Diaframu | Find My Method
 

Last modified on October 14th, 2020

diaphragm

[7]

 • Inaanza kufanya kazi mara hiohio. Inaweza kuwekwa masaa kabla ya kufanya ngono, na haiathiri homoni zako
 • Ufanisi: diaframu ina ufanisi wa wastani- ni bora kuliko dawa za kuuwa mbegu za kiume. Kwa matumizi kamilifu, wanawake 94 kati ya 100 wataweza kuzuia mimba. Kwa matumizi ya kawaida, diaframu itazuia mimba kwa wanawake 88 kati ya 100 wanaoitumia.
 • Madhara: haileti matatizo kwa wengi, lakini mwasho au maambukizi katika njia ya mkojo yanawezekana.
 • Jitihada: nyingi- lazima uiweke mahali pake kila wakati unafanya ngono.Lakini unaweza kuiwacha ndani kwa masaa 24.
 • Haikukingi dhidi ya magonjwa ya zinaa (STIs).

Ufupisho

Diaphragm Birth Control

Contraceptive Diaphragm Summary

Diaframu ni kijikombe chenye umbo wa kuba na kilio na kina fupi,kilio tengenezwa na kinachoitwa silicone. Unaingiza diaframu kwenye uke wako. inafunika shingo ya kizazi na inazuia mbegu za kiume kuingia. Unahitaji kuitumia pamoja na dawa za kuuwa mbegu za kiume ili ifanye kazi kwa ufanisi.

Maelezo

[10]

Unaridhika na mwili wako. Ikiwa hauwezi kuweka vidole vyako ndani ya uke wako, pengine diaframu haikufai. Ni kama kuweka tamponi. Ikiwa unaweza kufanya hivyo, basi unaweza kujifundisha kutumia diaframu.

Inahitaji nidhamu. Unahitaji kukumbuka kuingiza diaframu kabla ya kufanya ngono.Na unapaswa kuikumbuka kila wakati unafanya ngono. Inahitaji nidhamu binafsi na mpango. Lakini unaweza kuibeba ukitaka.

Upatikanaji. Kuna aina mbili za diaframu ambazo zinapatikana kwa kawaida. Ungependa kutumia njia hii? Tazama sehemu yetu ya ” Njia za uzuiaji mimba katika nchi yangu”ili kujifunza kuhusu njia zinazopatikana kwenye mtaa wako.

Maswala ya mzio. Ikiwa una mzio wa silicone au  dawa za kuuwa mbegu za kiume, haupaswi kutumia diaframu.

Swala la mimba. Utaweza kushika mimba punde baada ya kuwacha kutumia diaframu. Ikiwa hutaki mimba, tumia njia ingine ya uzuiaji mimba punde baada ya kuwacha kutumia diaframu.

 

Jinsi ya kutumia

Diaframu inaweza kuingizwa kabla tu ya ngono. Unaweza kuiingiza pia masaa machache kabla ya ngono. Haijalishi unaiingiza wakati mgani, hakikisha unaiwacha ndani angalau masaa 6 baada ya kufanya ngono. Ikiwa utafanya ngono tena siku hiyo, wacha diaframu mahali pake na uingize dawa zaidi za kuuwa mbegu za kiume ndani kabisa mwa uke. Usiwache diaframu ndani zaidi ya masaa 24.

 

Kabla ya kuiingiza ndani. ongeza karibu milimita 5 ya dawa za kuuwa mbegu za kiume kwenye sehemu ya ndani ya diaframu. Paka dawa zingine kwenye mzingo yake pia. ( sio nyingi sana ama itateleza na kutokwama vizuri). Dawa zingine za kuuwa mbegu za kiume zimetengenezwa maalum kwa matumizi ya diaframu, na zinakuja pamoja na kifaa cha kuipaka ambacho unaweza kutumia ikiwa utafanya ngono zaidi ya mara moja ndani ya masaa 6 ( Utahitaji kuongeza dawa zaidi za kuuwa mbegu za kiume). Jeli yoyote ya uzuiaji mimba au dawa za kuuwa mbegu za kiume zitafanya kazi, isipokuwa aina za utando au tembe za kuingizwa. Usisahau kuangalia tarehe ya mwisho kutumika. Ikiwa imepita, utahitaji kununua dawa mpya ya kuuwa mbegu za kiume.[3]

 

Jinsi ya kuiingiza. Kuingiza diaframu kunaonekana ngumu lakini sio hivyo. Hizi ndizo hatua za kuingiza:[5]

