Na ikiwa nataka kushika mimba?

Kuna uwezo utachelewa kushika mimba punde baada ya kutoa vipandikizi.Lakini wanawake wengi hushika mimba haraka baada ya kuwacha kutumia vipandikizi. Ikiwa hutaki kushika mimba, anza kutumia njia ingine baada ya kutoa vipandikizi. Kulingana na mwili wako, unaweza kungoja hadi miezi 2 kabla ya kupata hedhi yako ya kawaida baada ya kutoa vipandikizi.