Dawa za kuuwa mbegu za kiume | Find My Method
 

Last modified on October 14th, 2020

spermicide
 • Rahisi kupata, haina homoni, na hauhitaji agizo la daktari.
 • Ufanisi: Dawa ya kuuwa mbegu za kiume haina ufanisi ikitumika pekee yake. Inafanya vizuri zaidi ikitumika pamoja na njia ingine ya kuzuia manii. Watu 72 hadi 82 peke kati ya watu 100 ndio wataweza kuzuia mimba wakitumia njia hii.
 • Madhara: Nyingi zao hazileti matatizo, lakini wewe na mwenzi wako mnaweza kuwa na mwasho kidogo.
 • Jitihada: Nyingi. Unahitaji kupaka kila wakati unafanya ngono.
 • Haikukingi dhidi ya magonjwa ya zinaa (STIs).

Ufupisho

Spermicides

Spermicides Contraception Summary

Dawa za kuuwa mbegu za kiume zina kemikali ambazo zinaziua manii kusonga. Inaweza kuwa krimu, utando, povu, jeli au tembe ya kuingiza. Yoyote utakayochagua, unaingiza ndani kabisa kwenye uke ili izuie manii kupita kwenye shingo ya kizazi kuenda kwenye mji wa mimba.

Maelezo

[5]

Bora zaidi ikitumika pamoja na njia ingine. Dawa ya kuuwa mbegu za kiume inafanya kazi vizuri zaidi ikitumika na njia ingine, kama vile diaframu au kondomu za nje (kiume) kondomu za ndani (kike). Unaweza kutumia dawa ya kuuwa mbegu za kiume kuongeza ufanisi wa njia ya kuzuia manii, lakini haina ufanisi ikitumika pekee yake.

Haujali kushika mimba. Kiwango cha kufeli kwa dawa ya kuuwa mbegu za kiume kiko juu. Ikiwa hautaki kushika mimba, basi tumia njia ingine au tumia tu dawa ya kuuwa mbegu za kiume pamoja na njia ingine ya kuziba manii.

Hauhitaji agizo la daktari. Hauhitaji kumwona mtoaji huduma za kimatibabu ili kutumia dawa ya kuuwa mbegu za kiume. Zingatia pia kuchukua kondomu kadhaa wakati huo.

Watu wengine wana mzio wa dawa ya kuuwa mbegu za kiume. Ikiwa utapata mwasho ukitumia dawa za kuuwa mbegu za kiume, pengine una mzio wake. Dawa nyingi za kuuwa mbegu za kiume na jeli za uzuiaji mimba huwa na kemikali ya Nonoxynol-9. Ikiwa una mzio wa kemikali hii, basi dawa ya kuuwa mbegu za kiume huenda sio chaguo nzuri kwako.

Wenzi wote wawili hawana ukimwi (VVU). Kemikali ya Nonoxynol-9 inaleta mabadiliko kwenye ngozi yako iliyo na unyeti. Inakufanya uwe na uwezo mkubwa wa kupata VVU. Ikiwa wewe na mwenzi wako mnaishi na VVU, Hamjapimwa hivi karibuni au unafanya ngono na wenzi tofauti tofauti,zingatia kutumia njia itakayokukinga dhidi ya maambukizi ya VVU.

Upatikanaji. Je! Ungependa kutumia njia hii? Angalia sehemu ya “Mbinu katika nchi yangu” ili ujifunze kile kinachopatikana.

Jinsi ya kutumia

[3]

Kila aina ya dawa za kuuwa mbegu za kiume ni tofauti, na kuna aina nyingi zinazopatikana. Hakikisha umesoma maelekezo kwenye pakiti na umeangalia siku ya mwisho kutumika. Dawa ya kuuwa mbegu za kiume ni rahisi kutumia: Ingiza dawa kwa kutumia vidole au kwa kutumia kifaa cha kuingiza.

Baada ya kuziingiza, dawa zingine za kuuwa mbegu za kiume zitahitaji ungoje dakika 10 kabla ya kufanya ngono. Aina hizi huwa tu na ufanisi saa moja baada ya kuziingiza. Utahitaji kukuwa mwangalifu wa muda kati ya kuingiza dawa hizi na wa kufanya ngono.

