Mbona natokwa na damu kabla na baada ya hedhi ?

Ikiwa umeanza kutumia tembe ndani ya miezi michache iliyopita, jaribu kuvumilia-shida hii itaisha yenyewe. Hakikisha kwamba unameza tembe wakati sawa kila siku bila kukosa siku moja na kumeza mbili pamoja siku ingine.Kukosa kumeza tembe au kumeza tembe mbili pamoja kunaongeza uwezekano wa kutokwa matone ya damu.Bado haiendi sawa? Ikiwa umekuwa ukitumia tembe kwa miezi michache, unazitumia sahihi, na bado unatokwa matone ya damu, basi zingatia njia mpya. Pia unapaswa kupimwa magonjwa ya zinaa na mimba, ili kuhakikisha sio hizo zinasababisha utokwaji wa damu.
Jaribu njia tofauti: kiraka; pete; sindano