Sponji | Find My Method
 

Last modified on October 14th, 2020

sponge
 • Haina homoni. Hauhitaji agizo la daktari
 • Unaweza kuiingiza hadi masaa 24 kabla ya kufanya ngono
 • Ufanisi: Sponji haina ufanisi, hasa ikiwa tayari umepata mtoto. Kwa matumizi ya kawaida, watu 76 hadi 88 pekee kati ya watu 100 wataweza kuzuia mimba.
 • Madhara: Unaweza kuwa na mwasho
 • Jitihada: Nyingi- lazima uiingize kila wakati unafanya ngono.
 • Haikukingi dhidi ya magonjwa ya zinaa (STIs).

Ufupisho

Contraceptive Sponge

Birth Control Sponges Summary

Sponji ni kipande mviringo cha kisponji plastiki nyeupe. Ina kibonyo kidogo pande moja na kitundu cha nailoni sehumu ya juu. Ina ukubwa wa sentimita 5 toka upande moja hadi mwingine na inaingizwa kwenye uke kabla ya kufanya ngono. Sponji inafanya kazi kwa njia mbili: Inazuia mbegu za kiume kuingia kwenye mji wa mimba kwa kuziba shingo ya kizazi, na pia inaendelea kuwachilia dawa za kuuwa mbegu za kiume.

Maelezo

[6]
Ni chaguo nzuri ikiwa haujali kushika mimba. Watu wengi hawatumii sponji sahihi, kwa hivyo wanawake hushika mimba. Ikiwa hutaki kushika mimba au kupata mtoto, zingatia kutumia njia tofauti.

Unaridhika na mwili wako. Ikiwa hauwezi kuweka vidole vyako ndani ya uke wako, pengine sponji haikufai. Ni kama kuweka tamponi. Ikiwa unaweza kufanya hivyo, basi unaweza kutumia sponji.

Inahitaji nidhamu. Unahitaji kukumbuka kuingiza sponji kila wakati unafanya ngono.Utahitaji nidhamu binafsi na mpango. Lakini angalau unaweza kuibeba ukitaka.

Mzio? Usitumie sponji ikiwa una mzio wa dawa zenye sulfa, polyurethane au dawa za kuuwa mbegu za kiume.

Swala la mimba. Sponji haina homoni, kwahivyo utaweza kushika mimba punde baada ya kuwacha kutumia sponji. Jikinge na njia ingine ukiwacha kutumia sponji na hautaki kushika mimba.

Upatikanaji. Je! Ungependa kutumia njia hii? Angalia sehemu ya “Mbinu katika nchi yangu” ili ujifunze kile kinachopatikana

Jinsi ya kutumia

Unaweza kuingiza sponji hadi masaa 24 kabla ya kufanya ngono. Itachukua mazoea kuitumia sahihi, kwahivyo fuata maelekezo.

 

Jinsi ya kuiingiza:[4]

 1. Nawa mikono kwa sabuni na maji. Wacha yakauke yenyewe kwa upepo.
 2. Weka sponji iwe yenye unyevu kwa kuimwagia angalau milimita 30 ya maji safi, kabla uiingize.
 3. Chochea dawa za kuuwa mbegu za kiume kwa kufinya sponji kwa upole
 4. Ikiwa upande ulio na kibonyo kidogo umeangalia juu, kunja sponji katikati, ikiangalia juu.
 5. Ingiza sponji ndani kabisa iwezekanavyo mahali vidole vyako vinaweza kufika kwenye uke.
 6. Sponji itajikunjua peke yake na kufunika shingo ya kizazi ukiiwachilia.
 7. Telezesha kidole kwenye mzingo wa sponji kuhakikisha imeingia vizuri mahali pake. Unapaswa kuhisi kitundu cha nailoni upande wa chini wa sponji.
 8. Unapaswa kuingiza sponji mara moja pekee.Usitumie tena sponji ambayo umetoa ndani ya mwili wako. Ikiwa ndani, unaweza kufanya ngono mara nyingi unavyotaka.
 9. Uko tayari kufanya ngono mara tu imeingizwa ndani.

 

Jinsi ya kuitoa:[3]

 1. Iwache ndani kwa angalau masaa 6 baada ya ngono.
 2. Nawa mikono kwa sabuni na maji.
 3. Weka kidole ndani ya uke utafute kitundu.
 4. Mara ukishapata tundu, ivute sponji nje bila haraka na kwa upole.
 5. Tupa sponji kwenye pipa la takataka. Iweke mbali na watoto na wanyama.

 

Vidokezi na mbinu

Sponji inahitaji kuwa yenye unyevu kabisa ili kuchochea dawa za kuuwa mbegu za kiume. Hakikisha umeifinya ili kueneza maji.

Madhara

Kila mtu ni tofauti. Kile unachopitia pengine hakitafanana na mtu mwingine.

