Ufungaji uzazi | Find My Method
 

Last modified on October 14th, 2020

vasectomy
 • Suluhisho la kudumu kwa wale wanaojua hawataki kushika mimba siku za usoni. Inapatikana kwa miili ya kiume na kike.
 • Ufanisi: Ufanisi wa hali ya juu. Watu 99 kati ya 100 wataweza kuzuia mimba kwa mafanikio kwa nja hizi[5]
 • Madhara: Uwezekano wa maumivu au kutohisi viruzi mara tu baada ya upasuaji. [3]
 • Jitihada: kidogo. Unapitia utaratibu mara moja, na unamaliza
 • Haikukingi dhidi ya magonjwa ya zinaa (STIs).[2]

Ufupisho

Vasectomy

Sterilization Summary

Wanaume na wanawake wanaweza amua kufunga uzazi. Kwa wanawake, ufungaji uzazi ni utaratibu unaofunga au kuziba mirija ya uzazi kwahivyo hauwezi kushika mimba. Kwa wanaume, ufungaji uzazi unajulikana kama vasektomi. Inaziba mirija ambayo hubeba mbegu za kiume za mwanamume. Zungumza na mtoaji huduma za afya kujifunza zaidi na hakikisha umeuliza kuhusu matakwa, kama vile mambo ya umri na muda wa kungoja.

 

Aina za ufungaji uzazi:[3]

Mkato. Wanaume na wanawake wote wananaweza kufunga uzazi kwa njia ya mkato. kwa wanawake, taratibu za Laparoscopy, Mini-Laparotomy, na Laparotomy (ambazo kwa kawaida ni taratibu za kuchunguza tumbo)zinahitaji mkato, kwahivyo zinahitaji pia unusukaputi. Inaweza kuchukua toka siku 2 hadi siku 21 kupona ukitoka upasuaji.

Vasektomi kwa njia ya mkato kwa wanaume inachukua dakika 20. Inahitaji unusukaputi kwenye sehemu itakayo fanyiwa mkato. Watoaji wataweka mkato moja au mbili kwenye pumbu ili mbegu za kiume zisiingie kwenye manii. Kwa vile mbegu za kiume haziwezi toka, mwanamke hatashika mimba.

Vasektomi unaofanywa bila mkato (no-scapel). Inafanywa kwa sindano ambayo hugungwa kufikia mirija. Kisha mirija hufungwa,huchomwa au huzibwa. Hakuna kuwacha kovu, hakuna kushona na utaratibu huu unajulikana kupona haraka bila matatizo.

Maelezo

[9]
Hakika kabisa. Kabla ya kufunga uzazi, unapaswa kuwa na hakika kwamba hutaki kuwa na watoto uliowazaa mwenyewe.

Ni nani anapaswa kufunga uzazi? Ufungaji uzazi inawezekana kwa wanaume na wanawake, kwahivyo ikiwa unapanga kukuwa na mwenzi mmoja kwa muda, zungumzeni kuhusu ni nani kati yenyu atafungiwa uzazi.

Hakuna wasiwasi kuhusu homini. Ikiwa hutaki njia ya kuzuia mimba yenye homoni, hii ni mojawapo wa njia unaweza kuchagua. Pia, ufungaji uzazi haubadilishi homoni asilia za mwili wako.

Familia yako ni kubwa ya kutosha. Hii ni chaguo nzuri ikiwa uko na watoto wa kutosha, au hutaki watoto.

Ikiwa mimba itasababisha matatizo mabaya ya kiafya. Ikiwa kuna sababu ya kiafya ambayo inahitaji wewe na mwenzi wako msishike mimba, ufungaji uzazi unaweza kuwafaa.

Upatikanaji. Je! Ungependa kutumia njia hii? Njia hii inapatikana katika nchi zote. Walakini, kunaweza kuwa na vizuizi juu ya umri na mwenzi au idhini ya wazazi. Angalia sehemu ya “Mbinu katika nchi yangu” ili upate maelezo zaidi

Jinsi ya kutumia

Kuna aina mbili tofauti za ufungaji uzazi. Mkato (Mtoaji huduma za afya anaweka mikato) na bila-mkato ( hakuna mikato).[3]

Kwa wanawake [4]: Njia za mkato zinajumuisha Laparoscopy, Mini-laparotomy, and Laparotomy. Laparotamy ndio upasuaji mkubwa zaidi kwa zote tatu na pia ndio inafanywa mara chache zaidi. Inahitaji mtu alazwe hospitalini kwa siku nyingi na huchukua wiki mingi kupona. Laparoscopy na Mini-laparotomy ni nyepesi kidogo, na sio lazima mtu alazwe hospitalini na pia hupona haraka zaidi.

Kwa wanaume [1]: Njia ya mkato inaitwa vasektomi. Ni utaratibu wa haraka inayohitaji uende kwa mtoaji huduma za afya, lakini hauhitaji kulazwa hopitalini ama kwenye kliniki. Mtoaji huduma za afya atatumia unusukaputi kufanya ganzi pumbu, aweke mkato mdogo, kisha afunge na akate au azibe miraji. Mkato utazuia mbegu za kiume kupita na kuingia kwenye manii, lakini mbegu za kiume zinaweza baki kwenye miraji kwa miezi kadhaa. Mkato utapona haraka na hauhitaji kushonwa, lakini unapaswa kutumia njia ingine ya kuzuia mimba kwa miezi 3 (kama kondomu).

