Sindano | Find My Method
 

Last modified on October 13th, 2020

contraceptive-injection
 • Ufanisi: Aina zote za sindano zina ufanisi wa hali ya juu-Hata hivyo, unapaswa kukumbuka kupata sindano kwa saa. Wakati wanawake wanapata sindano kwa saa, 99 kati ya 100 wataweza kuzuia mimba.
 • Madhara: Za kawaida ni utokwaji wa damu usiotabirika na ongezeko kwa hamu ya chakula, inayosababisha ongezeko la uzani (kwa kawaida kilo 2 au lb 4.4). Wanawake wengi wanaotumia njia hii watakoma kupata hedhi ya kila mwezi baada ya mwaka wa kwanza wa matumizi. Usiwe na wasiwasi; hii haidhuru!
 • Jitihada:kidogo- unahitaji kudungwa kila miezi 1,2 au 3 (kulingana na aina zinazopatikana uliko)
 • Haikingi dhidi ya magonjwa ya zinaa (STI).

Ufupisho

Contraceptive Injection

Summary Injectable Contraceptive

Ndio, ni kile unafikiria! Sirinji na sindano na kioevu kiasi kinachodungwa ndani ya mwili wako.Sindano inazuia ovari kuachilia yai. Na pia inasababisha ute kwenye shingo ya kizazi uwe nzito kusaidia mbegu za kuime zisifikie yai. kuna aina nyingi- zingine zinaweza kosa kupatikana katika nchi yako.[4]

 • Sindano ya kila mwezi: Inakukinga kwa mwezi! Ina homoni mbili-projestini na estrojeni.
 • NET-EN au sindano ya miezi 2: Ina projestini. Inakukinga kwa miezi miwili! Njia bora kwa wanawake ambao hawawezi kutumia estrojeni [5].
 • DMPA au sindano ya miezi 3:Ina projestini. Inakukinga kwa miezi tatu! Njia bora kwa wanawake ambao hawawezi kutumia estrojeni [5].

Maelezo

[10]
Ikiwa hutaki kumeza tembe kila siku, sindano inaweza kuwa chaguo bora. Unahitaji kukumbuka kufanya kitu mara 1 kila mwezi (sindano ya mwezi 1), mara moja kila miezi 2 (NET-EN) au mara moja kila miezi 3 (DMPA). Utahitaji kuona mtoaji wa huduma za afya ama wafanya kazi wa afya ya jamii walio na mafunzo ili udungwe sindano.

Faragha kamili. Hakuna mtu anaweza jua ukitumia sindano. Hakuna kifurushi, wala kitu chochote unastahili kufanya kabla tu ya kufanya ngono.

Ndio, utadungwa sindano. Ikiwa unaogopa sindano, basi njia hii haikufai. Kumbuka ni sindano moja tu kila miezi 1, 2 au 3 na utakuwa umemaliza

 

Kanuni za sindano za kuchelewa.  Hukupata sindano tarehe ulipaswa? Bado unaweza kukingwa. Sindano ya DMPA (ya miezi 3) inaweza tumika hadi wiki 4 kuchelewa. NET-EN (ya miezi 2) inaweza tumika hadi wiki 2 kuchelewa. Sindano za mwezi 1 zinaweza tumika hadi wiki 1 kuchelewa. Lakini usizoe kuchelewa! Inaweza kupunguza ufanisi wa sindano. Zingatia kuweka king’ora kwa simu au kalenda ya karatasi ili kukumbuka tarehe ya kupata sindano.

Mimba. Inawezekana ushike mimba punde baada ya kuwacha sindano, lakini wanawake wengine wanaweza kuchukua miezi kadha kabla ya uwezo wa kushika mimba urudi. Ikiwa hauko tayari kushika mimba, endea sindano ingine ama tumia njia ingine ya kuzuia mimba.

Jinsi ya kutumia

Hauhitaji kufanya chochote ukichagua sindano, hakikisha tu kwamba unadungwa kwa wakati na mtoaji wako wa huduma za afya.

Umeskia kuhusu Sayana Press? Ni sindano unayojidunga mwenyewe kuzuia mimba kwa miezi 3. Kujifunza zaidi kuhusu njia hii, enda injectsayanapress.org

Ukianza kutumia sindano mara ya kwanza, zungumza kuhusu hedhi yako na mtoaji wako au mfanyakazi wa afya wa jamii aliyepata mafunzo. Hii itasaidia kujua utakuwa na kinga lini punde baada ya kupata sindano.

