Uelewa wa kizazi | Find My Method
 

Last modified on October 14th, 2020

sponge
 • Njia zinazohusisha Uelewa wa Kizazi hazina gharama. Pia, hazina homoni.
 • Ufanisi: Njia za Uelewa wa Kizazi hazina ufanisi sana. Zitakuwa bora zaidi zikitumika kamilifu.
  • Matumizi kamilifu:

   95-99%

  • Matumizi ya kawaida:

   76-88%

 • Madhara: Hakuna
 • Jitihada: Nyingi. Uchunguzi wa kila siku unahitajika ili kutumia sahihi njia zinazohusisha Uelewa wa Kizazi

Ufupisho

Natural Family Planning

Summary Rhythm Method

Njia zinazohusisha Uelewa wa Kizazi ni aina za njia za asili za uzazi wa mpango. Njia hizi zinahitali uweke rekodi za mzunguko wako wa hedhi, ili ujue siku ambazo unaweza kushika mimba. Kilicho kigumu zaidi ni kutambua hizo ziku. Tunakupa mbinu kadha za kuchunguza kizazi chako na kukusaidia kutambua siku unazoweza kushika mimba. Kwa wanawake walio na hedhi isiyotabirika, ikijumuisha vijana, hii njia sio bora. [9]

Aina za Uelewa wa Kizazi:

Njia ya siku Sanifu (SDM): Unaweza kutumia njia hii ikiwa mzunguko wa hedhi yako ni wa kati ya siku 26 na siku 32. Utahitaji kuweka rekodi ya hedhi yako na kubainisha ni lini hauwezi kushika mimba.[3]

SikuMbili (TDM): Kwa njia hii, unahitaji kuangalia kwa makini ute wa ukeni kuona wakati wa rutuba.

Ute wa Ukeni: Mwili wako hutengeneza ute maaulum siku za rutuba. Njia hii ni ya kuchunguza ute wako wa ukeni.[8]

Joto la mwili (BBT): Njia hii inahitaji urekodi joto la mwili wako kila asubuhi kubainisha ikiwa ni wakati wa kupevuka kwa yai.

Uchunguzi wa joto la mwili, ute wa ukeni na dalili zingine za rutuba(Symptothermal): Mwili wako una dalili mingi za kuonesha kwamba unaweza kushika mimba. Njia hii inachunguza baadhi zao kwa wakati mmoja. Hii inajumuisha ni kwa kiasi gani unahisi shingo ya kizazi imefungulika

Kunyonyesha (Lactational/LAM): Kunyonyesha hupunguza rutuba kwa asili. Njia hii itafanya kazi ikiwa umejifungua karibuni. Ili njia hii ifaulu, unahitaji kumnyonyesha tu mtoto wako bila kumpatia vyakula au vinywaji vingine .

Maelezo

[11]
Unahitaji kufahamu mwili wako zaidi. Uelewa wa kizazi unaweza kukusaidia kuzuia mimba. Pia ni njia nzuri ya kuelewa bora mwili wako. Utaona mabadiliko na utaelewa bora mzunguko wako wa hedhi.

Haujali kushika mimba. Viwango vya kufeli viko juu ikiwa hautatumia njia hii sahihi. Ikiwa hautaki kushika mimba na haufahamu vizuri njia ya Uelewa wa Kizazi, chagua njia ingine.Ikiwa bado unataka kuijaribu, tumia njia ya pili kama vile kondomu kila wakati unafanya ngono wakati bado unajifahamisha na njia hii.

Nidhamu binafsi kamili. Wewe na mwezi wako mtahitaji kukubaliana kutumia njia hii. Pia unapaswa kuufahamu mwili wako vizuri.

Haujali kutofanya ngono, au kutumia njia ingine. Ukitumia njia hii, utahitaji kurekodi siku ambazo unaweza kushika mimba kila mwezi. Hizo siku, utahitaji kuepuka ngono au kutumia njia bila homoni. Ikiwa hautaweza kuepuka ngono au kutumia njia ingine ya uzuiaji mimba, usitumie njia za uzuiaji mimba zinazohusisha Uelewa wa kizazi.

Unataka njia ambayo haileti madhara. Njia hii haiongezi homoni zingine kwenye mwili wako. Watu wengi wanaotumia njia hii wanataka kitu ambacho hakiathiri miili yao.

Hauhitaji agizo la daktari. Ikiwa hautaki kutumia homoni, hii ni chaguo moja.

Jinsi ya kutumia

Njia zinazohusisha Uelewa wa Kizazi ni rahisi. Rekodi mizunguko za hedhi na usifanye ngono siku unazoweza kushika mimba. Ukifanya ngono siku hizo, tumia njia ya pili, kama kondomu – ya nje (kiume) au ya ndani (kike) – au diaframu.

