Kiraka | Find My Method
 

Last modified on October 14th, 2020

birth-control-patch
 • Rahisi kutumia na hufanya kazi sawa na tembe. Lazima uweke kiraka kipya kila wiki
 • Ufanisi: Kiraka kina ufanisi kikitumika jinsi watu wengi hukitumia. Kwa matumizi kamilifu, wanawake 99 kati ya 100 wataweza kuzuia mimba. Kwa matumizi ya kawaida, ama jinsi watu wengi huitumia, kiraka huzuia mimba kwa wanawake 91 kati ya 100 wanaoitumia.
 • Madhara: kichefuchefu, utokwaji damu usio tabirika,ulaini wa matiti ndizo malalamiko ya kawaida zaidi, lakini haya kwa kawaida huwa ya muda mfupi. Kuwashwa ngozi pia inawezekana.
 • Jitihada: ya wastani. Unahitaji kuweka kiraka kipya kila wiki
 • Haikingi dhidi ya magonjwa ya zinaa (STI).

Ufupisho

Birth Control Patch

Summary Contraceptive Patch

Kiraka ni plastiki nyembamba inayofanana na bendeji yenye umbo la mraba.Ina ukubwa wa sentimita 5. Unabandika kiraka kwenye ngozi yako, na kinawachilia homoni zinazozuia ovari kuwachilia yai. Homoni pia hufanya ute kwenye shingo ya kizazi uwe nzito,na hivyo kuzuia mbugu za kiume kufikia yai.

Maelezo

[9]
Inahitaji jitihada kidogo kuliko tembe, na pia haundungwi. Ikiwa hutaki kumeza tembe kila siku, kiraka kinaweza kuwa chaguo bora. Unahitaji tu kukumbuka kuweka kiraka kipya mara moja kwa siku 7.

Kiraka ni bora zaidi ukiwa na uzani chini ya kilo 90. Ufanisi wake utarudi chini ikiwa una uzani zaidi ya kilo 90. Ukiwa na uzani wa kilo 90 au zaidi, unapaswa kutumia njia ingine ya kuzuia mimba.

Unataka hedhi za kutabirika. Ikiwa unapenda kupata hedhi kila mwezi, bila matone ya damu, basi kiraka kitakua chaguo nzuri.

Wewe ni mvuta sigara wa miaka chini ya 35. Ikiwa una miaka zaidi ya 35, kuvuta sigara wakati unatumia tembe kunaongeza hatari ya madhara fulani. Unashauriwa kuzungumzia swala hili na mtoaji wako wa matibabu.

Unataka kukomesha matumizi ya njia ya kupanga uzazi na ushike mimba haraka? Utaweza kushika mimba siku chache baada ya kuwacha kiraka. Ukiwacha kutumia kiraka na hauko tayari kushika mimba, tumia njia ingine ya kuzuia mimba.

 

Jinsi ya kutumia

[5]

 • Kiraka ni rahisi kutumia. Kitu kigumu zaidi ni kukumbuka kuweka kiraka kipya kila wiki. Bandika tu kiraka moja kipya mara moja kila wiki kwa wiki 3 mfululizo. Usitumie kiraka wiki ya 4.
 • Unaweza kuweka kiraka kwenye tako, tumbo, sehemu ya nje wa juu ya mkono, eneo la kifua. Usiweke kwenye matiti.
 • Pengine utapata hedhi yako katika wiki wiki hautatumia kiraka. Huenda bado hedhi inaendelea ikifika wakati wa kuweka kiraka kingine. Hii ni jambo la kawaida. Weka tu kiraka kipya.
 • Angalia vidokezi na mbinu hapa chini kukupa njia rahisi ya kutumia kiraka.

 

Kidokezo cha 1: ukianza kiraka ndani ya siku 5 za kwanza za kipindi chako, unalindwa na ujauzito mara moja. Ukianza baadaye, itabidi usubiri siku 7 kabla ya kulindwa. Unapaswa kutumia njia mbadala wakati huo.

Kidokezi 2: Fikiria kwa makini ni wapi mwilini uweke kiraka- itakuwa hapo kwa wiki nzima. Ni bora usiweke kiraka eneo lililo na ngozi inayolegea au palipo na mikunjo.

Kidokezi 3: Ambua nusu ya plastiki angavu kwanza, ili ubaki na sehemu ya kushika isiyo nata.

Kidokezi 4: Usiguse sehemu ya kunata na vidole vyako.

Kidozezi 5: Finyilia kiraka kwenye sehemu ya mwili uliochagua. Ifinyilie kwa sekunde 10 ili kijibandike vizuri.

Kidokezi 6: Usitumie losheni ya mwili, mafuta, poda, sabuni zenye rangi ya malai au vipodozi pahala pana kiraka.

Kidokezi 7: Angalia kiraka chako kila siku kuhakikisha kimejibandika vizuri.

Kidokezi 8: Kuna uwezekano wa kuwe na nyuzinyuzi kwenye upindo wa kiraka.

