Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

Yote unayostahili kujua kuhusu uelewa wa kizazi kama njia ya uzuiaji mimba

Je unafanya ngono mara kwa mara? Unatumia njia gani ya uzuiaji mimba? Umesikia kuhusu njia ya uelewa wa kizazi?
Wanawake wengi duniani kote wanafanya ngono kwa sababu tofauti na kupata watoto. Hawataki watoto. Wanafanya ngono kwa kupata furaha , kupata uhusiano,anasa, na sababu zingine tofauti.  

Kwanini unafanya ngono? Na ikiwa wewe ni mmoja wa wanawake hawataki mtoto, unafanya nini kuzuia mimba

Nawajua wanawake ambao hutegemea uelewa wa kizazi kuzuia mimba. Wanawake wengine wazee watakuambia wametumia njia hii kwa miaka  na ikawasaidia. Wengine watakuambia ilifeli na wakaamua kuzaa tu au walitoa mimba. Ukweli ni kwamba, kama tu njia zingine za uzuiaji mimba, njia ya uelewa wa kizazi haina ufanisi wa asilimia 100 kuzuia mimba. Ina mambo mazuri na mabaya na katika makala hii, nitakueleza jinsi inaweza kutumika  kuzuia mimba, na jinsi inaweza kufeli.

Tracking menstrual cycle-fertility awareness-ovulation-Cropped shot of a young woman lying on her bed with her eyes closed

Njia ya uelewa wa kizazi huzuia mimba vipi?

Kila anayepata hedhi huwa na siku salama (Siku mwili haina rutuba) na siku zisizo salama (siku mwili ina rutuba) za kufanya ngono na kuwepo na uwezo wa kushika mimba. Nadhani ulijua hili tayari! Kulingana na njia ya uelewa wa kizazi, siku zisizo salama ni pamoja na siku ya kupevuka kwa yai na siku chache kabla na baada ya siku hio. Siku zingine zote zikiwemo siku za hedhi huchukuliwa kama siku salama kufanya ngono bila kuwa na wasiwasi wa kushika mimba. 

Kwahivyo, kutumia njia ya uelewa wa kizazi, unahitaji kuchunguza mzunguko wa hedhi yako na kutambua siku zisizosalama  na kuepuka ngono siku hizo. Ukiwa na ngono siku hizo, tumia njia zingine za uzuiaji mimba kama vile kondomu, diaframu n.k. kuzuia mimba. 

Tracking menstrual cycle-fertility awareness-ovulation-On 2020 Calendar book,Female'hand of planner writing daily appointment.Woman mark and noted schedule(holiday trip) on diary at office desk.Calendar reminder event for planner concept

Siku zisizo salama:

Imekadiriwa kwamba mwanamke hupevuka yai katikati wa mzunguko wa hedhi na yai huachiliwa na huweza baki saa 12-48 kabla kufa. Kwahivyo siku mbili katika mzunguko wa hedhi ( katikati) zinachukuliwa kutokuwa salama.

Pia, manii ikimwagwa ukeeni, inabaki kwenye njia ya kizazi hadi siku tano kabla kutoka. Kwahivyo, siku kabla ya siku ya kupevuka kwa yai zinachukuliwa kutokuwa salama.

Kwahivyo kulingana na urefu wa mzunguko wa hedhi (kati ya siku 25 hadi siku 35), siku zisizo salama zitakuwa siku ya 8 na siku ya 19 ya mzunguko.

Kumbuka: Jinsi ya kutambua namba ya siku inalingana na urefu wa mzunguko wa hedhi wa kila mtu.Ikiwa una mzunguko wa kawaida wa siku 28, siku zako za kupevuka kwa yai zitakuwa siku ya 14 na siku ya 16 na ikiwa una mzunguko wa siku 31, siku zako za kupevuka kwa yai zitakuwa kati ya (siku 16 na siku 18)

Siku salama:

Ikiwa siku zisizo salama ni kati ya (siku 8 na siku 19), siku salama huanza  siku ya 1 ya hedhi yao (wakati hedhi inaanza) hadi siku ya 7  alafu kutoka siku ya 20 hadi siku ya 7 ya mzunguko wa kufuatiia.

Mentruation cycle safe days unsafe days fertile days infertile days period days

Mambo mazuri ya njia ya uelewa kizazi

Wanawake wengi hawapendi kutumia njia za uzuiaji mimba kwasababu zinawaletea madhara. Hawataki kuongeza uzani, kupata chunusi, kuwa na hisia zinazobadilika badilika na kupata hedhi  zisizotabirika, kwahivyo wanataka njia ambayo haitaleta madhara. Ikiwa wewe ni mmoja wa wanawake hawa, njia ya kalenda itakuwa bora kwako.

Ukweli ni kwamba, katika hali bora zaidi, ukitumia njia ya uelewa kizazi na uepuke kufanya ngono bila kinga siku zisizo salama, utaweza kuzuia mimba hadi wakati utakuwa tayari. Unahitaji tu kuchunguza mzunguko wako wa hedhi  ili kukuwa na uhakika wa siku za kupevuka kwa yai. Kitu kimoja unachoweza kufanya ni kuchunguza mzunguko wa hedhi kwa miezi 6 na ubaini muda wake ili kukuwa na kazi rahisi. Mambo ya kuchunguza kwa rahisi ni kama:

  • Dalili za kupevuka kwa yai

Wanawake wengine huwa na bahati   kujua wakati wao wa kupevuka kwa yai kwasababu ya joto ya mwili kupanda, kutokwa damu/ matone ya dama wakati wa kupevuka yai, ute wa shingo ya kizazi, maumivu ya hedhi, kuongezeka kwa tamaa ya kufanya ngono na mengine. Kuchunguza dalili hizi kwa miezi kadhaa (6 ikiwa bora) kutakufanya kujua mzunguko wako.

