Je, tembe itaniletea saratani ?

Tembe haikuletei saratani. Kwa visa vichache sana, wanawake wanaweza kupata tatizo la damu kuganda. Hatari ya damu kuganda wakati unatumia tembe iko chini kuliko hatari ya damu kuganda ukiwa na mimba. Wanawake wengine wana matatizo za kiafya ambayo humaanisha hawafai kutumia tembe.Ukiwa mwenye afya, tembe za kuzuia mimba ziko salama. Zinaweza kukusaidia kwa shida wakati huu (kama anemia inayosababishwa na hedhi nzito) na baadaye maishani (zinaweza kukukinga dhidi ya aina zingine za saratani)