Njia 5 za kupunguza uwezekano wa njia za uzuiaji mimba kufeli na za kuzuia mimba.

Njia 5 za kupunguza uwezekano wa njia za uzuiaji mimba kufeli na za kuzuia mimba.

Wengi wetu tumesoma na kutazama hadithi ya Cinderella; haswa ile sehemu alikimbia kutoka kwenye sherehe kwasababu ilifika saa sita usiku na nguvu ya juju iliotumika ilikuwa karibu kuisha. Kwa ile haraka ya kukimbia, aliwacha kiatu chake cha glasi. Mwana mfalme alianza kumtafuta na kuwauliza wasichana wote waliodai kiatu kilikuwa chao wakijaribu; haikutosha mwingine, ila Cinderella, kwani kiatu kilikuwa chake.
Njia za uzuiaji mimba huwa hivyo pia. Kuchagua njia ya uzuiaji mimba kulingana na watu wengine sio bora, na huenda njia hiyo ikafeli. Idadi kubwa ya mimba zisizopangwa– 42,870,000 duniani-hutokea kwa sababu ya kutotumia njia za uzuiaji mimba na pia kwa sababu ya njia ya uzuiaji mimba iliyotumika kufeli. Habari nzuri ni kuwa  mimba 82,080,000 zisizopangwa zimezuiliwa duniani kote kwa matumizi ya njia za uzuiaji mimba.

Cropped shot of a young woman taking a pregnancy test at home

Kufeli kwa njia za uzuiaji mimba ni nini?

Kufeli kwa njia za uzuiaji mimba hutokea wakati mwanamke anashika mimba licha ya kuwa anatumia njia ya uzuiaji mimba. Kuna aina mbili ya viwango vya kufeli kwa njia za uzuiaji mimba:

1) Kiwango cha  Kufeli kwa matumizi ya kawaida- hili linafanyika ikiwa hautumii njia za uzuiaji mimba kama vile ulivyoagizwa. Kutumia tena kondomu iliyokuwa imetumika tayari wakati maagizo yanasema uitupe baada ya kuitumia mara ya kwanza; kutomeza tembe za uzuiaji mimba kila siku; kuingiza diaframu vibaya; kuvaa kondomu wakati uko karibu kumwaga ni mifano ya viwango vya kufeli kwa matumizi ya kawaida ya njia za uzuiaji mimba.

2) Kiwango cha kufeli kwa matumizi bora- Hili linafanyika ikiwa unatumia njia ya uzuiaji mimba vizuri kwa kufuata maagizo lakini bado unashika mimba. Umewahi kuona ile picha ya mtoto aliyezaliwa akiwa ameshikilia kidude cha IUD? Kuna njia za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kufeli hata ukizitumia vizuri; kama tu vile kamba za chombo za kusikilizia zinajikunjakunja, licha ya bidii tunayoweka zisikunjike.

hand holds male condom, contraceptive method and also used to control sexually transmitted diseases

Ni muhimu kusema kwamba kufeli kwa njia za uzuiaji mimba sio sawa na utoaji mimba uliofeli. Utoaji mimba uliofeli ni ile hali ya mimba kuendelea kukuwa hata baada ya kujaribu kuitoa.

Kwa hivyo mtu hupunguza aje uwezekano wa kufeli kwa njia za uzuiaji mimba? Hatua unazoweza kuchukua ni:

1) Pata habari iliyo thibitishwa

Mambo mbalimbali kama vile umri, uzani, na mtindo wa maisha hutumika kutambua njia ya uzuiaji mimba itakayokufaa zaidi. Unaweza kuwa unanunua kondomu kwa urahisi, kumbe una mzio wa ulimbo wa mpira (latex); hautaki kuwashwa au kuhisi uchungu ukeeni, sivyo? Na ndio maana ni muhimu kufanya maamuzi bora.

Focused Indian woman using laptop at home, looking at screen, chatting, reading or writing email, sitting on couch, serious female student doing homework, working on research project online

Kuna watoaji huduma wengi wa afya ya kizazi wanaopatikana mtandaoni, ambao wanaweza kukusaidia kufanya maamuzi. Utatumia muda mfupi na kupata huduma bora.

2) Njia inayojulikana kama Double Dutch

Hili halimaanishi njia ya kuruka kamba. Inamaanisha kutumia njia mbili za uzuiaji mimba kwa wakati mmoja.

