Maambukizi ya njia ya mkojo ni nini?

Ambukizo la njia ya mkojo lijulikanalo kama UTI, hurejelea maambukizi ama kwenye kibofu, mrija wa mkojo (bomba linalosafirisha mkojo kutoka kwenye kibofu chako nje ya mwili wako), au figo. Kawaida, UTI husababishwa na bakteria wanaosafiri hadi kwenye kibofu cha mkojo na hata wakati mwingine kwenye figo. Wanawake huwa na uwezekano mkubwa wa kupata UTI kwa sababu mrija wa mkojo upo karibu na njia ya haja kubwa na uke na bakteria wanaweza kuingia ndani kwa urahisi. Ndiyo maana ni muhimu sana kuifuta kutoka mbele hadi nyuma ili kuepuka maambukizi.Ikiwa una UTI, unaweza kupata hisia inayowasha unapokojoa, mkojo wako unaweza kubadilika rangi na kuwa na mawingu zaidi au mwekundu, na kwa kawaida unahisi kukojoa mara nyingi zaidi. Ikiwa una dalili hizi, unapaswa kutembelea daktari. UTI kwa kawaida hutibiwa kutumia antibaotiki.