Vidokezi na Mbinu

 • Kutokwa matone ya damu hupungua na muda. Kwa hivyo ipe muda!
 • Ukianza kukosa hedhi yako ya kila mwezi baada ya mwaka 1 wa kutumia sindano, usiwe na wasiwasi! Hili ni la kawaida kwa watumiaji wa njia hii. Lakini, ikiwa ulichelewa kupata sindano na unadhani pengine una mimba,enda upimwe mimba punde iwezekanavyo.
 • Umeongeza uzani baada ya kupata sindano? Usiwe na wasiwasi! Ni kawaida kuongeza uzani ukitumia njia hii (kwa kawaida hadi kilo 2). Wanawake wanao ongeza uzani ndani ya miezi 6 ya matumizi, wako katika hatari ya kuendelea kuongeza uzani wakati wanatumia sindano. Hata ikiwa wanawake wengine hawana wasiwasi wakiongeza uzani, wengine hawatafurahia. Ikiwa hautaki uzani zaidi, fanya mazoezi kila siku au pata ushauri kutoka kwa mtoaji wako kuhusu vyakula unavyokula.

Madhara

Kila mtu ni tofauti. Kile unachopitia pengine hakitafanana na mtu mwingine.

Mambo chanya: Kuna vitu vingi kuhusu sindano ambavyo ni vizuri kwa mwili wako na pia maisha yako ya ngono [3].

 • Rahisi kutumia
 • Haiwezi katiza ngono
 • Faragha: Hakuna atakayejua isipokuwa ukiwaambia.
 • Haukuwi na wasiwasi juu ya kukumbuka kuipata kila siku
 • Inaweza kukupa hedhi nyepesi inayokuja siku chache- au ukose hedhi kabisa.
 • Ina ufanisi wa hali ya juu kwa kuzuia mimba-ukipata sindano kwa wakati
 • Unaweza itumia ukinyonyesha (isipokuwa sindano ya kila mwezi)

Mambo hasi: Kila mtu huwa na wasiwasi juu ya madhara hasi, lakini kwa wanawake wengi, hakuna shida. Kumbuka, unaingiza homoni mwilini mwako, kwahivyo inaweza kuchukua miezi michache mwili izoe. Ipe muda.

Malalamiko ya kawaida zaidi [6]:

 • Utokwaji wa damu usiotabirika, hasa kwa miezi 6-12 za kwanza (hii inaweza maanisha hedhi nzito inayokuja siku nyingi au kutokwa matone ya damu kati ya hedhi moja na inayofuata)
 • Mabadiliko kwa hamu ya chakula au ongezeko la uzani (Ni kawaida kwa wanawake wengine kuongeza kilo 1-2 kwa mwaka wa kwanza. Wanawake wengine hawaongezi uzani)

Malalamiko zisizo za kawaida zaidi::

 • Mabadiliko kwa tamaa ya ngono
 • Msongo wa mawazo
 • Kupoteza nywele au kupata nywele zaidi usoni mwako au mwilini
 • Wasiwasi au kizunguzungu
 • Maumivu ya kichwa
 • Kichefuchefu
 • Vidonda kwenye matiti

Hakuna mbinu ya kukomesha madhara zinazoletwa na sindano. Ikiwa unahisi kwamba madhara yamezidi kiwango unachoweza kuvumilia, tumia njia ingine uwe na kinga. Kumbuka, kuna njia kwa kila mtu, kila mahali!

* Kwa idadi ndogo mno ya wanawake, kuna hatari ya madhara makubwa. Zungumza na aliyekudunga ikiwa una wasiwasi kuhusu madhara unazopata.

 

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tuko hapa kukusaidia. kama bado unahisi sio ya kufaa, tuna mawazo ya njia zingine. Kumbuka tu: Ukiamua kubadilisha njia, hakikisha una kinga wakati unafanya mabadiliko. Kondomu zitakupa kinga bora wakati unatafuta njia itakayofaa mahitaji yako.
Je napaswa kuwa na wasiwasi juu ya utokwaji wa matone ya damu[3]?