Madhara

Kila mtu ni tofauti. Kile unachopitia pengine hakitafanana na mtu mwingine.
Mambo chanya:[3]

 • Rahisi kutumia na kupata
 • Inaweza kuingizwa kama mbinu ya utianaji nyege
 • Haina homoni
 • Hauhitaji agizo la daktari
 • Unaweza itumia ukiwa unanyonyesha

Mambo hasi:[2]

 • Inaweza kuleta uchafu/ au kuvuja toka ukeni.
 • Inaweza sababisha mwasho kwenye uke wako au kwenye uume wa mwezi wako.
 • Watu wengine wana mzio wa dawa za kuuwa mbegu za kiume.
 • Huenda ukose kupenda ladha yake
 • Dawa nyingi za kuuwa mbegu za kiume huwa na kemikali ya Nonoxynol-9,anbayo inaweza kusababisha mwasho (Hasa ukiitumia zaidi ya mara moja kwa siku) Na hili litaongeza hatari ya maambukizo ya VVU au magonjwa ya zinaa.
 • Ni ngumu kukumbuka kutumia ikiwa umelewa

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tuko hapa kukusaidia. Kama bado unahisi sio ya kufaa, tuna mawazo ya njia zingine. Kumbuka tu: Ukiamua kubadilisha njia, hakikisha una kinga wakati unafanya mabadiliko. Kondomu zitakupa kinga bora wakati unatafuta njia itakayofaa mahitaji yako.

Na ikiwa dawa ya kuuwa mbegu za kiume itasababisha mwasho?[4]

 • Mwasho unaweza kusababishwa na aina ya dawa za kuuwa mbegu za kiume unayotumia. Jaribu kutumia aina ingine ikiwa bado unataka kuendelea kutumia dawa za kuuwa mbegu za kiume.
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa una mzio wa Nonoxynol-9, ambayo ni kemikali kuu inayotumika kwenye dawa nyingi za kuuwa mbegu za kiume, zingatia njia ingine. Ikiwa unapendelea njia bila homoni, kondomu za nje (kiume), kondomu za ndani (kike), na IUD ya shaba zinawezaa kukufaa.
 • Jaribu njia tofauti: kondomu za nje (kiume); kondomu za ndani (kike); IUD

Na ikiwa dawa ya kuuwa mbegu za kiume zinachafua?

 • Dawa za kuuwa mbegu za kiume zina uchafuzi. Jaribu kutumia aina ingine tofauti na hakikisha kwamba unatumia dawa hizi jinsi maelekezo yanasema.Ukidhani ina uchafuzi sana, jaribu njia tofauti.
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa dawa za kuuwa mbegu za kiume sio chaguo bora zaidi kwado, zingatia Ikiwa una mzio wa Nonoxynol-9, ambayo ni kemikali kuu inayotumika kwenye dawa nyingi za kuuwa mbegu za kiume, zingatia njia ingine. Ikiwa unapendelea njia bila homoni, kondomu za nje (kiume), kondomu za ndani (kike) na IUD ya shaba zinawezaa kukufaa.
 • Try a different method: kondomu za nje (kiume); vipandikizi; kondomu za ndani (kike); IUD; sindano

References

[1] Banerjee, et al. (2014). Insights of Spermicidal Research: An Update. Journal of Fertilization: In vitro – IVF-Worldwide, Reproductive Medicine, Genetics & Stem Cell Biology, 3. Retrieved from https://www.longdom.org/open-access/insights-of-spermicidal-research-an-update-2375-4508.1000138.pdf
[2] CHIJIOKE, M. K. (2016). SPERMICIDES AND DIAPHRAGMS. UNIVERSITY OF BENIN CITY: DEPARTMENT OF HEALTH, SAFETY AND ENVIRONMENTAL EDUCATION. Retrieved from https://www.academia.edu/24646826/SPERMICIDES_AND_DIAPHRAGMS
[3] Shoupe, D. (2016). Barrier Contraceptives: Male Condoms, Vaginal Spermicides, and Cervical Barrier Methods. En D. Shoupe, The Handbook of Contraception: A Guide for Practical Management. Retrieved from http://eknygos.lsmuni.lt/springer/677/147-177.pdf
[4] Society of Obstetricians and Gynaecologists of Canada. (2015). Canadian Contraception Consensus Chapter 5: Barrier Methods. JOGC Journal of Obstetrics and Gynaecology Canada , 37. Retrieved from https://www.jogc.com/article/S1701-2163(16)39376-8/pdf
[5] World Health Organization Department of Reproductive Health and Research and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (2018) Family Planning: A Global Handbook for Providers. Baltimore and Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/260156/9780999203705-eng.pdf?sequence=1
[6] World Health Organization. (2016). Selected practice recommendations for contraceptive use. Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/252267/9789241565400-eng.pdf?sequence=1
[7] Xia, et al. (2020). DL-Mandelic acid exhibits high sperm-immobilizing activity and low vaginalirritation: A potential non-surfactant spermicide for contraception. Elsevier Masson. Retrieved from https://reader.elsevier.com/reader/sd/pii/S0753332220302961?token=063F3CA5FE829FE276755EF2EE8152EBC11B2906592153330A395D73878C354BC3E701A06960C98C04FA57B0D8AB401A


lang Kiswahili