Je,napaswa kuwa na wasiwasi juu ya damu kuganda?

Uko na hatari mdogo mno wa kupata tatizo la kuganda damu wakati unatumia tembe. Hata hivyo, kuna hali za kijeni au za kimatibabu ambazo zinaongeza hatari ya kupata tatizo la damu kuganda.Ukiwa na historia ya tatizo la damu kuganda au wasiwasi maalum kuhusu tatizo la damu kuganda, uliza anayekupa njia za kuzuia mimba kama kweli tembe ni chaguo bora kwako.