 1. Nawa mikono kwa sabuni na maji. Wacha yakauke yenyewe kwa upepo bila kuguza chochote.
 2. Kagua diaframu yako kuona kama ina mashimo na maeneo dhaifu. Kuijaza na maji safi ni mbinu mzuri ya kufanya hivyo- ikiwa maji yanavuja,kuna shimo. Diaframu yako ikiwa na shimo inamaanisha kwamba haifanyi kazi vizuri na unaweza kushika mimba.
 3. Weka karibu milimita 5 ya dawa za kuuwa mbegu za kiume kwenye diaframu. Paka zingine kwenye mzingo yake pia.
 4. Ikiwa umeketi au umesimama, panua miguu yako.
 5. Tenganisha midomo za nje za uke kwa mkono mmoja. Tumia mkono mwingine kuchuna mzingo wa diaframu na kuikunja iwe nusu.
 6. Weka kidole chako cha shahada katikati mwa mkunjo, ili ushikilie diaframu vizuri na thabiti. (Utakuwa unaguza dawa ya kuuwa mbegu za kiume)
 7. Sukuma diaframu ndani ya uke, ndani kabisa iwezekanavyo. Hakikisha umefunika shingo ya kizazi.

 

Unafanya ngono tena? Unapaswa kuwacha diaframu ndani kwa masaa 6 baada ya ngono. Ukifanya ngono mara ya pili ndani ya masaa hizo 6, kwanza weka dawa zaidi za kuuwa mbegu za kiume. Utaanza kuhesabu masaa 6 zingine, kutoka mara ya mwisho ulifanya ngono.

 

Jinsi ya kutoa diaframu. Ni hivi:[5]

 1. Nawa mikono tena. Tumia sabuni na maji. Wacha mikono yako yakauke yenyewe kwa upepo bila kuguza chochote
 2. Ingiza kidole chako cha shahada ndani ya uke na uiingize kwenye sehemu ya juu ya mzingo wa diaframu.
 3. Vuta diaframu chini kisha nje.

 

Unapata matatizo? Uliza daktari wako kuhusu kupata kifaa cha kuiingiza, au zingatia kutumia njia ingine.

 

Mwisho, tunza diaframu yako vizuri kwa vile inaweza tumika kwa miaka mingi.

 1. Baada ya kuitoa, ioshe kwa sabuni kidogo na maji ya uvuguvugu.
 2. Wacha ikauke kwa upepo.
 3. Usitumie poda au mafuta ya kulainisha yenye oili (kama Vaseline, losheni au krimu) kwenye diaframu yako.

 

Vidokezi na Mbinu

Wakati unaingiza diaframu, hakikisha kwamba sehemu kubwa ya dawa ya kuuwa mbegu za kiume inabaki ndani ya mkunjo wa diaframu, mahali ambamo itakuwa na ufanisi wa juu.

 

Madhara

Kila mtu ni tofauti. Kile unachopitia pengine hakitafanana na mtu mwingine.

Mambo chanya: Kuna vitu vingi kuhusu diaframu ambavyo ni vizuri kwa mwili wako na pia maisha yako ya ngono. [9]

 • Unaweza kuingiza diaframu masaa kabla ya ngono.
 • Unaweza kufanya ngono mara mingi unavyotaka ikiwa ndani ( bora tu uongeze  dawa zaidi za kuuwa mbegu za kiume kila mara)
 • Wewe au mwenzi wako hamupaswi kuhisi diaframu
 • Haina homoni
 • Inapunguza hatari ya ugonjwa wa uvimbe wa fupanyonga na utasa unaosababishwa na kuziba kwa mirija (tubal infertility)/li>
 • Inaweza kutumika wakati unanyonyesha

Mambo hasi:[4]

 • Wanawake wengine wanapata ugumu wa kuingiza diaframu
 • Inaweza kusababisha mwasho kwenye uke
 • Wanawake wengine wanapata maambukizi kwenye njia ya mkojo mara nyingi.
 • Lazima uiweke kila wakati unafanya ngono, hata iwe nini.
 • Ikiwa una mzio wa dawa za kuuwa mbegu za kiume ama silicone, usitumie diaframu
 • Inaweza kusukumwa kutoka mahali pake na uume mkubwa, mwanamume anaposukuma kwa nguvu, au staili fulani za ngono
 • Unahitaji agizo la daktari
 • Itakuwa ngumu kukumbuka ikiwa umekunya pombe

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tuko hapa kukusaidia. Kama bado unahisi sio ya kufaa, tuna mawazo ya njia zingine. Kumbuka tu: Ukiamua kubadilisha njia, hakikisha una kinga wakati unafanya mabadiliko. Kondomu zitakupa kinga bora wakati unatafuta njia itakayofaa mahitaji yako.

