Kondomu ya ndani (Kondomu ya kike) | Find My Method
 

Last modified on October 14th, 2020

internal-condom
 • Inawapa wanawake udhibiti zaidi.
 • Chaguo nzuri kwa wachumba walio na mzio wa ulimbe wa mpira
 • Ufanisi: Itakuwa bora ikitumika kamilifu; Ina ufanisi zaidi ikitumika pamoja na dawa ya kuuwa mbegu za kiume. Ikitumika inavyofaa, watu 95 kati ya 100 wataweza kuzuia mimba. Lakini watu wengi hawatumii kondomu inavyofaa- kwa hali hiyo, watu 79 pekee kati ya 100 wanaotumia njia hii wataweza kuzuia mimba.
 • Madhara:Kwa kawaida hakuna, lakini inaweza sababisha mwasho kwako au kwa mpenzi wako.
 • Jitihada:nyingi. Lazima utumie kondomu mpya KILA wakati unafanya ngono.

Ufupisho

Female Condoms

Summary Internal Condoms

Kondomu ya ndani -au kondomu ya kike-ni kipochi kinachoingizwa kwenye uke au mkundu wako. Kondomu za ndani (kike) zinafanya kazi sawa na kondomu za nje (kiume), isipokuwa kwamba unaivaa ndani badala ya kuivaa kwenye uume. Zinaweka mbegu za kiume ndani ya kondomu na nje ya uke wako au mkundu.

Maelezo

[10]
Kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa. kondomu za ndani (kike) zinaweza kusaidia kukukinga dhidi ya magonjwa mengi ya zinaa, ikiwemo virusi vya ukimwi.

Kondomu za ndani (kike) zinahitaji jitihada na kujitolea. Unahitaji kuhakikisha kwamba unatumia kondomu inavyofaa, kila wakati, ili ziwe na ufanisi.

Mwenzi wako anakataa kuvaa kondomu. Ikiwa mwenzi wako hatavaa kondomu, lakini bado unataka kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa, kondomu ya ndani (kike) ni chaguo nzuri.

Hauhitaji agizo la daktari. Ikiwa huwezi fika kwa mtoaji huduma za afya au (hutaki kuenda), unaweza kutumia kodomu za ndani (kike).

Ni bora kwa watu walio na mzio wa ulimbo wa mpira (latex). tofauti na kondomu za kiume nyingi, kondomu za ndani (kike) zimetengenezwa na plastiki au mpira bandia. Unaweza zitumia ikiwa una mzio wa ulimbo wa mpira.

Upatikanaji. Je! Ungependa kutumia njia hii? Angalia sehemu ya “Mbinu katika nchi yangu” ili ujifunze kinachopatikana

Jinsi ya kutumia

kondomu za ndani (kike) ni rahisi kutumia, lakini baada ya mazoea. Kumbuka, ikiwa hii ndio njia unastahabu,lazima uitumie KILA WAKATI.

Jinsi ya kuingiza kondomu ya ndani (kike)? [8]

 1. Kwanza, usiwe na haya. Kuvaa kondomu ya ndani (kike) inaweza kuwa sehemu ya kuongeza tamaa ya kingono kabla ya kuingiza uume kwenye uke. Ikiwa unaweza kuzungumza na mwezi wako kuhusu ngono, zungumza kuhusu jinsi mnavyoweza kutumia kondomu kuongeza ridhaa kwa maisha yenyu ya ngono.
 2. Nawa mikono kwa sabuni na maji. Wacha yakauke yenyewe kwa upepo bila kuguza chochote.
 3. Weka dawa za kuuwa mbegu za kiume au mafuta ya kulainisha nje ya sehemu ya mwisho iliyofungwa ya kondomu.
 4. Ikiwa umesimama au umeketi, panua miguu yako.
 5. Finya kabisa pamoja pande za mwisho wa kondomu zilizofungwa na ingiza kama tamponi.
 6. Sukuma pete ndani ya uke hadi mwisho inapoweza kufika. Sukuma ndani kabisa hadi ifike kwenye shingo ya kizazi.
 7. Toa kidole chako na uwache pete ya nje ining’inie karibu inchi moja nje ya uke wako. (Itaonekana la ajabu kidogo.)
 8. Ukitaka kutumia kondomu ya ndani (kike) kwa ngono ya mkundu, fuata taratibu sawa lakini kwenye mkundu.

