Njia za uzuiaji mimba baada ya kujifungua

Njia za uzuiaji mimba baada ya kujifungua

Una mimba! Una furaha, una wasiwasi, umesisimka, na unajitayarisha kwa maisha mapya.
Kati ya hizi hisia zote (na homoni)-huenda usifikirie mambo ya njia za uzuiaji mimba baada ya kujifungua. Lakini hauwezi kutaka kushika mimba isiyopangwa punde baada ya kujifungua.

Lakini unaweza kupata shida kuamua ni njia gani ya uzuiaji mimba utumie. Ni njia gani salama kwako na mtoto? Ni kwa njia gani kunyonyesha mtoto huathiriwa na njia za uzuiaji mimba? Ni lini unaweza kuanza kutumia njia ya uzuiaji mimba? Ahhh—Kuna mambo mengi ya kufikiria!

Tunaelewa haya. Ndio kwa maana timu ya Find My Method imeamua kuweka mwongozo huu kukusaidia kuchagua njia inayokufaa.

Nikishajifungua, ni baada ya muda mgani napaswa kutumia njia za uzuiaji mimba?

Wanawake wengi hupata rutuba tena punde baada ya kujifungua, kwahiyo kuamua njia ya uzuiaji mimba utakayo tumia kabla ya kurudi na mtoto nyumbani kutakupunguzia wasiwasi na kurahisisha kazi yako.

Baada ya kujifungua, ni bora ungoje angalau mwaka 1- weledi wengine husema miaka 2- kabla ya kushika mimba tena. Hili linaipa mwili wako muda wa kupona na kukuwezesha kumtunza mtoto wako mchanga. Kwa bahati nzuri, kuna aina nyingi za njia za uzuiaji mimba ambazo ni salama kutumia punde baada ya kujifungua na hata wakati unanyonyesha.

Ikiwa unataka kuanza punde baada ya kujifungua, jaribu njia hizi

IUD ya shaba au IUD ya homoni

IUD ya shaba na ya homon ni za kufaa, salama na zenye ufanisi- na aina zote mbili za IUD zinaweza kuingizwa punde baada ya kujifungua. IUD ikiingizwa punde baada ya kujifungua, tuwezekano wake wa kutoka uko juu zaidi kushinda ukiingiza baada ya wiki kadhaa,, lakini ina faida kwamba hautahitaji kupanga kurudi kwa daktari.

Vipandikizi

Ni rahisi sana na salama kutumia vipandikizi punde baada ya kujifungua. Ukilazwa hospitalini kwa siku chache, vipandikizi vinaweza kuingizwa wakati wowote kabla utoke hospitalini.

Sindano

Katika hospitali mingi ni rahisi kupata sindano kabla ya kuruhusiwa urudi nyumbani, kwahivyo ni chaguo bora kwa kinga ya muda mfupi au muda mrefu. Kwa vile madhara ya sindano yanabaki hadi wiki 12, unaweza kuiweka wakati unatoka hospitalini kisha wakati unarudi kliniki baada ya wiki 6 ubadilishe utumie njia ingine.

Tembe (projestini pekee) au POPs

Ikitumika saa sawa kila siku, POPs hufanya vizuri kwa wamama waliojifungua karibuni na hazileti shida yoyote ukinyonyesha. Inaweza kutumika na mwanamke yeyote, ikiwemo vijana na wanawake walio na umri wa miaka zaidi ya 40. Na una udhibiti kamili ukitumia njia hii, unaweza wacha kuitumia wakati wowote unataka.

Kondomu (ya miili ya wanawake na wanaume ) pia ni salama na inaweza kutumika ndani ya kipindi hiki. 