Na ikiwa diaframu itasababisha mwasho? [7]

 • Mwasho inaweza kusababishwa na mzio wa dawa za kuuwa mbegu za kiume. Ikiwa mwasho ni kidogo, jaribu aina ingine ya dawa ya kuuwa mbegu za kiume.
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa mwasho ni mkali na hauishi hata baada ya kujaribu aina zingine za dawa za kuuwa mbegu za kiume, zingatia njia ingine ambayo haihitaji matumizi ya dawa za kuuwa mbegu za kiume.
 • Jaribu njia tofauti: Vipandikizi; IUD; kiraka; tembe; pete; sindano

Na ikiwa diaframu ni ngumu kuingiza na/ au kutoa?[2]

 • Hii inaweza kukuwa rahisi zaidi kwa mazoea. Ikiwa bado haujasoma sehemu yetu ya jinsi ya kutumia, isome.
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa mazoea hayajasaidia, zingatia kutumia njia ambayo haihitaji wewe kuingiza chochote ndani ya uke. Ikiwa unataka kutumia njia inayozuia manii, zingatia ile hauhitaji kuingiza ndani yako, kama vile  kondomu za nje (kiume).
 • Jaribu njia tofauti: Vipandikizi; IUD; kondomu ; kiraka; tembe ; pete; sindano

Kwanini napata maambukizi ya njia ya mkojo kila mara?[7]

 • Wanawake wengine wanapata maambukizi ya njia ya mkojo wakitumia diaframu. Kukojoa kabla ya kuingiza diaframu kunaweza kusaidia. Kojoa tena baada ya kufanya ngono.
 • Pia unaweza kuenda kwa mtoaji huduma za afya kuhakikisha kwamba diaframu inaingia sahihi.
 • Bado haiendi sawa? Ikiwa bado unapata maambukizi ya njia ya mkojo na unataka kubadilisha njia, zingatia njia ambayo hauhitaji kuingiza kila wakati unafanya ngono.
 • Jaribu njia tofauti: Vipandikizi; IUD; kiraka; tembe; sindano

References

[1] Cornell Health. (2019). Using a Diaphragm. Cornell University , New York . Retrieved from https://health.cornell.edu/sites/health/files/pdf-library/using-a-diaphragm.pdf
[2] CHIJIOKE, M. K. (2016). SPERMICIDES AND DIAPHRAGMS. UNIVERSITY OF BENIN CITY: DEPARTMENT OF HEALTH, SAFETY AND ENVIRONMENTAL EDUCATION. Retrieved fromhttps://www.academia.edu/24646826/SPERMICIDES_AND_DIAPHRAGMS
[3] FPA the sexual health charity. (2015). Your guide to diaphragms and caps. Retrieved from https://www.fpa.org.uk/sites/default/files/diaphragms-and-caps-your-guide.pdf
[4] Family Planning NSW. (s.f). Single-Size Contraceptive Barrier Device – CAYA® DIAPHRAGM. Retrieved from https://www.fpnsw.org.au/sites/default/files/assets/caya_diaphragm_fs_1.pdf
[5] Reproductive Health Access Project. (2019). DIAPHRAGM Caya® and Milex®. Retrieved from https://www.reproductiveaccess.org/wp-content/uploads/2014/12/factsheet_diaphragm.pdf
[6] Reproductive Health Supplies Coalition. (2013). Diaphragm. Reproductive Health Supplies Coalition, Caucus on New and Underused Reproductive Health Technologies. Retrieved from https://www.rhsupplies.org/fileadmin/uploads/rhsc/Working_Groups/New_Underused_RH_Technologies_Caucus/Documents/Technical_Briefs/rhsc-brief-diaphragm_A4.pdf
[7] Society of Obstetricians and Gynaecologists of Canada. (2015). Canadian Contraception Consensus Chapter 5: Barrier Methods. JOGC Journal of Obstetrics and Gynaecology Canada , 37. Retrieved from https://www.jogc.com/article/S1701-2163(16)39376-8/pdf
[8] Schwartz, et al. (2015). Contraceptive Efficacy, Safety, Fit, and Acceptability of a Single-Size Diaphragm Developed With End-User Input. The American College of Obstetricians. Wolters Kluwer Health, Inc. Retrieved from https://www.essentialaccess.org/sites/default/files/Contraceptive_Efficacy_Safety_Fit.pdf
[9] Shoupe, D. (2016). Barrier Contraceptives: Male Condoms, Vaginal Spermicides, and Cervical Barrier Methods. En D. Shoupe, The Handbook of Contraception: A Guide for Practical Management. Retrieved from http://eknygos.lsmuni.lt/springer/677/147-177.pdf
[10] World Health Organization Department of Reproductive Health and Research and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (2018) Family Planning: A Global Handbook for Providers. Baltimore and Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/260156/9780999203705-eng.pdf?sequence=1
[11] World Health Organization. (2016). Selected practice recommendations for contraceptive use. Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/252267/9789241565400-eng.pdf?sequence=1


lang Kiswahili