchanga. Madhara moja tu ambayo estrojeni inaweza kuleta ni kupunguka kidogo kwa maziwa, lakini haileti mabadiliko kwa viini lishe vya maziwa.
Uongo: Wanawake vijana hawapaswi kutumia njia za uzuiaji mimba zenye homoni.
Njia za uzuiaji mimba zenye homoni zinaweza kutumika na mwanamke yeyote, hakuna umri wa juu kabisa au chini kabisa wa kuzitumia. Hata taasisi nyingi za kimatibabu kama vile Shirika la Afya Ulimwenguni, zinapendekeza matumizi ya njia za uzuiaji mimba kwa wasichana vijana,ikiwemo wale wanaonyonyesha, kwasababu hii ni njia fanisi ya uzazi wa mpango.
Tunapendekeza kwamba wakati unazingatia kutumia njia za uzuiaji mimba, tembelea daktari ambaye atakushauri kuhusu njia itakayo kufaa kulingana na historia yako ya kimatibabu na hali yako.
Ikiwa una maswali zaidi, wasiliana nasi kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii: Facebook, Instagram na Twitter, au tutumie maswali yako kupitia barua pepe kwenye info@findmymethod.org.
References:
- Contraception: Do hormonal contraceptives cause weight gain?, Institute for Quality and Efficiency in Health Care, June, 2017, https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK441582/
- Oral Contraceptives and Cancer Risk, National Cancer Institute, February, 2018, https://www.cancer.gov/about-cancer/causes-prevention/risk/hormones/oral-contraceptives-fact-sheet
- Prolonged use of oral contraception before a planned pregnancy is associated with a decreased risk of delayed conception, Human Reproduction, Volume 17, Issue 10, October 2002, https://academic.oup.com/humrep/article/17/10/2754/607778
- Optimizing maternal and neonatal outcomes with postpartum contraception: impact on breastfeeding and birth spacing, Aparna Sridhar and Jennifer Salcedo, January, 2017, https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5237348/
- Contraception in adolescence, World Health Organization, 2004, https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/42901/9241591447_eng.pdf;sequence=1