Ulijua kwamba kunyonyesha pia kunaweza kutumika kama njia ya uzuiaji mimba? Pia huitwa “Lactational Amenorrhea” njia hii hutegemea hali ya ukosefu wa rutuba wakati wa kunyonyesha. Wakati mwili wako unatengeneza maziwa, homoni inayoitwa prolaktini inaongezeka mwilini mwako na kuzuia kupevuka kwa yai. Lakini ukichagua njia hii hakikisha unaielewa vizuri; Ina ufanisi wa juu miezi 6 ya kwanza baada ya kujifungua, bora hedhi yako haijarudi na unanyonyesha mtoto bila kumpa vyakula vingine vyovyote ( yaani humlishi mtoto maziwa au vyakula vingine vya watoto)

Baada ya wiki 3 ikiwa haunyonyeshi au baada ya wiki 6 ikiwa unanyonyesha

Mchangano wa tembe za uzuiaji mimba 

Ina viwango vidogo vya projestini na estrojeni na huzuia ovari kuwachilia yai. Tumia tembe moja kila siku na uanze kifurishi kipya kwa wakati unaofaa ili upate ufanisi, na pia, unaweza kuanza kutumia tembe hizi wakati wowote wa mwezi na uwache kuitumia wakati wowote ukitaka.

Kiraka

Kifaa hiki kidogo, chembamba na chenye umbo la mraba kitazuia mimba na unaweza kuiweka kwenye mgongo, tumbo, fumbatio, n.k. Tumia kiraka kipya kila wiki 3, na wiki ya 4 usiweke kiraka.

Baada ya wiki ya 6
Ni bora uepuke diaframu na kofia ya kizazi kwa angalau wiki 6 baada ya kujifungua kwasababu mabadiliko ya kawaida yanayoletwa na mimba huweza kufanya vifaa hivi visiingie sahihi vinavyofaa. Uke hubadilika kidogo baada ya kujifungua, kwahivyo hata dawa za kuuwa mbegu za kiume hazipendekezwi.

Njia ya homoni ama bila homoni?

Usiamini uongo zozote kwamba mwanamke anayenyonyesha hawezi kutumia njia ya uzuiaji mimba yenye homoni! Kuna tafiti zilizothibitishwa zinazo onyesha kwamba hazitakudhuru au mtoto wako. Njia zote zilizo orodheshwa,ziwe za homoni au bila homoni, ni salama kabisa kutumia.

Kwa wiki za kwanza baada ya kujifungua, usitumie njia ya uzuiaji mimba yenye ina homoni ya estrojeni (k. v. tembe, kiraka au pete). Baada ya wiki 3, unaweza anza kutumia njia yoyote kati ya hizi.

Jua zaidi kuhusu njia mashuhuri zaidi za uzuiaji mimba baada ya kujifungua:

IUD ya homoni

Sindano

Vipandikizi

Unatafuta suluhisho la muda mrefu, wastani au mfupi?

Ukitaka kungoja muda mrefu kabla ya kushika mimba tena, au ikiwa hautaki mtoto mwingine, IUD ya shaba itakuwa chaguo bora kwako. Zina ufanisi wa asilimia 99% na ikiwa unataka kushika mimba tena, unahitaji tu kuitoa. IUD haziathiri rutuba yako.

Ukitaka kungoja miaka 3-5 kabla ya kushika mimba tena, zingatia IUD ya homoni au Vipandikizi. Vinaweza kupunguza maumivu ya hedhi na pia kufanya hedhi uwe mwepesi, wanawake wengine wanaweza kosa hedhi kabisa na vina ufanisi wa hali ya juu.

Ikiwa unatafuta njia ya muda mfupi au wa kutumika kwa muda tu, sindano au POP zinaweza kukufaa.

Ukitumia sindano, utahitaji kuenda kwa daktari kila miezi 2 au 3, na kwasababu ni ya kudungwa, ni njia ya siri kabisa. POP ina ufanisi ikitumika saa sawa kila siku na unaweza kuanza kuitumia au kuwacha kuitumia wakati wowote unataka.

Kujua zaidi, tembelea findmymethod.org na ujaribu kurasa wetu wa kutafuta njia za uzuiaji mimba. Kulingana na kile unachotaka kwa mwili wako na maisha yako, unaweza kulinganisha njia tofauti kabla uaume ni kipi kitakufaa.

Ukiwa na maswali, usisite kuwasiliana nasi kwenye mitandao yetu ya kijamii Facebook, Instagram na Twitter, au ukipenda, tuma barua pepe kwenye info@findmymethod.org


References: