
Last modified on October 14th, 2020
Pete ni kifaa cha kuingizwa kidogo kinachojikunga na kinacho kaa ukeni. Unaiwacha ndani kwa wiki 3 kwa wakati na kuitoa wiki ya 4. Pete inazuia mimba kwa njia mbili. Inawachilia homoni ambazo zinazuia ovari kuwachilia yai, na inafanya ute wa shingo ya kizazi uwe nzito na kuzuia mbegu za kiume kufikia yai.
[8]
Inahitaji jitihada kidogo kiasi kila mwezi. Ikiwa unaogopa sindano, ama wewe ni mtu anayeweza kuwa na shida ya kukumbuka kumeza tembe kila siku, pete ni njia inaweza kukufaa. Unahitaji tu kukumbuka kufanya kitu mara mbili kwa mwezi.
Unapaswa kuridhika na mwili wako. Ikiwa hauwezi kuweka vidole vyako ndani ya uke wako, pengine pete haikufai. Ni kama kuweka tamponi. Ikiwa unaweza kufanya hivyo, basi unaweza kujifundisha kutumia pete.
Unaweza kosa kupata hedhi yako. Pete inakuruhusu kukosa hedhi kabisa, na hili ni salama kwa asilimia 100.
Uhifadhi na faragha. Ukiwa na pete za ziada unaweza zihifadhi katika halijoto ya kawaida kati ya 68°F hadi 77°F (20°C hadi 25°C) kwa hadi miezi 4. Ikiwa utakuwa nazo kupita miezi 4, basi zihifadhi kwenye baridi. Usizitumie ikiwa tarehe ya mwisho kutumika imepita. Ikiwa unataka kuweka siri ya njia yako ya kuzuia mimba, hili ni la kukutia wasiwasi. Pia, wenzi wengine husema wanaweza kuihisi wakati wa ngono. kama hio inaleta shida, basi unaweza kutoa pete wakati unafanya ngono. Ukiitoa wakati wa kufanya ngono, irudishe ndani ya masaa 3. Pia, toa pete mara moja tu ndani ya masaa 24. Kuitoa mara nyingi ama kuitoa na ukose kuirudisha kwa masaa zaidi ya 3 kunarudisha chini ufanisi wake.
Pete inawachilia dozi ya chini ya homoni. Pete ina dozi ya chini ya homoni kuliko njia za uzuiaji mimba zingine. Kunaweza kuwa na madhara hasi chache.
Wavuta sigara wa miaka zaidi ya 35, muwe waangalifu. Kwa wanawake walio na miaka zaidi ya 35, kuvuta sigara wakati unatumia pete kunaongeza hatari ya madhara fulani. Unashauriwa kuzungumzia swala hili na mtoaji wako wa matibabu.
Ni lini naweza kushika mimba tena? Utaweza kushika mimba punde baada ya kutoa pete. Ukitaka kushika mimba, hio ni nzuri sana! Ukitaka kuepuka mimba, ingiza pete ingine au jikinge na njia tofauti.
Pete ni rahisi kutumia. Unachohitaji kukumbuka ni saa za kuingiza na kutoa pete.
Jinsi ya kuiingiza. Kwanza, nawa mikono kwa sabuni na maji. Wacha yakauke yenyewe kwa upepo. Kuingiza pete, ishikilie kati ya kidole gumba na kidole cha shahada na uingize jinsi unavyo weza kuingiza tamponi. Itasimama kwenye pande ya ukuta wa uke wako. Pahali inaposimama kwenye ukuta wa uke haijalishi, bora haikuumizi. Sio lazima uitoe ukifanya ngono. (Ni sawa ukitaka kuitoa ukifanya ngono. Hakikisha tu kwamba unairudisha ndani ya masaa 3. Na uitoe tu mara moja ndani ya masaa 24) [5]
Jinsi ya kuitoa. Ukishaingiza pete, iwache ndani kwa wiki 3. Itoe mwanzo wa wiki ya 4. Iwache nje kwa wiki 1. Kisha ingiza pete mpya na anza mzunguko tena. (Kutoa pete ingiza kidole ushike upindo wa chini wa pete na uivute nje). Pete ikishatoka nje, huenda ukapata hedhi yako.Usijali ikiwa bado unatokwa na damu ikifika wakati wa kuweka pete mpya.Hili ni la kawaida na hedhi yako itaisha punde [6].