Mambo chanya:[2]

 • Unaweza kuweka sponji ndani kabla ya ngono, hadi masaa 24 mapema
 • Unaweza fanya ngono mara nyingi unavyotaka ikiwa ndani
 • Wewe au mwenzi wako hamupaswi kuhisi sponji
 • Haina homoni.
 • Hauhitaji agizo la daktari
 • Unaweza itumia ukiwa unanyonyesha

Mambo hasi:[4]

 • Wanawake wengine wanapata ugumu wa kuiingiza
 • Inaweza sababisha mwasho ukeni
 • Inaweza haribu starehe ya ngono
 • Inaweza kufafanya ngono uwe mkavu zaidi
 • Wanawake wengine wana mzio wa dawa zenye sulfa, polyurethane au dawa za kuuwa mbegu za kiume na hawapaswi kutumia sponji.
 • Ni ngumu kukumbuka kutumia ikiwa umelewa

Viwango vya kufeli vya sponji vinatofautiana sana. Inaweza kutegemea ikiwa ulisha pata mtoto au la. Kwa wanawake ambao hawajazaa, kiwango cha kufeli ni asilimia 9 kwa matumizi kamili na asilimia 16 kwa matumuzi ya kawaida jinsi watu huitumia. Kwa wanawake walio na watoto tayari, kiwango cha kufeli kiko juu- asilimia 20 kwa matumizi kamili na asilimia 32 kwa matumizi ya kawaida.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tuko hapa kukusaidia. Kama bado unahisi sio ya kufaa, tuna mawazo ya njia zingine. Kumbuka tu: Ukiamua kubadilisha njia, hakikisha una kinga wakati unafanya mabadiliko. Kondomu zitakupa kinga bora wakati unatafuta njia itakayofaa mahitaji yako.

Na ikiwa sponji inatokatoka?[6]

 • Jaribu hili: Angalia ikiwa sponji imeingia ndani kabisa. Inastahili kuegemea kwenye shingo ya kizazi.
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa bado unashida, na unataka kutumia njia ya kuzuia manii, pengine ubadilishe utumie

  Na ikiwa sponji inaleta mwasho?[2]

  Kondomu za nje (kiume) kondomu za ndani (kike) au diaframu.

  • Au, ikiwa ungependa kujaribu njia ambayo hauhitaji kuingiza au kutumia kila wakati unafanya ngono, zingatia IUD, sindano, vipandikizi, kiraka au tembe.
  • Mwasho pengine unasababishwa na dawa ya kuuwa mbegu za kiume. Kwa vile hauwezi kutenganisha hizo mbili, jaribu njia tofauti.
  • Bado haiendi sawa? Zingatia kutumia njia ambayo haihitaji dawa yoyote ya kuuwa mbegu za kiume.
   • Ikiwa unataka kuendelea kutumia njia ya kuzuia manii, zingatia kutumia kondomu ya nje (kiume) au kondomu ya ndani (kike)
   • Pia zingatia kutumia njia ambayo hauhitaji kutumia kila wakati unafanya ngono, kama vile IUD, sindano, vipandikizi, pete, kiraka, au tembe.
  • Jaribu njia tofauti: kondomu ya nje (kiume); vipandikizi; kondomu ya ndani (kike); IUD; kiraka; tembe; pete; sindano

References

[1] CHIJIOKE, M. K. (2016). SPERMICIDES AND DIAPHRAGMS. UNIVERSITY OF BENIN CITY: DEPARTMENT OF HEALTH, SAFETY AND ENVIRONMENTAL EDUCATION. Retrieved from https://www.academia.edu/24646826/SPERMICIDES_AND_DIAPHRAGMS
[2] Mayer Laboratories, Inc. (2018). Drug facts: TODAY VAGINAL CONTRACEPTIVE- nonoxynol-9 sponge. Retrieved from https://dailymed.nlm.nih.gov/dailymed/getFile.cfm?setid=6b4e54d7-6ba8-4400-bd52-75d112e6fe50&type=pdf&name=6b4e54d7-6ba8-4400-bd52-75d112e6fe50
[3] Society of Obstetricians and Gynaecologists of Canada. (2015). Canadian Contraception Consensus Chapter 5: Barrier Methods. JOGC Journal of Obstetrics and Gynaecology Canada , 37. Retrieved from https://www.jogc.com/article/S1701-2163(16)39376-8/pdf
[4] Shoupe, D. (2016). Barrier Contraceptives: Male Condoms, Vaginal Spermicides, and Cervical Barrier Methods. En D. Shoupe, The Handbook of Contraception: A Guide for Practical Management. Retrieved from http://eknygos.lsmuni.lt/springer/677/147-177.pdf
[5] World Health Organization. (2016). Selected practice recommendations for contraceptive use. Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/252267/9789241565400-eng.pdf?sequence=1
[6] World Health Organization Department of Reproductive Health and Research and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (2018) Family Planning: A Global Handbook for Providers. Baltimore and Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/260156/9780999203705-eng.pdf?sequence=1
[7] Xia, et al. (2020). DL-Mandelic acid exhibits high sperm-immobilizing activity and low vaginalirritation: A potential non-surfactant spermicide for contraception. Elsevier Masson. Retrieved from https://reader.elsevier.com/reader/sd/pii/S0753332220302961?token=063F3CA5FE829FE276755EF2EE8152EBC11B2906592153330A395D73878C354BC3E701A06960C98C04FA57B0D8AB401A


lang Kiswahili