Je, njia za uzazi wa mpango huathiri vipi hedhi?

Vidhibiti mimba vya homoni hutumia ama projestini au estrojeni, au zote mbili ili kuzuia mimba kutokea, na homoni hizi pia ni muhimu katika mzunguko wa hedhi [1]. Ni mantiki basi kwamba uzazi wa mpango wa homoni utaathiri hedhi zako.Kulingana na aina ya uzazi wa mpango unaotumia, unaweza kusababisha kutokwa na damu nyepesi au nzito na pia unaweza kuathiri urefu wa hedhi yako [2]. Pia, mifumo ya kutokwa na damu huwa inabadilika kadiri muda unavyosonga.