Vidokezi na Mbinu. Kuingiza pete, hakikisha umesimama au umeketi vizuri- kwa mfano simama ukiwa umeweka mguu moja juu, chuchuma au ulale chini. Unaweza pia jaribu njia ya “kupinda”ambayo unapinda pete kuiingiza.
Kila mtu ni tofauti. Kile unachopitia pengine hakitafanana na mtu mwingine.
Mambo chanya: Kuna vitu vingi kuhusu pete ambavyo ni vizuri kwa mwili wako na pia maisha yako ya ngono [2].
Mambo hasi: Kila mtu huwa na wasiwasi juu ya madhara hasi, lakini kwa wanawake wengi, hakuna shida. Kumbuka, unaingiza homoni mwilini mwako, kwahivyo inaweza kuchukua miezi michache mwili izoe. Ipe muda.Kuna vitu pengine vitaisha baada ya miezi 2 au 3:[2]
Vitu ambavyo vinaweza kuwa muda mrefu:
Ikiwa baada ya miezi 3 unahisi kwamba madhara yamezidi kiwango unachoweza kuvumilia, tumia njia ingine uwe na kinga. Kumbuka, kuna njia kwa kila mtu, kila mahali!
* Kwa idadi ndogo mno ya wanawake, kuna hatari ya madhara makubwa.
Tuko hapa kukusaidia. kama bado unahisi sio ya kufaa, tuna mawazo ya njia zingine. Kumbuka tu: Ukiamua kubadilisha njia, hakikisha una kinga wakati unafanya mabadiliko. Kondomu zitakupa kinga bora wakati unatafuta njia itakayofaa mahitaji yako.
Na ikiwa sitaki kuiingiza?
Na nikiwa na ongezeko la mchozo wa uke?[6]
Mbona pete inatokatoka?[8]
Jaribu njia tofauti: vipandikizi; IUD; sindano
Je,napaswa kuwa na wasiwasi juu ya damu kuganda?
Uko na hatari mdogo mno wa kupata tatizo la kuganda damu wakati unatumia pete. Hata hivyo, kuna hali za kijeni au za kimatibabu ambazo zinaongeza hatari ya kupata tatizo la damu kuganda.Ukiwa na historia ya tatizo la damu kuganda au wasiwasi maalum kuhusu tatizo la damu kuganda, uliza anayekupa njia za kuzuia mimba kama kweli pete ni chaguo bora kwako [8].
Na ikiwa mpenzi wangu anasema kwamba anahisi pete tukifanya ngono?[4]
Je pete inaharibu mazingira kutokana na homoni kwenye mkojo wa wanawake?[8]
Je, kuna hatari ya kutumia tamponi au kikombe cha hedhi wakati natumia pete?[8]
[1] Dr Marie Marie Stopes International. (2017). Contraception. Retrieved from http://www.mariestopes.org.au/wp-content/uploads/Contraception-brochure-web-200417.pdf
[2] FPA the sexual health charity. (2019). Your guide to the contraceptive vaginal ring. Retrieved fromhttps://www.fpa.org.uk/sites/default/files/contraceptive-vaginal-ring-your-guide-2019.pdf
[3] FSRH The Faculty of Sexual & Reproductive Healthcare. (Amended 2019). FSRH Guideline: Combined Hormonal Contraception. Retrieved from https://www.fsrh.org/standards-and-guidance/documents/combined-hormonal-contraception/
[4] RamaRao, et al. (2015). PROGESTERONE VAGINAL RING: RESULTS OF A THREE-COUNTRY ACCEPTABILITY STUDY. Population Council . Retrieved from https://www.popcouncil.org/uploads/pdfs/2015RH_PVRAcceptability3Country.pdf
[5] Reproductive Health Access Project. (2015). THE RING. Retrieved from https://www.reproductiveaccess.org/wp-content/uploads/2015/03/factsheet_ring.pdf
[6] SHINE SA. (2017). Contraceptive Vaginal Ring. Retrieved from https://www.shinesa.org.au/media/product/2015/04/Contraceptive-vaginal-ring.pdf
[7] World Health Organization. (2016). Selected practice recommendations for contraceptive use. Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/252267/9789241565400-eng.pdf?sequence=1
[8] World Health Organization Department of Reproductive Health and Research and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (2018) Family Planning: A Global Handbook for Providers. Baltimore and Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/260156/9780999203705-eng.pdf?sequence=1