Kondomu ya nje (kiume) | Find My Method
 

Last modified on October 14th, 2020

condom
 • Kondomu za nje (kiume) zinakinga dhidi ya magonjwa ya zinaa ikiwemo ukimwi, hazihitaji kuagiziwa na daktari, ni za bei nafuu au hata bure, na ni rahisi kupata.
 • Ufanisi: Zikitumika inavyofaa, watu 98 kati ya 100 wataweza kuzuia mimba.Lakini watu wengi hawatumii kondomu inavyofaa- kwa hali hiyo, watu 82 pekee kati ya 100 wanaotumia njia hii wataweza kuzuia mimba.
 • Madhara:Kwa kawaida hakuna, Labda uwe na mzio wa ulimbo wa mpira ( latex) au mzio wa dawa za kuuwa mbegu za kiume.
 • Jitihada:nyingi. Lazima utumie kondomu mpya KILA wakati unafanya ngono.

Ufupisho

Male Condoms

Summary External Condoms

Kondomu za nje-zinazojulikana kama kondomu za kiume- ni njia maarufu sana ya kuzuia mimba na kukinga magonjwa ya zinaa (STIs). Ingiza tu kwenye uume. Kondomu za nje (kiume) zinapunguza hatari ya magonjwa ya zinaa (STI) kwa kuweka mbegu za kiume ndani ya kondomu na nje ya uke, mkundu au mdomo. (Pia kuna kondomu za ndani (kike) ambazo zinaingizwa ndani ya uke au mkundu.) Kondomu za nje (kiume) zinakuja kwa mamia ya umbo na ukubwa. Pia unaweza zinunua na mafuta ya kulainisha au bila.

Aina za kondomu za nje (kiume):

Zilizo na dawa za kuuwa mbegu za kiume (spermicide). Kondomu hizi zinalainishwa na kemikali ya kuuwa mbegu za kiume. Hazipendekezwi kwa ngono ya mdomo au ngono ya mkundu

Bila dawa za kuuwa mbegu za kiume. Ikiwa wewe au mwenzi wako mna mzio wa dawa za kuuwa mbegu za kiume, tafuta kondomu bila dawa za kuuwa mbegu za kiume. Kondomu zina madhara chache sana. Aina hii chache zaidi.

Ulimbo wa mpira ( latex). Kondomu za ulimbo wa mpira zinaweza nyooka hadi asilimia 800. Hii ndio aina inayotumika sana. Lakini usizitumie na mafuta za kulainisha yenye oili. Oili inaweza kufanya kondomu ipasuke au iteleze, na kuongeza hatari ya mimba au magonjwa ya zinaa.

Bila ulimbo wa mpira. Ikiwa una mzio wa ulimbo wa mpira au unapenda mafuta za kulainisha zenye oili, basi tumia kondomu sizizokuwa na ulimbo wa mpira. Zinatengenezwa kwa kile kinaitwa polyurethane na nyenzo zingine bandia za kiteknolojia au ngozi asilia ya mwanakondoo.

Maelezo

[10]
Kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa (STIs). Kondomu za nje (kiume) nyingi zitakukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa ikiwemo virusi vya ukimwi (VVU). Kondomu iliyotengezwa na ngozi ya mwanakondoo ndio aina pekee usitegemee itakukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa. Zinazuia mbegu za kiume lakini sio maambukizo.

Kondomu za nje (kiume) zinahitaji jitihada na kujitolea. Mwanamume anahitaji kuiingiza kwenye uume vizuri kila wakati, iwe nini, ili ziwe na ufanisi. katika maeneo zingine, inaweza kuwa ngumu kwa wanawake waombe wenzi wao wa kiume watumie kondomu kila wakati na vizuri.

Inaweza kusaidia ngono iende muda mrefu zaidi. Kondomu za nje ( kiume) zinaweza kupunguza hisia za ngono. Wakati mwingine hili ni jambo mzuri. (ikiwa wewe au mwenzi wako mna tatizo la kumwaga haraka, kondomu zinaweza kusaidia ngono yenyu kuenda muda mrefu)

Bei nafuu na rahisi kupata. Kondomu za nje (kiume) ni za bei nafuu na pia unaweza zipata bure wakati mwingine. Unaweza kuzipata karibu kila mahali. Kuna aina nyingi za kuchagua.

Hauhitaji agizo la daktari. Ikiwa huwezi fika kwa mtoaji huduma za afya au hutaki kuenda, unaweza kutumia kodomu za nje (kiume).

