Chagua chochote kinazokufaa au tumia maswali yetu kuhusu uzuwiaji mimba.
Tumia vichungi vyetu vya matibabu na mtindo wa maisha ili kubaini mbinu za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa na kisha ulinganishe chaguo zilizotolewa ili kufanya uamuzi unaofaa zaidi.
Njia zinazoingiana na mapendeleo yako
“Pata Njia Yangu” huonyesha yaliyokusudiwa kwa sababu ya habari tu na haihusiani na shirika la matibabu.
IUD ya Homoni
IUD yenye homoni ni kifaa kidogo chenye umbo wa herufi T cha plastiki ambacho kinaingizwa kwenye mji wa mimba ili kuzuia mimba.
GunduaIUD bila homoni
IUD bila Homoni ni kifaa kidogo chenye umbo wa herufi T cha plastiki na shaba ambacho kinaingizwa kwenye mji wa mimba ili kuzuia mimba.
GunduaKipandikizi cha Kudhibiti Uzazi
Kipandikizi cha kuzuia mimba ni kijijiti kidogo chembamba cha projestini ambacho kinaingizwa kwenye sehemu ya juu ya mkono ili zuia mimba.
GunduaTembe yenye projestini pekee (Tembe ndogo)
Tembe yenye projestini pekee ya kuzuia mimba ni tembe ndogo yenye homoni moja ya kuzuia mimba.
GunduaTembe mchanganyo ya uzuiaji mimba
Tembe Mchanganyo ya kuzuia mimba ni tembe ndogo yenye dozi ya kila siku iliyo na homoni mchanganyo, iliyowekwa kwenye kifurishi cha kila mwezi, ili kuzuia mimba.
GunduaSindano ya kuzuia mimba
Sindano ya uzuiaji mimba ni majimaji iliyo na aina bandia ya homoni zinazopatikana katika mwili wa mwanamke. Inadungwa ndani ya mwili ili kuzuia mimba.
GunduaKiraka
Kiraka cha uzuiaji mimba ni kitu chembamba, chenye umbo wa mraba cha sentimita 5 kinachofanana na Band-Aid na kilichobeba homoni za projestini na estrojeni. Kinabandikwa kwa mwili ili kuzuia mimba.
GunduaPete ya Kudhibiti Uzazi
Pete ya uke ni pete ndogo, inayopinduka ambayo inaingizwa ndani ya uke kama njia ya kuzuia mimba.
GunduaNjia za dharura za uzuiaji mimba tembe za Asubuhi ya kufuata
Tembe ya dharura ya kuzuia mimba inatumiwa kuzuia mimba baada ya ngono isiyo salama.
GunduaKondomu za nje
Kondomu ya nje ni kifuniko ambacho kinavaliwa kwenye uume uliosimama ili kuzuia mimba na maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
GunduaKondomu za ndani
Kondomu ya ndani ni ala ambayo inavaliwa ndani ya uke ili kuzuia mimba na maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
GunduaSponji ya uzuiaji mimba
Sponji ya uzuiaji mimba, ni kifaa cha plastiki nyeupe yenye unyevu ambacho kinaingizwa ndani ya uke kabla ya ngono ili kuzuia mimba.
GunduaKofia ya shingo ya kizazi
Kofia ya Shingo ya kizazi ni kofia ya ulimbo wa mpira au plastiki ambayo inaingizwa ndani ya uke kuzuia manii kuingia ndani ya mji wa mimba.
GunduaDayaframu ya kuzuia mimba
Dayaframu ni kijikombe chenye kina kifupi cha umbo wa kuba kilicho na mzingo laini inayonyumbulika, ambacho kinawekwa juu ya shingo ya kizazi kabla ya kufanya ngono ili kuzuia mimba.
GunduaDawa ya kuua manii
Dawa ya kuua manii ni kemikali au dawa inayozuia mimba kwa kuua manii kabla ikutane na yai kwa urutubisho.
GunduaKufunga mirija ya uzazi
Kufunga mirija ya uzazi ni kuziba kwa njia ya kimatibabu mirija ya uzazi ili kuzuia mimba.
GunduaVasektomi
Vasektomi ni taratibu ya upasuaji ambapo mirija ya kubeba manii zinazibwa ili kuzuia mimba. Mwanamume bado anaweza kumwaga manii, lakini shahawa haina manii.
GunduaNjia za uelewa wa uzazi
Njia za uelewa wa uzazi zinajumuisha uzuiaji mimba kwa kuweka rekodi za mzunguko wa hedhi yako ili kubaini siku ambazo unaweza kushika mimba na uepuke ngono siku hizo.
GunduaMbinu ya kunyonyesha kipindi hakuna hedhi (LAM)
Kunyonyesha Kipindi Hakuna Hedhi (LAM) ni njia asili ya uzuiaji mimba kwa muda mfupi ambayo inahusisha kumnyonyesha mtoto kikamilifu bila kumpa vyakula vingine au kunyonyesha karibu kikamilifu ndani ya miezi sita baada ya kujifungua, wakati ambao hedhi yako haijarudi.
GunduaMbinu ya kuchomoa uume (kuvuta nje)
Mbinu ya kuchomoa uume ni mbinu ya mwanamume kuvuta nje uume kwa saa ili kuzuia manii kuingia kwa mwili wa mwanamke.
GunduaKujinyima ngono
Kuepuka ngono ni kuchelewesha au kuepuka shughuli zote au baadhi za shughuli za ngono.
GunduaMaswali elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba
Je, unahitaji usaidizi zaidi kuchagua njia yako bora? Jibu maswali yetu elekezi kwa mbinu za kuzuia mimba.
Jibu maswali machache rahisi, na kulingana na majibu, tutapendekeza chaguo za uzuiaji mimba ambazo zinaweza kukufaa.