Je, kuingiziwa IUD kutaumiza?

Uchungu mtu anayohisi wakati IUD inaingizwa itakuwa tofauti kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kwa bahati mbaya, hakuna dawa ya kumeza ili kufanya uingizaji uwe na uchungu mdogo.
Unaweza jaribu kumeza ibuprofen kabla ya uingizaji na uhakikishe IUD inaingizwa wakati shingo ya uzazi uko wazi, kama vile wakati wa hedhi au kupevuka kwa yai. Hata ikiwa kutakuwa na uchungu, itafaa miaka ya kufanya ngono bila kushika mimba [1].


References

  1. Family Planning NT. (2016). Intra Uterine Contraceptive Device (IUD or IUCD). Retrieved from http://www.fpwnt.com.au/365_docs/attachments/protarea/IUD-46c2853c.pdf