Kidokezi 9: Ukitoa kiraka, ikunje katikati kabla ya kukitupa. Hili litasaidia homoni zisiingie kwenye mchanga. Usiitupe kwa choo cha maji.

Madhara

Kila mtu ni tofauti. Kile unachopitia pengine hakitafanana na mtu mwingine.

Mambo chanya: Kuna vitu vingi kuhusu sindano ambavyo ni vizuri kwa mwili wako na pia maisha yako ya ngono [8].

 • Rahisi kutumia-Ni kama kuweka utepe wa gundi
 • Sio lazima ukatize ngono kuitumia
 • Inaweza kukupa hedhi nyepesi na unayoweza kutabiri
 • Inaweza kumaliza chunusi
 • Inaweza kupunguza maumivu ya tumbo wakati wa hedhi na dalili za kabla ya hedhi (PMS).
 • kinakupa kinga dhidi ya matatizo mengine ya kiafya: Saratani ya ndani ya mji wa mimba na saratari ya ovari; anemia ya upungufu wa madini ya chuma; Uvimbe kwenye ovari na ugonjwa wa uvimbe wa fupanyonga

Mambo hasi: Kila mtu huwa na wasiwasi juu ya madhara hasi, lakini kwa wanawake wengi, hakuna shida. Kumbuka, unaingiza homoni mwilini mwako, kwahivyo inaweza kuchukua miezi michache mwili izoe. Ipe muda.

Vitu ambavyo pengine vitaisha baada ya miezi 2 au 3 [1]:

 • kutokwa damu kati ya hedhi moja na inayofuata au kutokwa matone.
 • Ulaini wa matiti
 • Kichefuchefu na kutapika

Vitu ambavyo vinaweza kuwa muda mrefu:

 • Mwasho eneo lililo na kiraka
 • Mabadiliko kwa tamaa ya ngono

Ikiwa baada ya miezi 3 unahisi kwamba madhara yamezidi kiwango unachoweza kuvumilia, tumia njia ingine uwe na kinga. Kondomu itakupa kinga bora wakati unatafuta njia itakayofaa mahitaji yako.Kumbuka, kuna njia kwa kila mtu, kila mahali!

* Kwa idadi ndogo mno ya wanawake, kuna hatari ya madhara makubwa.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tuko hapa kukusaidia. kama bado unahisi sio ya kufaa, tuna mawazo ya njia zingine. Kumbuka tu: Ukiamua kubadilisha njia, hakikisha una kinga wakati unafanya mabadiliko. Kondomu zitakupa kinga bora wakati unatafuta njia itakayofaa mahitaji yako.

Na ikiwa kiraka kina anguka anguka [7]?

 • Viraka havianguki kwa urahisi. Lakini kiraka chako kikianguka, usiwe na wasiwasi. Unaweza bandika tena kiraka hicho ikiwa hijapita masaa 24, na bado kina gundi. Au unaweza kutumia kiraka kipya.
 • Usitumie bendeji, utepe au gundi kubandika kiraka. Homoni za kukukinga zitachanganyika na gundi, na ikiwa kiraka hakita bandika, pia hakitakuwa na ufanisi.
 • Jaribu hili:Hakikisha hautumii losheni,mafuta, poda, krimu au madawa kwenye ngozi yako sehemu ilio na kiraka. Kutumia losheni au mafuta baada ya kuoga kunaweza kuzuia kiraka kubandika vizuri.
 • Bado haiendi sawa? kikiendelea kuanguka anguka, pengine ujaribu njia ya kuingizwa ndani. Pengine Vipandikizi, an IUD, au pete
 • Jaribu njia tofauti: Vipandikizi; IUD; ring

Na ikiwa nitakuwa na shida ya kukumbuka kubadilisha kiraka [7]?

 • Jaribu hili: Weka kumbusho kwenye simu.
 • Bado haiendi sawa? Ukiweka mfumo wa kumbusho na bado una shida kukumbuka, pengine uzingatie njia ambayo ukishaweka unaweza kusahau kwa miezi au miaka kadhaa. Pengine aina za sindano, vipandikizi  au IUD.
 • Jaribu njia tofauti: Vipandikizi; IUD;Sindano

Nifanye nini ikiwa ninawashwa ngozi sehemu kuna kiraka [9]?

 • Wanawake wengine huwashwa ngozi kwasababu ya gundi.
 • Jaribu hili: Songesha kiraka kwa sehemu ingine ya mwili iliyopendekezwa. Huenda usiwashwe.Ikiwa umekuwa ukikisongesha songesha , jaribu kukiwacha sehemu moja. Ikiwa bado unawashwa ngozi, jaribu kutumia krimu ya inayoitwa Cortisone Cream. Huenda ikapona haraka.
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa hakuna mabadiliko, zingatia njia isiyotumia gundi. Njia zifuatazo hata zinabadilishwa mara chache kuliko kiraka: sindano, vipandikizi, IUD , pete
 • Jaribu njia tofauti: Vipandikizi; IUD ; pete; sindano

Nifanye nini ikiwa sipendi madhara yanayoletwa na homoni?

