IUD yangu ilitoka. Kuna uwezekano gani hili litafanyika tena?

Kutoka kwa IUD kunawezekana kwa asilimia 2-10 ya wanawake ndani ya mwaka wa kwanza wa kuingizwa. Kutoka kunawezekana zaidi kwa wanawake ambao:

  • Wana umri chini ya miaka 20
  • Wana historia ya kuwa na hedhi nzito au hedhi iliyo na maumivu makali.
  • Waliwekewa IUD punde baada ya kujifungua au mimba ilitoka wakati wa trimesta ya pili (miezi 4-6)

Kipande cha IUD kutoka kunaweza kumaanisha kwamba IUD haikuingia sawa: Pengine ilikuwa chini sana kwenye mji wa mimba na ikatoka. Hili linaweza kuwa lilifanyika wakati wa kuingizwa au inaweza kuhusiana na umbo la mji wa mimba kama vile ukubwa,pembe, au kuwepo na uvimbe (fibroids) ambazo zinaweza kubadilisha umbo. Kwa wanawake ambao IUD ilitoka, kuna uwezekano mkubwa kwamba IUD ya pili pia itatoka- Kwa kiwango cha asilimia 20 (hadi asilimia 30 kwa tafiti zingine)[1].

Bado haiendi sawa? Ikiwa unapenda urahisi wa kutumia IUD, lakini una matatizo ya IUD kutoka, unaweza kujaribu kutumia njia ya vipandikizi-chaguo linalofanya muda mrefu na la kuhitaji kazi ndogo ya utunzaji.

Jaribu njia tofauti: Vipandikizi


References

    1. Madden T et al. “Association of age and parity with intrauterine device expulsion.” Obstetrics and Gynecology, 2014, 124:718. http://dx.doi.org/10.1097/AOG.0000000000000475 Accessed March 2024.

>