Ninawezaje Kutunza Uke Wangu?

Njia bora ya kutunza uke wako ni kuosha kwa maji moto; ni kiungo ambacho unasafisha mwenyewe, kwa hiyo, unapaswa kuepuka kutumia sabuni na manukato wakati unakiosha. Ni muhimu pia kuvaa chupi iliyotengenezwa kwa kitambaa kinachoweza kutowa hewa ambacho kinakutosha vizuri na ambacho hakijakubana sana. Pia, kumbuka kutumia kondomu na lmafuta unapofanya ngono. Unapaswa kumtembelea daktari wako ikiwa unaona unatokwa na uchafu usio wa kawaida au wenye harufu mbaya ukeni au unapata damu ukeni isiyohusiana na hedhi zako.