 

Madhara

Kila mtu ni tofauti. Kile unachopitia pengine hakitafanana na mtu mwingine.

Mambo chanya: [3]

 • Unaweza kufanya ngono bila kuwa na wasiwasi wa mimba.
 • Pitia utaratibu mara moja, na usahau mambo yake kabisa.
 • Hakuna homoni zinaingzwa mwilini mwako

Mambo hasi: [6]

 • Hatari mdogo sana kwamba mirija yako yataungana tena- hali ambayo itawezesha mimba
 • Kunaweza kutokea matatizo kutokana na upasuaji, kama vile utokwaji damu, maambukizo au matatizo yanayoletwa na unusukaputi.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tuko hapa kukusaidia. Kama bado unahisi sio ya kufaa, tuna mawazo ya njia zingine. Kumbuka, kuna njia kwa kila mtu, kila mahali!

Kwanini nahisi uchovu na uchungu ilhali nilifanya ufungaji uzazi wiki kadhaa zilizopita?[3]

 • Ni jambo la kawaida kuhisi uchungu na uchovu kwa siku au wiki mingi baada ya utaratibu huu.Hata hivyo, ukiwa na wasiwasi, au unakosa kupata tena nguvu yako, zungumza na mtoaji wako wa huduma za afya.

Na ikiwa nilifunga uzazi lakini nina dalili za mimba? Kuna uwezekano nina mimba?[4]

 • Ufungaji uzazi una ufanisi wa juu zaidi na inakusudiwa kudumu. Hata hivyo, takriban wanawake 5 kwa kila wanawake 1000 wanashika mimba ndani ya mwaka mmoja baada ya kupitia utaratibu huu, na hio hatari mdogo hubaki hadi mwanamke afike komahedhi.
 • Enda upimwe mimba ukiwa na wasiwasi kwamba huenda una mimba.

Nilitolewa bitana za mji wa mimba (endometrial ablation) na ninawasiwasi kuhusu kupata mimba. Je, ufungaji uzazi ni wazo nzuri?[9]

 • Baada ya kuharibu mji wa mimba, uwezo wa kushika mimba huwa chini kabisa, na pia haipendekezwi. Hata vivyo, inaweza kufanyika. Wanawake walioharibiwa mji wa mimba wanastahili kutumia njia za uzuiaji mimba hadi baada ya komahedhi. Hata ikiwa kuna uwezekano wa mimba baada ya utaratibu huu, mimba baada ya utaratibu huu inaweza kuwa na matatizo mingi, kwahivyo, usifanye ufungaji uzazi hadi uwe na uhakika kwamba hutaki watoto au watoto zaidi. Ufungaji uzazi unaweza kuwa chaguo nzuri kama uliharibiwa mji wa mimba na hautaki wasiwasi wa mimba isiyopangwa.

 

References

[1] Cook LA, et al. (2014). Vasectomy occlusion techniques for male sterilization (Review). John Wiley & Sons. Retrieved from https://www.cochranelibrary.com/cdsr/doi/10.1002/14651858.CD003991.pub4/full/es
[2] Dr Marie Marie Stopes International. (2017). Contraception. Retrieved from http://www.mariestopes.org.au/wp-content/uploads/Contraception-brochure-web-200417.pdf
[3] FPA the sexual health charity. (2015). Your guide to male and female sterilisation. Retrieved from https://www.fpa.org.uk/sites/default/files/male-and-female-sterilisation-your-guide.pdf
[4] FSRH Faculty of Sexual & Reproductive Healthcare. (2014). Male and Female Sterilisation. RCOG, London. Retrieved from https://www.fsrh.org/standards-and-guidance/documents/cec-ceu-guidance-sterilisation-cpd-sep-2014/
[5] Patil, E., & Jensen, J. T. (2015). Update on Permanent Contraception Options for Women. Current Opinion in Obstetrics and Gynecology. Retrieved from https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4678034/
[6] Reproductive Health Access Project. (2018). Permanent Birth Control (Sterilization). Retrieved from https://www.reproductiveaccess.org/wp-content/uploads/2014/12/sterilization.pdf
[7] RCOG Royal College of Obstetricians and Gynaecologists. (2016). Female Sterilisation. Royal College of Obstetricians and Gynaecologists, London. Retrieved from https://www.rcog.org.uk/globalassets/documents/guidelines/consent-advice/consent-advice-3-2016.pdf
[8] World Health Organization. (2016). Selected practice recommendations for contraceptive use. Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/252267/9789241565400-eng.pdf?sequence=1
[9] World Health Organization Department of Reproductive Health and Research and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (2018) Family Planning: A Global Handbook for Providers. Baltimore and Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/260156/9780999203705-eng.pdf?sequence=1


lang Kiswahili