IUD bila homoni | Find My Method
 
non-hormonal-iud
 • Rahisi kuficha. Ni kifaa kidogo bila homoni cha plastiki na shaba kinachowekwa kwenye mji wa mimba (tumbo la uzazi).
 • Ufanisi: IUD ni mojawapo ya njia zilizo na ufanisi wa hali ya juu. Watu 99 kati ya 100 wataweza kuzuia mimba.
 • Madhara: Kuna uwezekano wa hedhi na maumivu kwa tumbo kuongezeka.
 • Jitihada:kidogo: Inaingizwa mara moja na hukaa miaka mingi.
 • Haikingi dhidi ya magonjwa ya zinaa (STI).

Ufupisho

Copper IUD

Summary Non Hormonal IUD

IUD ni kifaa kidogo chenye umbo wa herufi T cha plastiki na shaba. Shaba inabadilisha kidogo mazingira ya mji wa mimba na kuzuia bengu za kiume kufikia yai. IUD zinakupa kinga kwa miaka 3 hadi 12 kulingana na aina ya IUD uliyopata. Ukitaka kushika mimba, unaweza kutolewa IUD.

Maelezo

Ipate kisha usahau mambo yake. Ikiwa hutaki kuwa na wasiwasi kuhusu njia yako ya kuzuia mimba, IUD itakufaa. Mara tu ikiwa ndani, unaweza kuiacha huko kwa miaka 3 hadi 12.

Kazi rahisi. Hakuna kifurushi, au cha kununuliwa kwenye duka la dawa. Hakuna kinachoweza kupotea au kusahaulika.

Faragha kamili. Hakuna mtu anaweza jua ukiwa na IUD. (Wanaume wengine husema wanaweza kuhisi nyuzi, lakini hakuna mtu mwingine atajua ipo). Hakuna kifurushi, wala kitu chochote unastahili kufanya kabla tu ya kufanya ngono.

Salama na kufaa miili ya wanawake. Wataalamu wengi wanakubaliana, ukiwa mwenye afya na una mji wa mimba, IUD itakufaa. Hili nila kweli hata ukiwa kijana, hujawai shika mimba au hujawai pata watoto. Pia ni njia bora kwa akina mama waliojifungua karibuni (hata ikiwa unanyonyesha).

Swala la mimba. Unapaswa kuwa na uwezo wa kushika mimba haraka baada ya kutolewa IUD. Ikiwa hauko tayari kushika mimba punde unavyotolewa IUD, hakikisha umejikinga kwa nji nyingine.

Upatikanaji. Je, ungependa kutumia njia hii? Njia hii inapatikana kwa wingi. Uliza tu kwenye kituo chako cha afya cha mtaa.

Jinsi ya kutumia

Mara tu iko ndani, hakuna unachohitaji kufanya. Vipandikizi vinabaki chini ya ngozi yako,na kukupa kinga dhidi ya mimba hadi miaka 3-5, kulingana na vipandikizi ulivyotumia [4].

Unaweza ingiziwa IUD wakati wowote wa mwezi. Watoaji wengine wanapendelea kuiingiza wakati wa hedhi, lakini wakati wowote ni nzuri, bora tu una hakika hauna mimba. Itakuwa rahisi mno ikiwekwa wakati wa hedhi (Wakiti ambapo shingo ya kizazi , mdomo wa mji wa mimba- uko wazi zaidi) [9].

Ni kawaida kuhisi maumivu ya tumbo ukiwa na IUD, lakini maumivu yataisha ukipumzika au ukitumia dawa. Wanawake wengine wanaweza kuwa na kizunguzungu pia. Mara tu IUD iko ndani, utaona uzi ndogo inayo ning’inia kwenye uke wako. Iko hapo kwa ajili ya kusaidia kutoa IUD baadaye.( Nyuzi hazining’ini nje ya uke). [7]

Mara tu iko ndani, unapaswa kukagua ikiwa nyuzi zipo,mara chache kwa mwaka kuhakikisha kwamba iko pahali pake. Hivi [11]:

Nawa mikono kwa sabuni na maji, kisha keti au chuchumaa chini.

