IUS yangu ilitoka. Kuna uwezekano gani hili litafanyika tena?

Kutoka kwa IUS kunawezekana kwa asilimia ndogo ya wanawake ndani ya mwaka wa kwanza wa kuingizwa. Kutoka kunawezekana zaidi kwa wanawake ambao[1]:

  • Hawajawahi kushika mimba
  • Wana umri chini ya miaka 20
  • Wana historia ya kuwa na hedhi nzito au hedhi iliyo na maumivu makali.
  • Waliwekewa IUS punde baada ya kujifungua au mimba ilitoka wakati wa trimesta ya pili (miezi 4-6)

Kipande cha IUS kutoka kunaweza kumaanisha kwamba IUS haikuingia sawa: Pengine ilikuwa chini sana kwenye mji wa mimba na ikatoka. Hili linaweza kuwa lilifanyika wakati wa kuingizwa au inaweza kuhusiana na umbo la mji wa mimba kama vile ukubwa,pembe, au kuwepo na uvimbe (fibroids) ambazo zinaweza kubadilisha umbo. Kwa wanawake ambao IUS ilitoka, kuna uwezekano mkubwa kwamba IUS ya pili pia itatoka [2].

Bado haiendi sawa? Ikiwa unapenda urahisi wa kutumia IUD, lakini una matatizo ya IUD kutoka, unaweza kujaribu kutumia njia ya vipandikizi-chaguo linalofanya muda mrefu na la kuhitaji kazi ndogo ya utunzaji.

Jaribu njia tofauti: Vipandikizi


References

  1. Nelson, A. L., & Massoudi, N. (2016). New developments in intrauterine device use: focus on the US. Retrieved from https://www.dovepress.com/new-developments-in-intrauterine-device-use-focus-on-the-us-peer-reviewed-fulltext-article-OAJC
  2. World Health Organization. (2016). Selected practice recommendations for contraceptive use. Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/252267/9789241565400-eng.pdf?sequence=1