Nilitolewa bitana za mji wa mimba (endometrial ablation) na ninawasiwasi kuhusu kupata mimba. Je, ufungaji uzazi ni wazo nzuri?

Baada ya kuharibu mji wa mimba, uwezo wa kushika mimba huwa chini kabisa, na pia haipendekezwi. Hata vivyo, inaweza kufanyika. Wanawake walioharibiwa mji wa mimba wanastahili kutumia njia za uzuiaji mimba hadi baada ya komahedhi. Hata ikiwa kuna uwezekano wa mimba baada ya utaratibu huu, mimba baada ya utaratibu huu inaweza kuwa na matatizo mingi, kwahivyo, usifanye ufungaji uzazi hadi uwe na uhakika kwamba hutaki watoto au watoto zaidi. Ufungaji uzazi unaweza kuwa chaguo nzuri kama uliharibiwa mji wa mimba na hautaki wasiwasi wa mimba isiyopangwa.


References:

  1. World Health Organization Department of Reproductive Health and Research and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (2018) Family Planning: A Global Handbook for Providers. Baltimore and Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/260156/9780999203705-eng.pdf?sequence=1