Usijali ikiwa kondomu inasonga toka pande moja hadi ingine wakati wa ngono. Ikiwa mwanamume atateleza toka kwenye kondomu aingie ukeni au kwenye mkundu, toa kondomu kwa upole kisha uiingize tena. Kama kwa ajali atamwaga nje ya kondmu (kike) na ndani ya uke , zingatia njia za dharura za kuzuia mimba kuepuka hatari ya mimba.

Jinsi ya kutoa kondomu ya ndani (kike)? [7]

 1. Finya pete ya nje na uipindue uifunge kuzuia manii kumwagika nje.
 2. Vuta kondomu kwa upole
 3. Itupe kondomu mahali watoto hawafiki. Usiitupe kwenye choo cha maji. Itaziba mifereji.

Kutumia kondomu ya kawaida pamoja na kondomu ya ndani (kike) haikupi kinga maradufu. Inaongeza tu uwezekano wa kuraruka kwa zote mbili.[4]

Vidokezi na mbinu: Kabla ya kutumia kondomu ya ndani (kike), hakikisha umeangalia tarehe ya mwisho ya kutumia na uangalie ikiwa pakiti ina miraruo au mashimo.

 

Madhara

Kila mtu ni tofauti. Kile unachopitia pengine hakitafanana na mtu mwingine.

Mambo chanya:[8]

 • Inasaidia kukukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa
 • Pete ya nje inaweza kuchechemua kinembe chako
 • Hauhitaji agizo la daktari
 • Inaweza kutumika ikiwa una mzio wa ulimbo wa mpira
 • Inaweza kutumika pamoja na mafuta ya kulainisha yenye oili au yenye maji
 • Inabaki mahali pake hata ikiwa uume umelegalega

Mambo hasi: [8]

 • Inaweza sababisha mwasho
 • Watu wengine wana mzio kwa aina fulani ya mafuta ya kulainisha. Hili likifanyika, jaribu aina nyingine ya kondomu.
 • Inaweza kupunguza hisia za ngono wakati unafanya ngono
 • Kondomu zingine za ndani (kike) zinaweza kuwa na kelele fulani ya kuudhi (lakini aina mpya hazina)
 • Ni ngumu kukumbuka kutumia ikiwa umekuwa ukinywa pombe.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tuko hapa kukusaidia. kama bado unahisi sio ya kufaa, tuna mawazo ya njia zingine. Kumbuka tu: Ukiamua kubadilisha njia, hakikisha una kinga wakati unafanya mabadiliko. Kondomu za nje (kiume) zitakupa kinga bora wakati unatafuta njia itakayofaa mahitaji yako.

Na ikuwa ngumu kabisa kuingiza?

 • Kuingiza kondomu ya ndani (kike) kunapaswa kuendelea kuwa rahisi na matumizi ya mara nyingi. Jaribu kufanya mazoea ya kuiweka ndani wakati hauko karibu kufanya ngono ili uzoe.
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa bado haikuwi rahisi kuingiza na unawasiwasi kuhusu magonjwa ya zinaa, tumia kondomu za nje(kiume) badala yake.
  • Ikiwa hauna wasiwasi ya kukinga mangonjwa ya zinaa kwa wakati huu, zingatia njia ya uzuiaji mimba ambayo haihitaji uingize kitu chochote. IUD na vipandikizi zote mbili huingizwa kwenye kliniki.
 • Jaribu njia tofauti: vipandikizi; IUD

Na ikikwama kwenye uume? [10]

 • Jaribu kutumia mafuta ya kulainisha kidogo uone kama bado itakwama.
 • Bado haiendi sawa? Nyinyi wawili mkikubaliana, badilisha utumie kondomu za nje (kiume). Hizo pia zitakukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa.
  • Ikiwa hauna wasiwasi ya kukinga magonjwa ya zinaa, zingatia kutumia njia tofauti. Pete, kiraka, au sindano zinaweza kuwa chaguo bora kwako.
 • Jaribu njia tofauti: kondomu za nje (kiume); kiraka; pete; sindano

Kwanini kondomu ya ndani (kike) inatoa kelele fulani? [4]

 1. Jaribu kutumia mafuta ya kulainisha uone kama kelele itapungua. Aina mpya za kondomu za ndani (kike) hazina kelele, kwahivyo jaribu hizo.
 2. Bado haifanyi? Ikiwa atakubali, tumia kondomu. Zitakukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa pia.
  • Ikiwa hauna wasiwasi kuhusu magonjwa ya zinaa kwa wakati huu, zingatia njia tofauti. IUD, petekiraka, au sindano zinaweza kuwa chaguo bora kwako.
 3. Jaribu njia tofauti: kondomu; IUD