Unaweza kuchunguza mzunguko wako wa hedhi kwa mbinu tofauti. Kutumia mbinu mbili au zaidi itakusaidia kuhakikisha usahihi. Utahitaji kuchunguza kwa makini mabadiliko kwa mwili wako na upige hesabu mahali uko kwa mzunguko wako wa hedhi. Hii itachukua jitihada nyingi na kujitolea. Kabla ya kuchagua njia hii, hakikisha unaelewa kile utapaswa kufanya. Kuwa tayari kuepuka ngono siku saba kila mwezi, au kutumia njia ya pili hizo siku.[5]

Njia ya siku Sanifu. Hii njia itafanya kazi ikiwa mzunguko wa hedhi yako ni kati ya siku 26 na siku 32. Jifunze zaidi kuhusu njia hii.[3]

SikuMbili. Kila siku, utachunguza kwa makini ikiwa una ute wa ukeni. Ukiona ute wowote, jana au leo, unaweza kushika mimba. Usifanye ngono siku hizo, na ukiamua kufanya ngono, tumia njia ingine ya uzuiaji mimba. Pata taarifa zaidi hapa.

Njia ya kuchunguza ute wa ukeni. Unahitaji kuchunguza ute wa ukeni kila siku. Unaweza shika mimba kuanzia mwazo wa kutoka kwa ute wa ukeni ( wakati ute uko angavu, una nyooka, unateleza na yenye unyevu) hadi siku ya tatu baada ya ute kuisha. Tumia njia hii pamoja na njia zingine za kuchunguza mwili (Symptothermal) au njia ya Siku sanifu[8]

Joto la msingi la mwili (BBT). Utahitaji kupima joto la mwili wako kila asubuhi kabla usimame. Iandike kwenye chati.Tumia njia hii pamoja na njia zingine za kuchunguza mwili (Symptothermal) au njia ya Siku sanifu[1]

Uchunguzi wa joto la mwili, ute wa ukeni na dalili zingine za rutuba (Symptothermal). Njia hii inachanganyisha njia mbalimbali za Uelewa kizazi kutabiri siku ambazo unaweza kushika mimba. Inaweka rekodi za joto la msingi la mwili na ute wa ukeni. Unaweza kupata taarifa zaidi hapa.

Njia ya kunyonyesha. Unaweza kuzuia mimba kwa kunyonyesha mtoto hadi miezi 6 baada ya kumpata. Hii hufanya kazi tu ukifuata mambo haya 3 hapa chini:

 1. Haujapata hedhi tangu umzae mtoto wako.
 2. Unamnyonyesha mtoto (bila kumpa vyakula au vinyuaji vingine)
 3. Unamnyonyesha mtoto angalau masaa 4 mchana na masaa 6 usiku.

Unaweza kujifunza zaidi kuhusu njia ya kunyonyesha (LAM) hapa..

Madhara

Kila mtu ni tofauti. Kile unachopitia pengine hakitafanana na mtu mwingine.

Mambo chanya:[7]

 • Ni njia bila malipo-isipokuwa bei ya kipimajoto au shanga za mzunguko wa hedhi.
 • Hauhitaji agizo la daktari
 • Hakuna homoni zinaongezwa mwilini mwako.
 • Hakuna homoni, kwahivyo usiwe na wasiwasi kuhusu madhara. Wasiwasi wako ni kuhusu uwezekano wa kushika mimba
 • Njia hii inakusaidia kufahamu zaidi mwili wako na jinsi inavyofanya kazi

Mambo hasi:[5]

 • Unahitaji kuchukua wakati wako kupanga na kuchukua rekodi.
 • Njia hii inahitaji kujidhibiti
 • Inahitaji kujinyima ngono (au utumie njia ingine) angalau wiki moja kila mzunguko wa hedhi.
 • Wewe na mwenzi wako munahitaji kushirikiana.
 • Njia ya kalenda na njia ya siku sanifu hazifanyi kazi kwa wanawake wanaopata hedhi isiyotabirika.
 • Ikiwa umewacha kutumia njia ya homoni hivi karibuni, njia zinazohusisha uelewa wa kizazi zinaweza kuleta hatari. Homoni zinaathiri hedhi yako, na hali hii inafanya njia za uelewa wa kizazi ziwe na ufanisi mdogo mwanzoni. Tumia njia bila homoni wakati bado unajifahamisha na mzunguko wako wa hedhi.
 • Ni ngumu kufuata mpango ikiwa umelewa

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tuko hapa kukusaidia. Kama bado unahisi sio ya kufaa, tuna mawazo ya njia zingine. Kumbuka tu: Ukiamua kubadilisha njia, hakikisha una kinga wakati unafanya mabadiliko.