Hazifai ukiwa una mzio wa ulimbo wa mpira ( latex). Ikiwa una mzio wa ulimbo wa mpira, utahitaji kutumia kondomu ya nje (kiume) bila ulimbo wa mpira. Ikiwa huwezi pata kondomu bila ulimbo wa mpira, jaribu njia ingine.

Jinsi ya kutumia

Kondomu za nje (kiume) ni rahisi kabisa kutumia. Tuna vidokezi hapa chini ya kuku kumbusha jinsi ya kuzitumia vizuri. Na kumbuka-ikiwa unatumia kondomu pekee,lazima ukumbuke kuzivaa KILA WAKATI unapofanya ngono.

 

Jinsi ya kuvaa kondomu ya nje (kiume) :[9]

 1. Kwanza, usiwe na haya. Kuvaa kondomu ya nje (kiume) inaweza kuwa sehemu ya kuongeza tamaa ya kingono kabla ya kuingiza uume kwenye uke. Ikiwa unaweza kuzungumza na mwezi wako kuhusu ngono, zungumza kuhusu jinsi mnavyoweza kutumia kondomu kuongeza ridhaa kwa maisha yenyu ya ngono.
 2. Angalia tarehe ya mwisho kutumika kabla ya kutumia kondomu. Kondomu zinaweza kuharibika. Kondomu ambazo zimepita tarehe ya mwisho kutumika hupasuka haraka.
 3. Hakikisha umevaa kondomu kabla uume uguse uke. Manii- majimaji mbayo hukota kwenye uume kabla ya mwanaume kufika kilele na kumwaga-inaweza kuwa na mbegu za kiume zilizobaki wakati wa mwisho mwanaume alimwaga.
 4. Kondomu moja kwa uume mmoja uliosimama. Hakikisha kwamba una kondomu za ziada. Usitumie tena kondomu ambayo ilishatumika.
 5. Kuwa mwangalifu usirarue kondomu wakati unaitoa kwenye pakiti. Ikiwa imeraruka, gumu lakini nyepesi, au haikunjiki, itupe. Tumia ingine.
 6. Unaweza kuweka mafuta kidogo ya kulainisha yenye haina oili, ndani ya kondomu. Itasaidia kondomu kuingia laini na kukupa wewe na mwenzi wako furaha ya ngono.
 7. Ikiwa mwanamume hajatahiriwa, ni muhimu kuvuta nyuma ngozi ya mbele inayofunika uume kabla ya kuingiza kondomu kwa kuibingirisha.
 8. Ukishaingiza, wacha nafasi ya nusu inchi kwenye ncha ya kukusanya manii, kisha chuna ncha ili hewa itoke.
 9. Kunjua kondomu ukiisukuma ifunike uume hadi mwisho inapoweza kufika.
 10. Lainisha kutoa matone ya hewa, kwasababu yanaweza kufanya kondomu ipasuke kwa urahisi.
 11. Ukipenda, tumia mafuta ya kulainisha ili kupunguza maumivu.

 

Jinsi ya kuvua kondomu ya nje (kiume)[3]:

 1. Hakikisha uume uko nje ya uke kabla haujalegea.
 2. Ni muhimu kushika sehemu ya mwisho ya kondomu mwanamume anapo toa uume wake. Hii itazuia manii ndani ya kondomu kumwagika.
 3. Itupe kondomu. Iweke mbali na watoto au wanyama zipenzi. Usiitupe kwenye choo cha maji. Itaziba mifereji.
 4. Uume unastahili kuoshwa kwa sabuni na maji kabla ukaribiane na uke tena.

 

 

Madhara

Kila mtu ni tofauti. Kile unachopitia pengine hakitafanana na mtu mwingine.

Mambo chanya: Kuna vitu vingi kuhusu kondomu ya nje (kiume) ambavyo ni vizuri kwa mwili wako na pia maisha yako ya ngono[9]

 • Inakinga dhidi ya magonjwa ya zinaa, ikiwemo virusi vya ukimwi VVU
 • Bei nafuu na rahisi kupata
 • Hauhitaji agizo la daktari
 • Inaweza kusaidia kwa tatizo la kumwaga haraka

Mambo hasi:[5]