 • Tumia kiraka kwa miezi michache. Madhara pengine yatapungua na wakati.
 • Bado haiendi sawa? Pengine hutapata madhara sawa na njia za homoni zingine. Ikiwa mambo hayabadiliki na wakati, zingatia pete, sindano, IUD , au vipandikizi.
 • Jaribu njia tofauti: vipandikizi; pete; sindano

Je, kiraka huaribu mazingira [9]?

 • Njia yoyote ni bora kuliko kutotumia njia yoyote, ikifika kwa swala la mazingira
 • Homoni zingine kutoka kwa kiraka zitaingia kwenye mazingira kupitia mkojo wa mwanamke. Lakini ni kiwango kidogo kushinda vyanzo vingine vya estrojeni katika mazingira.
 • Estrojeni kutoka kwenye michakato ya viwanda na uzalishaji, mbolea na viuadudu, na madawa yanayopewa wanyama yote yanaingia katika mazingira kwa viwango vikubwa kushinda estrojeni kwa mkojo wa mwanamke kutoka kwenye kiraka.
 • Ikiwa hutaki kuongeza homoni kwenye mazingira au mwilini mwako, kuna njia zingine unaweza kutumia. Kondomu zenye ulimbo wa mpira ( latex) na IUD ya shaba yote ni bora. Chochote utakacho amua, chagua njia na uendelee kuitumia.
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa unataka kutumia njia yenye ufanisi wa juu bila homoni, jaribu IUD.

Je,napaswa kuwa na wasiwasi juu ya damu kuganda?

 • Uko na hatari mdogo mno wa kupata tatizo la kuganda damu wakati unatumia kiraka. Hata hivyo, kuna hali za kijeni au za kimatibabu ambazo zinaongeza hatari ya kupata tatizo la damu kuganda.Ukiwa na historia ya tatizo la damu kuganda au wasiwasi maalum kuhusu tatizo la damu kuganda, uliza anayekupa njia za kuzuia mimba kama kweli kiraka ni chaguo bora kwako.

Kwanini kiraka kinawacha alama mraba yenye vitu vyeusi vyenye gundi?

 • Haupaswi kuwa na wasiwasi, kuna uwezekano mkubwa kwamba ni vumbi na uchafu zimeshikwa na gundi inayofanya kiraka ikwame kwa ngozi yako.Bora kiraka kiko mahali pake, hakuna unachoweza kufanya. Jaribu usitoe kiraka au kuvutavuta upindo wa kiraka kwasababu haitakwama. mara ukitoa kiraka, jaribukupaka mafuta kwenye alama
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa gundi inakusumbua na unataka njia ya kuzuia mimba ambayo hauhitaji kukumbuka kila siku au kila mara unafanya ngono, zingatia vipandikizi, the IUD, the pete, or the sindano.
 • Jaribu njia tofauti: vipandikizi; IUD; pete; sindano

References

[1] Cornell Health. (2019). The Contraceptive Patch. Cornell University , New York . Retrieved from https://health.cornell.edu/sites/health/files/pdf-library/the-patch.pdf
[2] Contraceptive Choice Center . (2015). Contraceptive Patch FACT SHEET. Washington University in St. Louis School of Medicine, Department of Obstetrics & Gynecology, St. Louis. Retrieved from https://contraceptivechoice.wustl.edu/wp-content/uploads/2015/07/Contraceptive-Patch-Fact-Sheet.pdf
[3] Dr Marie Marie Stopes International. (2017). Contraception. Retrieved from http://www.mariestopes.org.au/wp-content/uploads/Contraception-brochure-web-200417.pdf
[4] FSRH The Faculty of Sexual & Reproductive Healthcare. (Amended 2019). FSRH Guideline: Combined Hormonal Contraception. Retrieved from https://www.fsrh.org/standards-and-guidance/documents/combined-hormonal-contraception/
[5] FPA the sexual health charity. (2019). Your guide to the contraceptive patch. Retrieved from https://www.fpa.org.uk/sites/default/files/contraceptive-patch-your-guide-2019_0.pdf
[6] Galzote, et al. (2017). Transdermal delivery of combined hormonal contraception: a review of the current literature. International Journal of Women´s Health. Retrieved from https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5440026/
[7] Reproductive Health Access Project. (2015). THE PATCH. Retrieved from https://www.reproductiveaccess.org/wp-content/uploads/2014/12/factsheet_patch.pdf
[8] Society of Obstetricians and Gynaecologists of Canada. (2017). Canadian Contraception Consensus Chapter 9: Combined Hormonal Contraception. Retrieved from https://www.jogc.com/article/S1701-2163(16)39786-9/pdf
[9] World Health Organization Department of Reproductive Health and Research and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (2018) Family Planning: A Global Handbook for Providers. Baltimore and Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/260156/9780999203705-eng.pdf?sequence=1
[10] World Health Organization. (2016). Selected practice recommendations for contraceptive use. Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/252267/9789241565400-eng.pdf?sequence=1


lang Kiswahili