 • Kutokwa matone ya damu inaweza kusababishwa na matumizi ya njia tofauti. Haupotezi damu nyingi ukitokwa na matone ya damu, hata ikiwa inaweza kuonekana hivyo.
 • Bado haiendi sawa? Unaweza kuwa na bahati nzuri zaidi ukitumia tembe iliyo na dozi ya juu kidogo ya estrojeni au inayokupa estrojeni wakati wa sehemu tofauti wa hedhi yako
 • Jaribu njia tofauti: IUD; tembe

Na ikiwa sina uwezo wa kulipia sindano?

 • Katika nchi zingine, njia za kuzuia mimba zinaweza kuwa ghali. Unaweza kupata za bure au kwa bei nafuu ukienda kwenye kituo cha afya cha serikali, au kwa mtoa huduma za afya ya jamii.

Ukiwa na mwenzi moja na unaweza kuzungumza naye juu ya mambo haya, pengine mjadiliane kuhusu mchango kila moja wenu atatoa kugharamia swala hili.

Na ikiathiri tamaa yangu ya kufanya ngono[10]?

 • Wakati hili sio lalamiko la kawaida kwa watumizi wa sindano,ni madhara inayoweza kutokea. kwa hivyo, hatua ya kwanza ni kuchunguza ni kipi kingine maishani mwako kinaweza kubadilisha tamaa yako ya ngono? Una fadhaika? Una matatizo ya kimapenzi? Pengine unaweza kubadilisha haya mambo mengine, na kwa kujaribu kuboresha tamaa yako ya ngono, jaribu kufanya mazoezi zaidi, jaribu vitu vipya kitandani, jaribu kuzungumza na mwenzi wako kuhusu hisia na mahitaji yako.
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa umechunguza mambo mengine maishani mwako ambayo yanaweza kufanya ukose tamaa ya ngono na bado unadhani kwamba ni sindano, zingatia kubadilisha utumie tembe, kiraka, au pete (ambazo zina homoni kwa kiwango ya chini na ni rahisi kuwacha ikiwa shida itazidi) au IUD ( ambayo ina homoni kwa kiwango ya chini au bila homoni). Pia unaweza kujaribu nji bila homoni kama vile diaframu, kondomu za nje (kiume), au kondomu za ndani (kike).
 • Jaribu njia tofauti: IUD; kiraka; tembe; pete

Na ikiwa nataka kushika mimba hivi karibuni [3]?

 • Hauwezi kugeuza athari za sindano, kwahivyo ikiwa tayari ulidungwa sindano, lazima ungoje miezi 1,2 au 3 (Kulingana na aina ya sindano) kabla ya kuanza kujaribu kushika mimba.Kuwa mwenye subira-saa zingine inaweza chukua hadi miezi 10 ndio upate tena uwezo wa kushika mimba.
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa unataka kushika mimba karibuni, zingatia sindano ya kila mwezi, NET-EN (ya miezi 2) au njia za homoni tofauti. Tembe, kiraka, pete, au IUD zote zinakupa uwezo wa kushika mimba haraka kushinda sindano. Pia unaweza zingatia njia bila homoni kama vile kondomu za nje (kiume) au kondomu za ndani (kike).
 • Jaribu njia tofauti: Kondomu ya nje (kiume) ; IUD; kiraka; tembe; pete

Mbona napata maumivu ya kichwa [2]?

 • Maumivu ya kichwa ni madhara yanaoweza kutokea ukitumia sindano. Ikiwa una maumivu makali ya kichwa, jaribu kuchunguza sababu zingine zinazoweza kuyaleta. Jaribu kupunguza mafadhaiko, kunywa maji mingi kuzuia upungufu wa maji mwilini, na hakikisha kwamba unapata usingizi wa kutosha. Kama haya hayasaidii, basi zungumza na mtoaji huduma za afya kuhusu maumivu haya ya kichwa.
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa hupati sababu zingine za maumivu ya kichwa, na unataka kubadilisha njia, zingatia IUD, tembe, kiraka , au pete.
 • Jaribu njia tofauti: IUD; kiraka; tembe; pete .

Mbona hisia zangu zinabadilika badilika [6]?