Na ikiwa nimefanya ngono siku isiyofaa?[11]

 • Ikiwa imepita siku 5 au chache tangu ufanye ngono,na hautaki mimba, tumia njia za dharura za uzuiaji mimba. Ikiwa ni zaidi ya siku 5 zilizopita, enda upimwe mimba ikiwa hedhi yako ya kufuatia itachelewa.
 • Ukitaka kufanya ngono bila kinga siku ambazo kuna uwezekano wa kushika mimba, na hutaki kushika mimba, pengine uzingatie njia ingine rahisi.
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa unapata shida kubaini siku ambazo unaweza kushika mimba, pengine uzingatie njia kama IUD ama vipandikizi.
  • Unapenda kwamba hakuna homini kwa njia ya uelewa wa kizazi? Jaribu IUD au njia za kuzuia manii kama kondomu.
 • Jaribu njia tofauti: kondomu za ndani (kike); vipandikizi; IUD; kondomu za nje (kiume)

Na ikiwa siwezi kukumbuka kupima joto la mwili, kuweka rekodi za hedhi au kuchunguza ute wa ukeni kila siku?[1]

 • Njia hii itafanya kazi ikiwa tu umejitolea kuitumia sahihi na kwa msimamo. Kuna nyenzo nyingi kama vile apu, vipimajoto, na shanga za mzunguko wa hedhi za kukusaidia kuchunguza na kuweka rekodi za hedhi yako.
 • Bado haiendi sawa? ikiwa hauna hakika kwamba unaweza kuchunguza dalili zako za rutuba kila siku, zingatia njia ingine inayohitaji jitihada kidogo.
  • IUD au Vipandikizi ni nzuri kwa kinga ya miaka, sindano kwa kinga ya miezi, pete inabadilishwa tu kila mwezi, na unabadilisha kiraka mara moja kwa wiki.
 • Jaribu njia tofauti: Vipandikizi; IUD;
  kiraka
  ; pete; sindano

Na ikiwa tunataka kufanya ngono siku za rutuba?[7]

References

[1] FPA the sexual health charity. (2015). Your guide to natural family planning. Retrieved from https://www.sexwise.fpa.org.uk/sites/default/files/resource/2017-08/natural-family-planning-your-guide.pdf
[2] Manhart, et al. (2013). Fertility awareness-based methods of family planning: A review of effectiveness for avoiding pregnancy using SORT. ACOFP American College of Osteopathic Family Physicians. Retrieved from https://www.sympto.org/data/Fertility_awareness-based_methods_of_family_planning_2013.pdf
[3] Marstona, C. A., & Church, K. (2016). Does the evidence support global promotion of the calendar-based Standard Days Method® of contraception? Elsevier. Retrieved from https://www.contraceptionjournal.org/article/S0010-7824(16)00005-6/pdf
[4] Peragallo, et al. (2018). Effectiveness of Fertility Awareness–Based Methods for Pregnancy Prevention: A Systematic Review. The American College of Obstetricians. Wolters Kluwer Health, Inc. Retrieved from https://www.replyobgyn.com/wp-content/uploads/2019/01/ACOG_Urrutia-Systematic-Review.pdf
[5] Reproductive Health Access Project. (2019). Fertility Awareness. Retrieved from https://www.reproductiveaccess.org/wp-content/uploads/2014/12/nfp.pdf
[6] Smith, A. (2019). Fertility Awareness Based Methods (FABMs): Evaluating and Promoting Female Interest for Purposes of Health Monitoring and Family Planning. University of Arkansas: Theses and Dissertations. Retrieved from https://scholarworks.uark.edu/cgi/viewcontent.cgi?article=4837&context=etd
[7] Society of Obstetricians and Gynaecologists of Canada. (2015). Canadian Contraception Consensus Chapter 4: Natural Family Planning. JOGC Journal of Obstetrics and Gynaecology Canada. Retrieved from https://www.jogc.com/article/S1701-2163(16)39375-6/pdf
[8] Thijssen, et al. (2014). ‘Fertility Awareness-Based Methods’ and subfertility: a systematic review. FAcTs VieWs Vis Obgyn. Retrieved from https://www.researchgate.net/publication/267872637_’Fertility_Awareness-Based_Methods’_and_subfertility_a_systema-tic_review
[9] The American College of Nurse-Midwives. (2018). Fertility Awareness Methods. Journal of Midwifery and Women´s Health , 63. Retrieved from https://onlinelibrary.wiley.com/doi/epdf/10.1111/jmwh.12906
[10] World Health Organization. (2016). Selected practice recommendations for contraceptive use. Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/252267/9789241565400-eng.pdf?sequence=1
[11] World Health Organization Department of Reproductive Health and Research and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (2018) Family Planning: A Global Handbook for Providers. Baltimore and Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/260156/9780999203705-eng.pdf?sequence=1


lang Kiswahili