Sio sasa hivi | Find My Method
 

Last modified on October 14th, 2020

abstinance-not-right-now
 • Ikiwa hautafanya ngono, hautashika mimba
 • Ufanisi: “Sio sasa hivi” ina ufanisi wa asilimia 100 ikiwa hautafanya ngono
 • Madhara: hakuna
 • Jitihada: Nyingi. Lazima uwe na udhitibiti, na inafanya kazi tu ikiwa hautafanya ngono ya ukeni

Ufupisho

Abstinance

Summary “Not Right Now”

“Sio sasa hivi” Ni njia moja ya kusema kujinyima ngono au ” Ngono isiyo ya uume-uke.” Ni njia iliyo na ufanisi wa juu- hata hivyo, kwa watu wengine ni njia ngumu sana kutumia. Ikiwa unaitumia kila mara, unahakikishiwa kuwa hautapata mimba. Ikiwa unaepuka shughuli zote za ngono, pia utakuwa salama kutoka kwa magonjwa ya zinaa (STIs)

Maelezo

[5]
Inahitaji nidhamu na kujitolea. Kusema ” Sio sasa hivi” itakuwa na matokeo bora kama njia ya uzuiaji mimba ukiifanya kila mara.

Stadi nzuri za mawasiliano. Ikiwa una uhusiano wa kimapenzi, Utahitaji kuwa na uwezo wa kuambia mwenzi wako kile kiko sawa na kile hakiko sawa. Inamaanisha unahitaji kuwa huru kuzungumza na mwenzi wako na kumwambia kile unacho fikiria.

Una egemeo. Ukiwa katika uhusiano wa kimapenzi, nyote wawili munapaswa kukubaliana hamtafanya ngono ya ukeni. Lakini kumbuka, kusema ” sio sasa hivi” haimanishi ujinyime raha. Ni njia bora ya kuwa mbinifu na maisha yako ya ngono.

 

Jinsi ya kutumia

Usifanye ngono ya ukeni. Njia hii ya uzuiaji mimba inahitaji uamue kwamba hautafanya ngono ya ukeni. Ni chaguo ambalo utahitaji kukumbuka kila siku. Ili uweze kulitekeleza, jikumbushe kila mara ni kwa nini uliamua kutofanya ngono ya ukeni. Pia kumbuka madhara yatakayotokea ikiwa utabadilisha msimamo. Ukiamua kufanya ngono, hakikisha umejikinga kwa njia ingine ya uzuiaji mimba.

Madokezo mengine sadizi:[3]

 • Epuka kujiweka kwenye hali ambazo utapata ugumu wa kutekeleza msimamo wako.
 • Zingatia kuepuka pombe na madawa za kulevya kwasabu zinaweza kufanya upoteze msimamo.
 • Tafuta watu amao unaweza kuzungumza nao kuhusi maamuzi yako na utegemee msaada wao.
 • Zungumuza kwa kina kuhusu maamuzi yako na mwenzi wako kabla mujipate kwenye hali ya ngono.
 • Kuwa wazi kabisa na mwenzi wako kuhusu mipaka yako kwa swala hili.
 • Jaribu njia zingine za ngono ambazo unaweza kufurahia pia.

 

Madhara

Kila mtu ni tofauti. Kile unachopitia pengine hakitafanana na mtu mwingine.

Mambo chanya:[2]

 • Haikugharimu chochote
 • Haisababishi madhara yoyote

Mambo hasi:[2]

 • Inaweza kuwa ngumu kutekeleza kila mara
 • Ni ngumu kutekeleza ikiwa umelewa

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tuko hapa kukusaidia. kama bado unahisi sio ya kufaa, tuna mawazo ya njia zingine. Kumbuka tu: Ikiwa unafikiria kufanya ngono baada ya kipindi cha kujinyima ngono, hakikisha kwamba umetumia njia ingine ya uzuiaji mimba yenye ufanisi. Ni vipi nitamweleza mwenzi wangu kwamba sifanyi ngono wakati huu?

 • Kwanza, hakikisha kwamba umezungumza na mwenzi wako kabla muanze kufanya ngono. Pili, Fikiria jinsi ya kumweleza mwenzi wako kuhusu maamuzi yako. Sema ukweli kuhusu sababu zako. Kuwa wazi juu ya kile unachoweza kufanya na kile hautafanya. Ikiwa mwenzi wako anaingiliana nawe, ataheshimu maamuzi yako.

Na ikiwa natamani kufanya ngono?[5]

 • Ni jambo la asili kuvutiwa na mtu. Ikiwa unafikiria kufanya ngono baada ya kipindi cha kujinyima ngono, ni muhimu uchukue muda kuwaza kuhusu sababu zako za kungoja.
 • Ukiamua hautafanya ngono sasa hivi, zungumza na mwenzi wako kuhusu sababu zako za kutofanya ngono. Pia zungumza kuhusu vitu unavyoweza kufanya na vile hauwezi.
 • Ukiamua kwamba unataka kuanza kufanya ngono, zingatia kutumia njia ya uzuiaji mimba ambayo itakufaa. Hakikisha umefanya hivyo kabla ya kufanya ngono.
 • Chochote utakacho amua, zingatia kukuwa na njia za uzuiaji mimba kama kondomu za nje (kiume), kondomu za ndani (kike) na njia za dharura za uzuiaji mimba, endapo utazihitaji.
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa “Sio sasa hivi” haiwezekani tena, zingatia njia ya uzuiaji mimba ambayo unaweza kutegemea (na inayopatikana kwa urahisi) kabla uanze kufanya ngono. Zingatia njia ya kufanya kwa muda na ambayo athari zake zinaweza geuzika.
 • Jaribu njia tofauti: kondomu za ndani (kike); vipandikizi; IUD; kondomu za nje (kiume); sindano

 

References

[1] Reproduction, (HRP) Department of Reproductive Health and Research World Health Organization. Retrieved from https://www.gfmer.ch/Endo/Lectures_11/Naturalc.htm
[2] SOGC The Society of Obstetricians and Gynaecologists of Canada. (2016). Contraception. Retrieved from https://www.sexandu.ca/wp-content/uploads/2016/09/Contraception_Methods_Booklet.pdf
[3] Society of Obstetricians and Gynaecologists of Canada. (2015). Canadian Contraception Consensus Chapter 4: Natural Family Planning. JOGC Journal of Obstetrics and Gynaecology Canada. Retrieved from https://www.jogc.com/article/S1701-2163(16)39375-6/pdf
[4] Vogelsong, K. M. (2017). Natural Contraceptive Methods. UNDP/UNFPA/WHO/World Bank Special Programme of Research, Development and Research Training in Human Reproduction, (HRP) Department of Reproductive Health and Research World Health Organization. Retrieved from https://www.gfmer.ch/Endo/Lectures_11/Naturalc.htm
[5] World Health Organization Department of Reproductive Health and Research and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (2018) Family Planning: A Global Handbook for Providers. Baltimore and Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/260156/9780999203705-eng.pdf?sequence=1
[6] World Health Organization. (2016). Selected practice recommendations for contraceptive use. Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/252267/9789241565400-eng.pdf?sequence=1


lang Kiswahili