 • Kubadilika badilika kwa hisia ni madhara inayoweza kutokea ukitumia sindano. lakini kabla ya kudadilisha njia, chunguza ni kipi kingine kinaweza kusababisha hisia zako zibadilike badilike.
 • Bado haiendi sawa? Sindano ina homoni, kwahivyo ikiwa unasumbuliwa na mabaliko ya hisia, zingatia kutumia njia ya muda mfupi na yenye dozi ya chini, kama vile tembe, kiraka, au pete. Pia unaweza jaribu aina yoyote ya IUD.
 • Jaribu njia tofauti: IUD; kiraka; tembe; pete

Je sindano inaharibu mazingira kutokana na homoni kwenye mkojo wa wanawake [10]?

 • Njia yoyote ni bora kuliko kutotumia njia yoyote, ikifika kwa swala la mazingira
 • Homoni zingine kutoka kwa sindano zitaingia kwenye mazingira kupitia mkojo wa mwanamke. Lakini ni kiwango kidogo kushinda vyanzo vingine vya estrojeni katika mazingira.
 • Estrojeni kutoka kwenye michakato ya viwanda na uzalishaji, mbolea na viuadudu, na madawa yanayopewa wanyama yote yanaingia katika mazingira kwa viwango vikubwa kushinda estrojeni kwa mkojo wa mwanamke kutoka kwenye sindano.
 • Ikiwa hutaki kuongeza homoni kwenye mazingira au mwilini mwako, kuna njia zingine unaweza kutumia. Kondomu zenye ulimbo wa mpira ( latex) na IUD ya shaba yote ni bora. Chochote utakacho amua, chagua njia na uendelee kuitumia.
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa unataka kutumia njia yenye ufanisi wa juu bila homoni, jaribu IUD bila homoni.
 • Jaribu njia tofauti: IUD

References

[1] Dr Marie Marie Stopes International. (2017). Contraception. Retrieved from http://www.mariestopes.org.au/wp-content/uploads/Contraception-brochure-web-200417.pdf
[2] FPA the sexual health charity. (2017). Your guide to contraceptive injections. Retrieved from https://www.fpa.org.uk/sites/default/files/contraceptive-injections-your-guide.pdf
[3] FSRH Faculty of Sexual and Reproductive Healthcare. (Amended 2019). Progestogen-only Injectable Contraception. RCOG. Retrieved from https://www.fsrh.org/standards-and-guidance/documents/cec-ceu-guidance-injectables-dec-2014/
[4] Family Planning Division Ministy of Health and Family Welfare Government of India. (2016). REFERENCE MANUAL FOR INJECTABLE CONTRACEPTIVE (DMPA). New Delhi . Retrieved from https://nhm.gov.in/images/pdf/programmes/family-planing/guidelines/Reference_Manual_Injectable_Contraceptives.pdf
[5] IPPF. (2013). IMAP Brief Statement Comparing Injectable Contraceptives: depot medroxyprogesterone acetate (DMPA) versus norethisterone enanthate (NET-EN). Retrieved from https://www.ippf.org/sites/default/files/tks_medbulletin_july13_en.pdf
[6] Khadilkar, S. S. (2017). Short-Term Use of Injectable Contraception: An Effective Strategy for Safe Motherhood. J Obstet Gynaecol India. Retrieved from https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5895545/
[7] Kennedy, et al. (2019). Self-administration of injectable contraception: a systematic review and meta-analysis. BMJ Global Health . Retrieved from https://gh.bmj.com/content/bmjgh/4/2/e001350.full.pdf
[8] PATH. (2016). Depot-medroxyprogesterone acetate (DMPA-SC). Application for Inclusion in the WHO Essential Medicines List. Retrieved from https://www.who.int/selection_medicines/committees/expert/21/applications/s18_medroxyprogesterone_acetate_form.pdf
[9] Rani, S. (2017). A study on injectable DMPA (Depomedroxy progesterone acetale) isomg use as short-term. International Journal of Medical and Health Research. Retrieved from http://www.medicalsciencejournal.com/download/561/3-7-56-875.pdf
[10] World Health Organization Department of Reproductive Health and Research and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (2018) Family Planning: A Global Handbook for Providers. Baltimore and Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/260156/9780999203705-eng.pdf?sequence=1
[11] World Health Organization. (2016). Selected practice recommendations for contraceptive use. Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/252267/9789241565400-eng.pdf?sequence=1


lang Kiswahili