Weka kidole chako kwenye uke wako hadi uguse shingo ya kizazi, ambayo itakuwa imara na kuhisi kama mpira, kama vile ncha ya pua yako.

Tafuta nyuzi. Ukizipata, Hongera! IUD yako iko sawa. Lakini ukigusa sehemu mgumu wa IUD kwenye pande za shingo ya kizazi, unaweza kuhitaji irekebishwe au ibadilishwe na mtoaji wako.

Usivute nyuzi! Ukifanya hivyo, IUS inaweza kutoka pahali pake.

Kama huwezi tafuta nyuzi peke yako,unaweza mwacha mtoaji wako afanye hivyo mwezi baada ya kuingiziwa, kisha kila mwaka baada ya hapo [13].

Madhara

Kila mtu ni tofauti. Kile unachopitia pengine hakitafanana na mtu mwingine.

Mambo chanya: Kuna vitu vingi kuhusu IUDs ambavyo ni vizuri kwa mwili wako na pia maisha yako ya ngono [5].

 • Rahisi kutumia
 • Haiwezi katiza ngono
 • Kinga ya muda mrefu mno bila jitihada nyingi
 • Ni salama kwa wavuta sigara na walio na shinikizo la damu na ugonjwa wa sukari.
 • IUDs hazibadilishi viwango vyako vya homoni
 • Unaweza itumia ukiwa unanyonyesha

Mambo hasi: Kila mtu huwa na wasiwasi juu ya madhara hasi, lakini kwa wanawake wengi, hakuna shida. Wanawake wengi huzoea IUD haraka sana, lakini kuna uwezekano wa kuchukua miezi michache [6].

Malalamiko ya kawaida zaidi:

 • Matone ya damu kati ya hedhi moja na nyingine (hususan miezi ya kwanza baada ya kupata IUD)
 • Ongezeko wa hedhi
 • Maumivu ya tumbo na maumivu ya mgongo

Maswala mengine ya kuangalia:

 • IUD kuteleza na kutoka nje
 • Maambukizo
 • IUD kutoka nje ya ukuta wa mji wa mimba

Ukihisi kwamba madhara yamezidi kiwango unachoweza kuvumilia baada ya miezi 3, tumia njia ingine uwe na kinga. Kumbuka, kuna njia kwa kila mtu, kila mahali!

* Kwa idadi ndogo mno ya wanawake, kuna hatari ya madhara makubwa.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tuko hapa kukusaidia. kama bado unahisi sio ya kufaa, tuna mawazo ya njia zingine. Kumbuka tu: Ukiamua kubadilisha njia, hakikisha una kinga wakati unafanya mabadiliko. Kondomu zitakupa kinga bora wakati unatafuta njia itakayofaa mahitaji yako.

Je, IUD itaumiza mwenzi wangu?

IUD haipaswi kuumiza mwenzi wako. Kuna uwezekano umesikia kwamba nyuzi za IUD zinaweza kusumbua wanaume wakati wa ngono, lakini wenzi wengi hata hawahisi hizo nyuzi. Ikiwa mwenzi wako anazihisi nyuzi hizo na zinamsumbua, mtoaji wako wa huduma za afya anaweza kuzipunguza. Pamoja na hayo, nyuzi huwa laini na muda.

Bado haiendi sawa? unaweza kuwa na bahati nzuri zaidi ukitumia njia inayokupa estrojeni wakati wa sehemu wa mzunguko wa hedhi. Zingatia tembe, kiraka au pete.

Je, napaswa kuwa na wasiwasi juu ya matone ya damu?

Kutokwa matone ya damu, ambayo inaweza kusababishwa na matumizi ya njia tofauti, haikufanyi upoteze damu nyingi, hata ikiwa inaweza kuonekana hivyo [5].

Na ikiwa hedhi ni nzito zaidi na/au maumivu ya tumbo wakati wa hedhi yatazidi?

Hili ni jambo la kawaida na IUD. Ijaribu kwa miezi michache, na utumie ibuprofen siku chache za kwanza za hedhi.

