Nilikosa kumeza tembe, au nilimeza tembe kuchelewa. Nifanye nini?

Meza tembe yako ya kufuata punde tu unapokumbuka, na utumie njia ingine kwa siku 7 baada ya hapo. Ikiwa ilisahau kumeza tembe bila homoni wa wiki ya 4,tupa hio tembe bila homoni kwa hiyo siku na rudi kwenye mpangilio siku ifuatayo.Ikiwa umefanya ngono tangu uende nje ya mpangilio wako wa kumeza dawa, na ni ndani ya siku 5 zilizopita, zingatia kutumia njia ya dharura ya kuzuia mimba.