 • Isipokuwa uwe na mzio wa ulimbo wa mpira ( latex) , kondomu za nje ( kiume) hazileti madhara kwa mwili.
  • Ni mtu 1 au watu 2 kati ya watu 100 walio na mzio huu. Ikiwa wewe ni mmoja wao, beba kondomu ambazo sio za ulimbo wa mpira badala yake.
 • Watu wengine wana mzio kwa aina fulani ya mafuta ya kulainisha. Hili likifanyika, jaribu aina nyingine ya kondomu.
 • Wanaume wengine hulalamika kwamba kondomu hupunguza hisia za ngono
 • Ukiwa mlevi, unaweza kusahau kutumia kondomu. Hata hivyo, ukiziweka karibu, unaweza kukumbuka.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tuko hapa kukusaidia. kama bado unahisi sio ya kufaa, tuna mawazo ya njia zingine. Kumbuka tu: Ukiamua kubadilisha njia, hakikisha una kinga wakati unafanya mabadiliko. Kondomu zitakupa kinga bora wakati unatafuta njia itakayofaa mahitaji yako.

Je, kondomu za nje (kiume) zitapunguza hisia za ngono za mwanamume? [5]

 1. Jaribu kondomu za kampuni tofauti tofauti au aina tofauti, kama itasaidia. Pia zingatia kondomu zinazosemekana ni “nyembamba kuzidi mno” au “ya kusisimua kuzidi mno”
 2. Bado haiendi sawa? Jaribu njia ambayo unaweza “kusahau kuhusu” kwa muda kama vile IUD, Vipandikizi, sindano, pete, or kiraka.
  • Hizi njia zingine hazitakukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa (STIs). Kwahivyo, ukitaka kinga dhidi ya STI, jaribu kondomu ya ndani (kike) badala yake.

Jaribu njia tofauti:

Vipandikizi; IUD; kiraka; pete,; sindano

Kwanini kondomu ya nje (kike) inashinda ikiteleza au/ na kupasuka? [8]

 • Hakikisha unaangalia tarehe ya mwisho kutumika kabla kutumia kondomu. Angalia pakiti kuhakikisha haijaharibiwa.
 • Kunauwezekano kwamba hauivai inavyofaa. Tazama sehemu ya Jinsi ya kuvaa kondomu.
 • kuna uwezekano kwamba mwanamume anatoa uume ukisha legea.
 • Bado haiendi sawa? Zingatia njia ambazo hazizui manii kama vile kiraka, tembe, pete, IUD, Vipandikizi, or sindano.
  • Hizi njia zingine hazitakukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa (STIs). Kwahivyo, jaribu kondomu ya ndani (kike)badala yake. Au jaribu tena kupata kondomu ya nje (kiume) ambayo inakufaa. Kunazo aina tofauti huko nje.
 • Jaribu njia tofauti: kondomu ya ndani (kike); Vipandikizi; IUD; kondomu; kiraka; tembe,; pete; sindano

Je, kondomu mbili ni bora kuliko moja kwa kukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa na kuzuia mimba?[10]

Na ikiwa mwenzi wangu ana mzio wa ulimbo wa mpira(latex)?[8]

 • Visa vya watu kuwa na mzio wa ulimbe wa mpira ni vichache, lakini viko. Ikiwa wewe au mwenzi wako mna mzio wa ulimbe wa mpira, tafuta kondomu bila ulimbe wa mpira ili kujikinga dhidi ya mimba na magonjwa ya zinaa. Kondomu za nje (kiume) zilizotengenezwa na ngozi ya mwanakondoo ni njia ingine ya kuzuia mimba, lakini hazikingi dhidi ya magonjwa ya zinaa (STI).
 • Jaribu njia ingine: kondomu ya ndani (kike)

Na ikiwa kondomu yangu ya nje (kiume) imepita tarehe ya mwisho kutumika?

 • Hakikisha unaangalia tarehe ya mwisho kutumika kabla kutumia kondomu. Angalia pakiti kuhakikisha haijaharibiwa.
 • Kuhakikisha kwamba kondomu yako bado ni nzuri, finya pakiti- unapaswa kuhisi ikiwa na hewa.Ikiwa unaweza kuhisi hewa, inamaanisha kwamba pakiti haijaharibiwa au tobolewa.
 • Unapofinya pakiti,tafuta utelezi wa mafuta ya kulainisha. (hii haitakuwa kwa kondomu bila mafuta ya kulainisha). Kondomu zikiwachwa kwenye joto au zikitobolewa,mafuta ya kulainisha itakauka au itavuja na kusababisha kondomu kukauka, na kuifanya dhaifu na kuongeza uwezo wake wa kupasuka wakati wa matumizi.
 • Ikiwa kondomu imepita tarehe ya mwisho kutumika au pakiti imeharibika, tumia kondomu mpya.
 • Hifadhi kondomu zako pahali tulivu, pakavu.
 • Jaribu njia tofauti: Vipandikizi; IUD; Tembe; Pete; Sindano

Na ikiwa nina kondomu za nje (kiume) zenye ladha pekee? [5]

 • Watu wengine wanapenda kondomu zenye ladha kwa ngono ya mdomo. Zinaweza kusaidia kuzuia magonjwa ya zinaa kushika koo lako.
 • kondomu zingine zenye ladha huwa na sukari. Sukari hii huweza kusababisha maambukizi ya chachu. Tafuta kondomu bila sukari.