Bado haiendi sawa? Ikiwa unapenda urahisi wa kutumia IUD, lakini madhara hayapungui na wakati au na dawa za kupunguza maumivu, jaribu kutumia IUS ya homoni au njia ya vipandikizi. [15]

Jaribu njia tofauti: Vipandikizi, IUS

Na ikiwa nataka kushika mimba?

Ikiwa uko tayari kushika mimba, ambia mtoaji wako atoe IUD yako. Mwili wako unastahili kurudi kawaida haraka, na unaweza kuanza kujaribu kushika mimba mara hio [10].

IUD yangu ilitoka. Kuna uwezekano gani hili litafanyika tena?

Kutoka kwa IUD kunawezekana kwa asilimia 2-10 ya wanawake ndani ya mwaka wa kwanza wa kuingizwa. Kutoka kunawezekana zaidi kwa wanawake ambao:

 • Wana umri chini ya miaka 20
 • Wana historia ya kuwa na hedhi nzito au hedhi iliyo na maumivu makali.
 • Waliwekewa IUD punde baada ya kujifungua au mimba ilitoka wakati wa trimesta ya pili (miezi 4-6)

Kipande cha IUD kutoka kunaweza kumaanisha kwamba IUD haikuingia sawa: Pengine ilikuwa chini sana kwenye mji wa mimba na ikatoka. Hili linaweza kuwa lilifanyika wakati wa kuingizwa au inaweza kuhusiana na umbo la mji wa mimba kama vile ukubwa,pembe, au kuwepo na uvimbe (fibroids) ambazo zinaweza kubadilisha umbo. Kwa wanawake ambao IUD ilitoka, kuna uwezekano mkubwa kwamba IUD ya pili pia itatoka- Kwa kiwango cha asilimia 20 (hadi asilimia 30 kwa tafiti zingine) [5].

Bado haiendi sawa? Ikiwa unapenda urahisi wa kutumia IUD, lakini una matatizo ya IUD kutoka, unaweza kujaribu kutumia njia ya vipandikizi-chaguo linalofanya muda mrefu na la kuhitaji kazi ndogo ya utunzaji.

Jaribu njia tofauti: Vipandikizi

Je, kuingiziwa IUD kutaumiza?

Uchungu mtu anayohisi wakati IUD inaingizwa itakuwa tofauti kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kwa bahati mbaya, hakuna dawa ya kumeza ili kufanya uingizaji uwe na uchungu mdogo.

Unaweza jaribu kumeza ibuprofen kabla ya uingizaji na uhakikishe IUD inaingizwa wakati shingo ya uzazi uko wazi, kama vile wakati wa hedhi au kupevuka kwa yai. Hata ikiwa kutakuwa na uchungu, itafaa miaka ya kufanya ngono bila kushika mimba [15].

Nataka IUD yangu itolewe. Naweza kuitoa mimi mwenyewe?

Unaweza kupata masimulizi mengine kwenye mitandao ya watu kutoa IUD wenyewe.Hatupendekezi kuijaribu. Hakuna tafiti za kutosha kujua kama ni salama. Kama haufurahi IUD yako, kuenda kwa mtoaji wako ili itolewe itakupa fursa ya kuzungumzia njia zingine za uzuiaji mimba au kushika mimba [8].

Ikiwa uko tayari kushika mimba,unaweza kuzungumza na mtoaji wako kuhusu vitu unavyopaswa kufanya kujitayarisha kwa mimba yenye afya.

Bado haiendi sawa? Ukitaka njia ya muda mrefu na ni rahisi kutumia, njia ya vipandikizi inaweza kuwa chaguo nzuri.

Jaribu njia tofauti: Vipandikizi

Je, naweza kutumia tamponi ikiwa niko na IUD?