Mfano wa njia hii, ambao hujulikana kama mchanganyo wa njia za uzuiaji mimba, ni kama kutumia kondomu pamoja na dawa ya kuuwa mbegu za kiume (spermicide). Lakini ni muhimu kupata ushauri wa mtoaji huduma za afya ya kizazi au upate habari mtandaoni kutoka kwenye tovuti zilizothibitishwa za huduma za afya ya kizazi kwasababu unahitaji kuhakikisha ikiwa njia mbili tofauti zinaweza kutumiwa pamoja. Kwa mfano, kutumia kondomu ya kiume na ya Kike kwa pamoja kunaweza kusababisha msuguano na kuzifanya ziraruke.

3) Matumizi bora kila mara

Vyanzo vya kawaida vya mimba zisizopangwa ni kama matumizi mabaya ya njia za uzuiaji mimba na kutotumia kabisa njia ya uzuiaji mimba. Kupata tu njia ya uzuiaji mimba haitoshi kuzuia mimba; lazima utumie njia hiyo ya uzuaji mimba vizuri na kila mara  ili uzuie mimba.

Closeup shot of a couple holding hands during a consultation with a doctor

Kufuata maagizo unayopewa na mhudumu wa afya ya kizazi au kutoka kwa tovuti za afya ya kizazi zilizothibitishwa kunaweza kupunguza uwezo wa njia ya uzuiaji mimba kufeli, kwasabu hizo hufeli ikiwa hazijatumiwa vizuri.

4) Maamuzi mazuri

Mtu, tumwite A, anatumia tembe za kuzuia mimba na mtu mwingine B pia anaamua kwamba tembe ni bora kwake, bila kuzingatia kwamba pia anastahili kujikinga magonjwa ya zinaa. Usisahau mambo ya kujikinga magonjwa ya zinaa, kwasababu sio uzuiaji wa mimba tu hutufanya tutumie njia za uzuiaji mimba.

Ukihitaji njia za uzuiaji mimba zitakazo kinga hadi magonjwa ya zinaa, jaribu njia zinazozuia manii kuingia ukeni. Ukizihitaji kuzuia mimba, chagua njia zilizo bora kwa mwili wako. Na ukihitaji kukinga zote mbili, tumia njia mbili kwa wakati mmoja.

5) Njia ya uzuiaji mimba ya ziada

Tukichelewa kidogo na tuwachwe na ndege tuliopanga kuabiri, huwa tunatafuta mpango mbadala wa kusafiri. Hili pia hufanyika wakati tunapanga kuhudhuria sherehe; tunakuwa na chaguo mbili ya mavazi, kujitayarisha ikiwa kitu kitaenda kinyume na matarajio.  Mbona tusiwe na mpango mbadala pia kwa maisha ya ngono? Kondomu ikivunjika? Au usahau kumeza tembe na ufanye ngono?

Kwa hali kama hizi, tunastahili kukuwa na njia ya uzuiaji mimba ya ziada ambayo bado itatusaidia kuzuia mimba baada ya ngono.Hili linaitwa njia ya dharura ya uzuiaji mimba na inapatikana kupitia tembe au chombo cha IUD (ambacho unaweza kuendelea kutumia kwa muda mrefu).

Cropped shot of an unrecognizable teenage girl drinking medication

Tofauti kati ya njia ya uzuiaji mimba ya ziada na njia zinazochanganywa ni kuwa njia za ziada zinatumika baada ya njia ingine kufeli, wakati njia ya mchanganyo inamaanisha mtu anatumia njia zaidi ya moja kwa pamoja kwa wakati mmoja.

Kwahivyo, wakati mwingine ukitaka kuchagua njia ya uzuiaji mimba, zingatia haya. Njia za uzuiaji mimba zinaweza feli na kukuweka katika hali usiyoitarajia; kwahivyo ni jambo la busara kujaribu kuzuia haya kutokea.

Je, una jambo la kusema?Wacha ujumbe wako hapa chini, wasiliana nasi kwenye kurasa zetu za mitandao ya  kijamii: Facebook, Instagram na  Twitter u tutumie barua pepe kwenye info@findmymethod.org. Kwa taarifa zaidi kuhusu njia za uzuiaji mimba, tembelea  findmymethod.org

Kuhusu mwandishi: Amos Sanasi ni mdemografia, na mtaalamu wa maswala yanayohusiana na ngono na pia mwanzilishi wa jina la  rajamu la mambo chanya kuhusu ngono la kwanza nchini Nigeria  Revaginate NG ambalo linatoa taarifa za kina kuhusu ngono na vifaa vya ngono, haswa kwa watu walemavu. Yeye huandika kwenye akaunti ya twitter @thesanasi