Na ikiwa mwanamume hapendi kutumia kondomu? Anasema zitamfanya akose kusimama..

 • Ikiwa kondomu inabana sana au haistarehishi, mwanamume anaweza kosa kusimama. Wewe sio chanzo; Ni kondomu. Usione aibu.
 • Epuka kondomu za kubana sana au ambazo hazistareheshi kwa kujaribu kondomu za aina tofauti.

Je, nahitaji kutumia mafuta ya kulainisha kwa kondomu? [3]

 • Kutumia mafuta ya kulainisha kwa kondomu kunaweza kuongeza furaha ya ngono. Pia kupunguza usumbufu na uwezekano wa kondomu kufeli. kondomu nyingi huja na mafuta ya kulainisha, lakini unaweza ongeza kidogo. Jaribu kuepuka mafuta ya kulainisha yenye oili ( kama vile mafuta ya kusinga, losheni ya mikono na vaseline) kwasabu zinaweza sababisha kondomu kupasuka.

 

References

[1] CATIE Canadian AIDS Treatment Information Exchange. (2013). Condoms for the prevention of HIV and STI transmission. Toronto . Retrieved from https://www.catie.ca/ga-pdf.php?file=sites/default/files/condoms-en.pdf
[2] Dr Marie Marie Stopes International. (2017). Contraception. Retrieved from http://www.mariestopes.org.au/wp-content/uploads/Contraception-brochure-web-200417.pdf
[3] FPA the sexual health charity. (2019). Your guide to condoms. Retrieved from http://www.fpa.org.uk/sites/default/files/condoms-external-and-internal-your-guide.pdf
[4] Festin MR. (2013). Non-latex versus latex male condoms for contraception.The WHO Reproductive Health Library; Geneva: World Health Organization. Retrieved from https://extranet.who.int/rhl/topics/fertility-regulation/contraception/non-latex-versus-latex-male-condoms-contraception
[5] IPPF and UNFPA. (2010). MYTHS, MISPERCEPTIONS AND FEARS: ADDRESSING CONDOM USE BARRIERS. New York . Retrieved from http://bibliobase.sermais.pt:8008/BiblioNET/Upload/PDF4/002988.pdf
[6] Lopez, et al. (2014). Behavioral interventions for improving condom use for dual protection. Cochrane Database of Systematic Reviews 2013, Issue 10. Art. No.: CD010662. DOI: 10.1002/14651858. CD010662.pub2 Retrieved from https://extranet.who.int/rhl/topics/fertility-regulation/contraception/behavioural-interventions-improving-condom-use-dual-protection
[7] Stover, et al. (2017) The case for investing in the male condom. PLoS ONE 12(5): e0177108. Retrieved fromhttps://journals.plos.org/plosone/article/file?id=10.1371/journal.pone.0177108&type=printable
[8] Society of Obstetricians and Gynaecologists of Canada. (2015). Canadian Contraception Consensus Chapter 5: Barrier Methods. JOGC Journal of Obstetrics and Gynaecology Canada , 37. Retrieved from https://www.jogc.com/article/S1701-2163(16)39376-8/pdf
[9] Shoupe, D. (2016). Barrier Contraceptives: Male Condoms, Vaginal Spermicides, and Cervical Barrier Methods. En D. Shoupe, The Handbook of Contraception: A Guide for Practical Management. Retrieved from http://eknygos.lsmuni.lt/springer/677/147-177.pdf
[10] World Health Organization Department of Reproductive Health and Research and Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (2018) Family Planning: A Global Handbook for Providers. Baltimore and Geneva. Retrieved from https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/260156/9780999203705-eng.pdf?sequence=1
[11] World Health Organization. (2016). Selected practice recommendations for contraceptive use. Geneva. Retrieved fromhttps://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/252267/9789241565400-eng.pdf?sequence=1


lang Kiswahili