Utakuwa sawa ilimradi uwe mwangalifu usivute nyuzi za IUD, jambo ambalo lisikupe wasiwasi sana kwasababu uzi ya tamponi iko nje ya uke wako, na nyuzi za IUD ziko ndani ya uke, juu karibu na shingo ya kizazi. ( Ukigundua kwamba nyuzi za IUD ziko karibu na nyuzi za tamponi, muone mtoaji wako wa huduma za afya kwasababu IUD inaweza kutoka.) [6]

References

[1] Arrowsmith, et al. (2013). Strategies for improving the acceptability and acceptance of the copper intrauterine device. Cochrane Database of Systematic Reviews. Retrieved from https://www.cochranelibrary.com/es/cdsr/doi/10.1002/14651858.CD008896.pub2/abstract
[2] BATESON, D., & McNAMEE, K. (2016). Intrauterine contraception A best practice approach across the reproductive lifespan. Medicine Today. Retrieved from https://www.shinesa.org.au/media/2016/07/Intrauterine-contraception-A-best-practice-approach-Medicine-Today.pdf
[3] Dr Marie Marie Stopes International. (2017). Contraception. Retrieved from http://www.mariestopes.org.au/wp-content/uploads/Contraception-brochure-web-200417.pdf
[4] FSRH The Faculty of Sexual & Reproductive Healthcare. (Amended 2019). UK MEDICAL ELIGIBILITY CRITERIA. RCOG, London. Retrieved from https://www.fsrh.org/standards-and-guidance/documents/ukmec-2016/
[5] FPA the sexual health charity. (2017). Your guide to the IUD: Helping you choose the method of contraception that’s best for you. Retrieved from https://www.fpa.org.uk/sites/default/files/intrauterine-device-iud-your-guide.pdf
6] IFPA Sexuality, Information, Reproductive Health and Rights. (2009). Copper intrauterine devices (IUCD). Dublin. Retrieved from https://www.ifpa.ie/sites/default/files/documents/media/factsheets/iucd.pdf
[7] Nelson, A. L., & Massoudi, N. (2016). New developments in intrauterine device use: focus on the US. Retrieved from https://www.dovepress.com/new-developments-in-intrauterine-device-use-focus-on-the-us-peer-reviewed-fulltext-article-OAJC
[8] Planned Parenthood. (2020). What are the benefits of IUDs? Retrieved from Planned Parenthood https://www.plannedparenthood.org/learn/birth-control/iud/what-are-the-benefits-of-iuds
[9] Pathfinder International. (2008). Intrauterine Devices (IUDs): Trainer’s Guide. Retrieved from http://www2.pathfinder.org/site/DocServer/IUD2E_combined.pdf?docID=11263
[10] Reproductive Health Access Project. (2017). IUD Information. Retrieved fromhttps://www.reproductiveaccess.org/wp-content/uploads/2014/06/IUD_facts.pdf
[11] Reproductive Health Access Project. (2015). Copper IUD. Retrieved from https://www.reproductiveaccess.org/wp-content/uploads/2014/12/factsheet_iud_copper.pdf
[12] Society of Obstetricians and Gynaecologists of Canada. (2016). Canadian Contraception Consensus: Chapter 7 Intrauterine Contraception. JOGC. Retrieved from https://www.jogc.com/article/S1701-2163(15)00024-9/pdf
[13] Shefras and Forsythe. (2019). Copper intrauterine device IUD. Oxford University Hospitals NHS Foundation Trust. Retrieved from https://www.ouh.nhs.uk/patient-guide/leaflets/files/43583Pcopper.pdf
[14] Sanders, et al. (2018). Bleeding, cramping, and satisfaction among new copper IUD users: A prospective study. PLOS. Retrieved from https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6221252/
[15] Tudorache, et al. (2017). Birth Control and Family Planning Using Intrauterine Devices (IUDs). Retrieved from https://www.intechopen.com/books/family-planning/birth-control-and-family-planning-using-intrauterine-devices-iuds-
[16] World Health Organization Department of Reproductive Health and Research and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (2018) Family Planning: A Global Handbook for Providers. Baltimore and Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/260156/9780999203705-eng.pdf?sequence=1
[17] World Health Organization. (2016). Selected practice recommendations for contraceptive use. Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/252267/9789241565400-eng.pdf?sequence=1


lang Kiswahili