Happy Asian Lover kissing and hugging on the bed in bedroom at home, Couple and life style concept,

  • Vifaa vya kupima kupevuka kwa yai

Kama tulivyo na vifaa vya kupima mimba, tuna vifaa vya kupima kupevuka kwa yai. Vinahitaji kupima mkojo; na unaweza kujua kutoka kwa matokeo ikiwa siku yako ya kupevuka kwa yai inakaribia. Kwa bahati mbaya, vifaa huenda vikose kufanya vizuri kwa watu walio na polycystic ovary syndrome- hali ya yai kutowachiliwa mara kwa mara inavyofaa.

  • Shanga za mzunguko wa hedhi

Hii ni njia ya kitambo ya kuchunguza mzunguko wa hedhi ambayo inawapa  wanawake kazi rahisi. Shanga ina ushanga za rangi ya kahawia, nyeupe, moja nyekundu na pete inayosonga. Ushanga za kawahia zinasimamia siku salama, ushanga nyeupe zinasimamia siku zisizo salama, na ushanga nyekundu inasimamia siku ya kwanza ya hedhi yako. Kuitumia, songesha pete juu ya shanga, ushanga moja kila siku. Hedhi ikianza, songesha pete juu ya ushanga nyekundu. Siku inayofuata, isongeshe juu ya ushanga moja kahawia na uisongeshe kila siku. Pete ikisonga juu ya ushanga kawahia, unajua uko salama na ikiwa juu ya ushanga nyeupe, unajua hauko salama.

Tazama picha hizi kuelewa jinsi shanga  ya mzunguko wa hedhi hufanya kazi.

  • Programu za simu za hedhi

Na ubunifu wa simu njanja, kuchunguza hedhi kumerahisishwa na programu za simu za hedhi. Kila mtu ninayemjua ana programu ya simu ya hedhi kwasababu inatoa uzito wa kuhesabu. Kile unahitaji kufanya ni kufungua programu na kuingiza siku ya kwanza na ya mwisho wa hedhi yako na programu itafanya kazi iliyobaki. Itakuonyehsa siku zako salama na siku zisizo salama.

Mambo mabaya ya njia ya uelewa kizazi

Njia ya uelewa kizazi ina ufanisi wa asilimia 80-87 wa kuzuia mimba. Hili linamaanisha kuna uwezekano wa asilimia 13-20 wa kupata mimba ukitumia njia hii. Ni kwanini?

Hata ikiwa kufuata mzunguko wako wa hedhi vizuri na kutumia njia zingine za uzuiaji mimba siku mwili wako una rutuba kunaweza kuongeza ufanisi wa njia hii, bado hakuna njia hakika kabisa ya kujua wakati haswa mtu anapopevuka yai. Wanawake wengine hujua siku hizi kwa urahisi wakati wanawake wengine hupata shida kuzijua. Pia, kuna sababu kadhaa ambazo zinaweza kufanya njia ya uzuiaji mimba kufeli wakati mtu anatumia njia ya uelewa kizazi. Ni kama yafuatayo:

  • Mzunguko wa hedhi ambao hautabiriki

Njia ya uelewa kizazi huwa na ufanisi wa juu ikiwa mzunguko wa hedhi unatabirika kwasababu itakuwa rahisi kujua siku mwili una rutuba na kutambua siku salama na siku zisizo salama.

  • Kuchelewa kwa kupevuka kwa yai

Mambo kama kuwa na wasiwasi, dawa, hali ya anga, ugonjwa, ukomo wa hedhi, na kunyonyesha kunaweza kuchelewesha kupevuka kwa yai. Au kuisababisha kufanyika mapema kinyume na matarajio. Hali hii inaweza kufanya uchunguzi uwe mgumu  na mwanamke anaweza kushika mimba akifanya ngono siku anadhani ni salama kumbe sio salama.

Tracking menstrual cycle-fertility awareness-ovulation-Teenage girl holding medical mask and laying on bed using smartphone. Self-quarantine. Coronavirus quarantine concept.

  • Matokeo ya kipimo ya kupevuka kwa yai yasio sahihi

Hata ikiwa vifaa vya kupima siku za kupevuka kwa yai hufanya kazi vizuri, wakati mwingine matokeo huwa hayatoki sahihi. Hili linaweza kumfanya mwanamke afanye ngono bila kinga siku ambazo sio salama

  • Kupevuka yai zaidi ya mara moja kwa mwezi

Katika hali zingine nadra sana, wanawake huwa na wakati zaidi ya moja kwa mwezi wa kupevuka kwa yai. Inaweza tokea mara mbili au tatu. Hili linaweza kufanya njia ya uelewa kizazi kufeli kwasababu inatambua tu yai kupevuka mara moja kwa mwezi, sio zaidi.

Tukishasema hayo, tafadhali kumbuka kwamba njia ya uelewa wa kizazi bado ni chaguo nzuri. Ni muhimu kuelewa jinsi ya kuitumia ili isifeli. Pia, zaidi ya mimba, zingatia kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa.

Je, una jambo la kusema?Wacha ujumbe wako hapa chini, wasiliana nasi kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii:  Facebook, Instagram na Twitter u tutumie barua pepe kwenye info@findmymethod.org. Kwa taarifa zaidi kuhusu njia za uzuiaji mimba, tembelea  findmymethod.org

Kuhusu mwandishi: AmiShikah ni mtaalamu wa afya ya kijinsia na kizazi. Anazungumzia ngono kwenye tovuti yake na maswala ya kijinsia kwenye podcast yake inayoitwa Sex and Sanity.