Na nikisafiri niende ukanda wa muda tofauti? Ninapaswa kubadilisha saa ya kumeza tembe?

Kuna chaguo tofauti [13]:
Chaguo la 1: Tumia saa za nchi yako

Unahitaji kujua saa za nchi yako na umeze tembe kwa hizo saa. Kwa mfano, Ukiishi mji wa Mexico na usafiri uende Morocco ambayo ni masaa 6 mbele, unastahili kumeza tembe zako masaa 6 baadaye kuliko kawaida kwa siku. Kwahivyo, ukiwa unameza tembe zako saa tatu asubuhi ukiwa Mexico, zimeze saa tisa alasiri ukiwa Morocco.
Ikiwa uliweka king’ora kwenye simu kikukumbushe saa ya kumeza tembe, hakikisha umekibadilisha inavyotakikana ukiwa safarini.

Chaguo la 2: Kufuata ukanda wa muda mpya

Ikiwa rahisi zaidi, au ikiwa unahamia eneo lingine kwa muda mrefu, unaweza badilisha mpangilio wako wa kumeza tembe, bora usimalize masaa 24 bila kumeza tembe.Kwahivyo, ukiishi mji wa Mexico na uende Morocco na unataka kuendelea na mpangilio wa saa tatu asubuhi, ni sawa kabisa kumeza tembe zako saa tatu asabuhi, saa ya Morocco,( masaa 18 baada ya tembe yako ya mwisho Mexico).

Ikiwa unasafiri kwa muda mrefu na utahitaji kifurushi kingine cha tembe ukiwa safarini, usisahau kuibeba kwenye begi lako. Ikiwa ulilazimishwa kusafiri ghafla, na hukupata nafasi ya kubeba tembe zako (k.m uko maeneo ya msiba), jaribu kutafuta mtoaji wa mtaa wa huduma za afya au mtoaji wa huduma za afya ya jamii punde iwezekanavyo kwenye eneo lako jipya. Tumia mbinu za asilia za kuzuia mimba wakati ambao bado huwezi pata njia zingine kama kondomu.

Bado haiendi sawa? Ikiwa wewe husafiri sana na unapenda njia ya homoni, pengine ungependa kubadilisha njia utumie pete au kiraka ili usiwe na wasiwasi kuhusu kanda za muda. Ukitaka kusahau kabisa mambo ya kupiga hesabu kanda za muda, chunguza vipandikizi au IUD.

Jaribu njia tofauti: vipandikizi;IUD kiraka; pete