
Vipandikizi ni njiti au kapsuli ndogo za plastiki zinazo ingizwa chini ya ngozi ya sehemu ya juu ya mkono wa mwanamke. Ni vidogo mno; kwa hakika, watu wengi hawawezi kuiona ikishaingizwa. Vipandikizi huachilia projestini, homoni inayozuia ovari kuachilia yai na hufanya ute kwenye mji wa mimba kuwa mzito-hivyo kuzuia mbegu za kiume kufikia yai. Inakinga dhidi ya mimba miaka hadi 5, ikilingana na aina utakayo chagua. kuna aina mbalimbali, ikiwemo Nexplanon, Jadelle na Levoplant.
Ipate kisha usahau mambo yake. Ikiwa hutaki kuwa na wasiwasi kuhusu njia yako ya kuzuia mimba, vipandikizi itakufaa. Mara tu ikiwa ndani, inaweza kubaki kwa miaka 3-4, kulingana na vipandikizi gani vimetumika.
Kazi rahisi. Hakuna kifurushi, au cha kununuliwa kwenye duka la dawa – hakuna kinachoweza kupotea au kusahaulika.
Faragha kamili. Hakuna mtu anaweza jua ukiwa na vipandikizi. Hakuna kifurushi, wala kitu chochote unastahili kufanya kabla tu ya kufanya ngono.
Swala la mimba. Unapaswa kuwa na uwezo wa kushika mimba wakati wowote baada ya kutolewa Vipandikizi. Vikitolewa , lakini hautaki kushika mimba, hakikisha umejikinga kwa nji nyingine mara hio hio.
Upatikanaji. Je, ungependa kutumia njia hii? Njia hii inapatikana kwa wingi. Hata hivyo, kuna aina zingine hazipatikani katika nchi zingine. Tazama sehemu ya “Njia zinazopatikana nchini mwangu” ili kujifunza zaidi
Mara tu iko ndani, hakuna unachohitaji kufanya. Vipandikizi vina baki chini ya ngozi yako,na kukupa kinga dhidi ya mimba hadi miaka 3-5, kulingana na vipandikizi ulivyotumia [4].
Kuingiza vipandikizi. Mtoaji atakusanya taarifa yako ya afya na kufanya uchunguzi wa kimatibabu. Kisha watafanya ganzi sehemu mdogo wa juu ya mkono wako kwa dawa za kupunguza maumivu na kuingiza njiti au kapsuli chini ya ngozi yako. Hivyo tu [7].
Ikiwa utawekewa vipandikizi siku tano za kwanza za hedhi yako, unakingwa dhidi ya mimba mara hio hio. Ikiwa ni nje ya hizi siku tano za kwanza, utahitaji kutumia njia ingine ya kujikinga kwa wiki inayofuata. Kondomu za nje (kiume), Kondomu za ndani (kike), diaframu, sponji, au njia za dharura za kuzuia mimba )[10].
Wakati wa kutoa vipandikizi, mtoaji wako tena atafanya ganzi sehemu mdogo wa juu ya mkono wako, akate sehemu mdogo kabisa wa ngozi yako, na atoe vipandikizi. Ikiwa bado unataka kuendelea kutumia vipandikizi, wanaweza kukuwekea ingine wakati huo huo. [5].
Kila mtu ni tofauti. Kile unachopitia pengine hakitafanana na mtu mwingine.
Mambo chanya: Kuna vitu vingi kuhusu vipandikizi ambavyo ni vizuri kwa mwili wako na pia maisha yako ya ngono [8]
Mambo hasi: Kila mtu huwa na wasiwasi juu ya madhara hasi, lakini kwa wanawake wengi, hakuna shida. Ukipata madhara, huenda yakaisha. Kumbuka, unaingiza homoni mwilini mwako, kwahivyo inaweza kuchukua miezi michache mwili izoe.
Malalamiko ya kawaida zaidi [7]:
Malalamiko zisizo za kawaida zaidi [8]:
Ikiwa baada ya miezi 6 unahisi kwamba madhara yamezidi kiwango unachoweza kuvumilia, tumia njia ingine uwe na kinga. Kumbuka, kuna njia kwa kila mtu, kila mahali! Hakikisha tu kwamba umejikinga kwa kuanza kutumia njia ingine mara hio hio.
* Kwa idadi ndogo mno ya wanawake, kuna hatari ya madhara makubwa.
Tuko hapa kukusaidia. kama bado unahisi sio ya kufaa, tuna mawazo ya njia zingine. Kumbuka tu: Ukiamua kubadilisha njia, hakikisha una kinga wakati unafanya mabadiliko. Kondomu zitakupa kinga bora wakati unatafuta njia itakayofaa mahitaji yako.
Je, napaswa kuwa na wasiwasi juu ya matone ya damu?
Na ikiwa sipendi hali ya kutokwa na matone ya damu?
Na ikiwa nataka kushika mimba?
Na ikiwa hisia zangu zitabadilika badilika, niwe na kuvimbiwa, au niwe na wasiwasi?[11]
Na ikiwa sitaki kitu mwilini mwangu kwa muda mrefu?
Nitajuaje niko na mimba ikiwa sipati hedhi ya kawaida?
Na ikiwa nataka kushika mimba?
[1] Allen, et al. (2016). Hormonal Contraception. In Williams Textbook of Endocrinology. Retrieved from https://www.sciencedirect.com/science/article/pii/B9780323297387000186
[2] Dr Marie Marie Stopes International. (2017). Contraception. Retrieved from http://www.mariestopes.org.au/wp-content/uploads/Contraception-brochure-web-200417.pdf
[3] FSRH The Faculty of Sexual & Reproductive Healthcare. (Amended 2019). UK MEDICAL ELIGIBILITY CRITERIA. RCOG, London. Retrieved from https://www.fsrh.org/standards-and-guidance/documents/ukmec-2016/
[4] FPA the sexual health charity. (2017). Your guide to the contraceptive implant. Retrieved from https://www.fpa.org.uk/sites/default/files/contraceptive-implant-your-guide.pdf
[5] Family Planning NSW. (2013). The contraceptive implant. Retrieved from https://www.fpnsw.org.au/sites/default/files/assets/CONTRACEPTIVE%20IMPLANT.pdf
[6] Kukstas, C. (2016). The contraceptive implant. Retrieved from https://journals.sagepub.com/doi/abs/10.1177/1755738016634119
[7] Pathfinder International. (2016). Contraceptive Implants: Clinical Training. Retrieved from https://www.pathfinder.org/publications/implants-training/
[8] Rowlands, S., & Searle, S. (2014). Contraceptive implants: current perspectives. Open Access Journal of Contraception. Retrieved from https://www.dovepress.com/contraceptive-implants-current-perspectives-peer-reviewed-article-OAJC
[9] Reproductive Health Access Project. (2018). PROGESTIN IMPLANT. Retrieved from https://www.reproductiveaccess.org/wp-content/uploads/2015/03/factsheet_implant.pdf
[10] SHINE SA. (2018). Contraceptive implant . Retrieved from https://www.shinesa.org.au/media/product/2015/04/Contraceptive-implant.pdf
[11]World Health Organization Department of Reproductive Health and Research and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (2018) Family Planning: A Global Handbook for Providers. Baltimore and Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/260156/9780999203705-eng.pdf?sequence=1
[12] World Health Organization. (2016). Selected practice recommendations for contraceptive use. Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/252267/9789241565400-eng.pdf?sequence=1