Na ikiwa mwanamume atahisi pete ya ndani? [7]

 • Ikiwa mwanamume atahisi pete ya ndani, huenda haujaiingiza ndani kabisa kwenye uke au mkundu. Jaribu kuisukuma ndani kidogo.
 • Bado haiendi sawa? Nyote wawili mkikubaliana, tumia kondomu za nje (kiume). Zitakukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa pia.
  • Ikiwa hauna wasiwasi kuhusu magonjwa ya zinaa na huyu mwenzi wako, zingatia njia ambazo hazizui manii. The Sindano  na vipandikizi zote mbili zina ufanisi wa juu.
 • Jaribu njia tofauti: kondomu ya nje (kiume); vipandikizi; sindano

Je, kutumia kondomu mbili ni bora kuliko kutumia moja kwa kukinga magonjwa ya zinaa na kuzuia mimba?[10]

 • Kutumia kondomu, mbili kwa hakika SIO bora kuliko kutumia moja. Kondomu mbili zitaleta msuguano zaidi, na hivyo kuongeza uwezekano wa kondomu (moja kati yao ama zote mbili) kupasuka.
 • Ukitaka kuwa salama kabisa, tumia kondomu na njia ingine ya uzuiaji mimba yenye ufanisi.
 • Jaribu njia tofauti: vipandikizi

Kwanini kondomu ya ndani (kike) inaning’inia nje nikisimama?[10]

 • Unaweza ingiza kondomu ya ndani (kike) hadi masaa 8 kabla ya kufanya ngono.
 • Ukisimama ikiwa ndani, kondomu ya ndani (kike) inaweza kuning’inia kidogo nje ya uke au mkundu. Ikiwa unataka kuiingiza mapema lakini isining’inie nje, jaribu kuvaa chupi isiyobana kuzuia sehemu ya nje ya kondomu kuning’inia.

 

 

 

References

[1] Beksinska, et al. (2015). A randomized noninferiority crossover controlled trial of the functional performance and safety of new female condoms: an evaluation of the Velvet, Cupid2, and FC2. Contraception, Volume 92, Issue 3,. Retrieved from https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/26002805
[2] Dr Marie Marie Stopes International. (2017). Contraception. Retrieved from http://www.mariestopes.org.au/wp-content/uploads/Contraception-brochure-web-200417.pdf
[3] FPA the sexual health charity. (2015). Your guide to male and female condoms. Retrieved from https://www.victoriaparkhealthcentre.co.uk/website/C82124/files/male-and-female-condoms-your-guide.pdf
[4] IPPF and UNFPA. (2010). MYTHS, MISPERCEPTIONS AND FEARS: ADDRESSING CONDOM USE BARRIERS. New York . Retrieved from http://bibliobase.sermais.pt:8008/BiblioNET/Upload/PDF4/002988.pdf
[5] Mome, et al. (2018). Effectiveness of female condom in preventing HIV and sexually transmitted infections: a systematic review protocol. BMJ Open. Retrieved from https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6078242/
[6] Reproductive Health Access Project. (2015). FEMALE/INTERNAL CONDOM. Retrieved from https://www.reproductiveaccess.org/wp-content/uploads/2015/03/factsheet_female_condom.pdf
[7] Society of Obstetricians and Gynaecologists of Canada. (2015). Canadian Contraception Consensus Chapter 5: Barrier Methods. JOGC Journal of Obstetrics and Gynaecology Canada , 37. Retrieved from https://www.jogc.com/article/S1701-2163(16)39376-8/pdf
[8] Shoupe, D. (2016). Barrier Contraceptives: Male Condoms, Vaginal Spermicides, and Cervical Barrier Methods. En D. Shoupe, The Handbook of Contraception: A Guide for Practical Management. Retrieved from http://eknygos.lsmuni.lt/springer/677/147-177.pdf
[9] Ting RS, et al. (2018). A pilot study on the functional performance and acceptability of an innovative female condom (Wondaleaf®) in Malaysia. Open Access J Contracept., 9. Retrieved from https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5804018/
[10] World Health Organization Department of Reproductive Health and Research and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (2018) Family Planning: A Global Handbook for Providers. Baltimore and Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/260156/9780999203705-eng.pdf?sequence=1
[11] World Health Organization. (2016). Selected practice recommendations for contraceptive use. Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/252267/9789241565400-eng.pdf?sequence=1


lang Kiswahili